Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Hbr za siku tele.

Narudia kusema kuwa, nilichopongeza ni jamii kumiliki ajenda. Kila siku tunasema kuwa community participation and ownership. Ndiyo hii sasa. Kama wamemiliki, hii ni hatua ya kwanza nzuri kabisa kama wanavyomiliki ajenda za kujenga shule, zahanati, kuchonga barabara nk. Mbona wanapomiliki wanaanza wanakosea wanarekebishwa wanaenda mbele? Hivyo hivyo, hata kwenye ajenda za jamii tuwapongeze kwa kumiliki na tuwafuatilie tuwape semina na kuwajengea uwezo Wamiliki vzr kwa tija. Sasa mkiona pongezi zimetolewa wengi mnaona negativity tu kuliko positivity. Je uta bond vipi na jamii for change ikiwa tunayaona mabaya tu pasipo mema?

Mm nawapongeza kwa kumiliki ajenda hii na ndiyo mwanzo wa safari ya mabadiliko chanya kwa msaada wa maafisa wa Maendeleo na Ustawi walioko huko.

Ahsante Sana .. kwa maoni .. tuendelee na kuelimishana....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Safi sana mh Waziri,tunataka jamii zinazojitambua
 
Kwa hiyo una watetea hao wanao vaa vichupi na vitaiti na kutembea navyo barabarani [emoji848] au na wewe ni mmoja wao[emoji848] Kwani kuna faida gani mtu ukivaa nasu uchi na kutembea hadharani [emoji848] sio Kila kitu kwa sababu wazungu wanafanya basi na nyie huku uswahilini mfanye mnaonekana kama wendawazimu, kwani mkivaa kwa kujistili vizuri kuna madhara yoyote mnapata [emoji848] kama unaona ni Sheria za kijinga hamia Marekani ambako hata ukitembea uchi wa mnyama hakuna atakae kuwaza

Tena waziri uangalie na mziki wa bongo flavor kwa jicho la tatu kwa sababu kuna wasanii ni chanzo kikubwa cha uvunjifu wa maadili, Kila siku kwenye nyimbo zao wana hamasisha kunywa pombe na kuvuta bangi bila kusahau ngono tena hadi ngono ya kinyume na maumbile, lakini cha ajabu kwenye mikutano yenu ya kiasa ndio mnawaita kutumbuiza na wanaimba hizo nyimbo zao ambazo kama una akili timamu huwezi kusikiliza ushenzi wanao tamka humo ndani, wanapaswa kushughulikiwa kabisa hao wapuuzi [emoji35][emoji35]
Ahsante Sana kwa mchango wako. Tayari tumeimarisha umoja na BASATA na COSOTA na Bodi ya FILAMU katika hili. Naamini safari yetu ya kuimarisha mifumo husika itaenda salama na kudhibiti haya mambo. Tayari ma MC na maafisa utamaduni wamepelekewa maelekezo ya kukumbushwa wajibu wao ambao uko kwenye mipango yao ila sijui kwa nn baadhi ya watu wanaishi hadi wakumbushwe. Ila tutafika.

Ngoja nitafute picha hapa ya 12 Sept 2023 tulipoanzia safari.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru sana uongozi wa kijiji kizima kwa kujaribu kujiwekea utaratibu mzuri sana ambao utawezesha Jamii husika kuishi katika maadili, sioni shida kabisa katika hilo, Ndugu Doroth Gwajima, Umefanya vema kuunga Mkono jitihada hizi kwani hii itakua chachu hata kwenye maeneo Mengine mengi, Nina ushahidi usio na shaka kuthibitisha kwamba Uvaaji wa nguo fupi , unyoaji wa viduku pamoja na kushinda vijiweni ni matokeo makubwa ya mmonyoko wa maadili kwani uchochea ukahaba, uvutaji bangi, wizi, pamoja na umaskini , Naombeni sana nifikishieni pongezi kwa Jamii husika kwa kutambua umuhimu wa vijana katika kuliendeleza Taifa.

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
Pongezi zimefika, maana kesho tutakuwa nao.

Sisi hili bara letu, tutasonga mbele tu kwa kupendana na kuamini kuwa Kila mmoja anao mchango anataka kwenda pazuri na Ili afike huko, anahitaji kuanzisha mwendo na apate ushirikiano wa jamii na wataalamu mbalimbali kwenye safari yake Ili afike salama. Ubarikiwe [emoji1666]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hapo unaendelea kunipiga porojo na ngonjera. Ulisema ipo ukanipa ni google, kwenda nakuta mipngo expired. Dah.

Hilo la tajiri na mlinzi mfano mfu huo. Hapo nikutafuta ku "score points" kijinga tu. "I am way ahead of that BS".

Hio habari za bajeti sijuwi ni nini, nazo ni kujitafutia "scapegoat" tu. Kuwa na ubunifu. Mbona jamii yetu matatizo yake mengi (siyo yote) najulikana na mnachoshindwa mpaka sasa ni kuwa wabunifu wa kuyapatia ufumbuzi wa kuyatatua tu. Yaani mnakuwa kama mzazi anaevuta sigara halafu anamwabia kijana wake "usivute sigara ni mbaya kwako", hivi yatamuingia kweli?.

Ndiyo hivyo, bora liende tu.

Yaani mmekaa kujibu kisiasa siasa (yaani uongo uongo tu )na kutowana njiani.

Tuonesheni plan zenu, siyo unanipa mpango wa ofisi ya waziri mkuu uliopitwa na wakati halafu unanambia bado unafanyiwa tathmini uletwe mpya. Ina maana hakuna mpango wowote hapo mnajiendea kimazowea tu. Badilika.

Majibu yako ni "highly contradictive". Tafadhali huku mitandaoni tusipigane porojo, porojo pelekeni bungeni huko. Hapa tunataka facts, kama yapo unasema hili na hili hili ndilo lipo, kama hauna plan, simple tu, sema hatuna plan, lakini tumekuelewa na tutaifanyia kazi, na ukitoa ahadi uifanye kweli.
Nadhani hili nimejibia, kuwa, mpango ni huo phase one ni hiyo Iko online, imetekelezwa imeisha juni 2022. Tathmini imefanyika na wataalamu watafiti wabobezi kuanzia huko ngazi ya jamii Hadi taifa, na Sasa umeshaandaliwa mpango mpya wenye mambo mapya na ubunifu tele tele. Utatoka Novemba 2022 tunaadhimisha hizi siku 16 za kupinga ukatili.

Hivyo kukupeleka google uone wa zamani ni Ili Hadith yetu ya engagement ianzie kwenye background hiyo. Halafu acha nijisifie mwenyewe kuwa, sidhani kama mm ni miongoni mwa watu wapenda porojo Ili nimpoteze mtu... 😅 sidhani. Ila kufikiriwa hivyo napo sawa tu....

Na ukisoma humo ndani utaona role ya wizara ya Jamii ni uratibu wa kisekta, kamati tendaji Iko hapo na Sasa kwa ubunifu tumepanua muundo Ili machinery hii ifanye kazi kitofauti hadi ngazi za mikoa na wilaya. Nisimwage mtama kwenye yaliyomo yasubiri uzinduzi.

Ila msiwe na hasira hasira jamani... hoja ngumu zahitaji utulivu utulivu [emoji847]

Ndugu zangu, nimewaongezea na kapicha la siku ile tumekusanya sekta zote kwenda kujadili tathmini ya MTAKUWWA iliyoisha 2022 na ile ijayo. Someni iliyoisha Ili mje msome na ijayo kisha mje sasa na maoni, mm nitapokea na nitakuja Twitter space kabisa huko huko tuongee mchambue mwanzo mwisho. Ahsante sana FaizaFoxy kwa kuchangia mjadala moto moto kabisa 🤝🇹🇿🔥💪

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Attachments

  • IMG-20231014-WA0007.jpg
    IMG-20231014-WA0007.jpg
    72.3 KB · Views: 2
Hii video ina kila kitu na kinaeleweka . Na ulichofanya kuunga mkono agenda ya wanakijiji cha Olevolos ambacho kiko umbali wa karibu kilometa 10 kutoka Arusha mjini ni jambo jema sana. Na mara nyingi maeneo kama haya ya pembezoni mwa mji kwa nchi yetu huwa kwa asilimia kubwa yanakaliwa na wenyeji wenye asili ya mkoa huo au mji huo walio na mila na desturi zao. Kiasi kwamba mgeni akiingia eneo hilo lazima afuate utaratibu uliopo.

Labda tukumbushane kidogo kuhusu asili yetu.Wote ambao asili yetu ni vijijini mara zote tunapokwenda kusalimia ndugu wa ukoo vijijini nguo za mjini huwa tunaziacha mjini hukohuko. Kwa nini tunafanya hivyo? Bila shaka tunatambua mila na desturi za kila eneo husika. Na kujua mila na desturi za kila eneo ni kujua mavazi na mapambo ambayo yanakubalika kwenye jamii husika katika hicho kijiji. Na hii ipo kwenye vijiji vyote Tanzania. Maeno hayo huwezi kwenda na nguo fupi kama kimini au zile taiti transparent watakushangaa na utaonwa umeenda kuiharibu jamii yao . Na ndio maana akina mama wakiwa wanaenda vijijini huwa wananunua vitenge na kushona mavazi yenye staha na huwezi kuta vijijini uvaaji wa kata K umeshamiri.

Agenda ya kijiji cha Olevolos ipewe heko na iwe mfano kwa vijiji vingine kuweka standards zao . Hizo nguo zikivaliwa bar huko hakuna atakayewafuata .
Amina umefafanua vzr kimantiki kabisa na mifano hai

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwa aina ya mtindo wa maisha ya vijana walio wengi kwa jinsia zote hao wazee kwenye hiko kijiji na msimamo wa waziri dhidi ya ajenda yao hilo nadhani wapo sawa.

Nadhani pia kwa msaada wa serikali na wizara husiki inaweza kuwa mwanzo mzuri wa jamii kuanza wajibu wa kurudisha maadili kwenye jamii husika .

Maoni yalio wasikishwa kwenye mada hii na majibu ya waziri yanatia moyo sana haswa sisi vijana tunao ona vijana wenzetu wakiwa kwenye uvunjifu mkubwa wa maadili kwa kuiga mitindo mibovu kutoka kwa wafu wasio paswa kuigwa .

Tulipo jaribu kuwaambia vijana wenzetu juu y mitindo huo wanayo iga kwamba sio rafiki kwa hatma ya maisha yao walitubeza na kutuona washamba tusioenda na wakati .

Inapotokea hoja na mijadala kama hii na maazimio kutoka Kwa wazee wetu kama hao wanaojadiliwa hapa tunaona mwanzo mzuri wa ujenzi wa maadili mema kwa vijana wenzetu.

Kwenu wizara natumaini mna watendaji na maafisa wenu kwenye wilaya kata na hata vijiji, wanaweza kuwa mabalozi kwa jamii nyingine huko wanako hudumu kuwaeleza kwamba kijiji cha arumeru huko Arusha wamechukua uamuzi wa kurudisha maadili kwenye jamii yao kwa mfumo huu nasi kama serikali ama wizara tukawapa mwongozo huu, mnaweza pia nanyi kuutumia kwa lengo ya kufanya jamii kuwa na maadili .

Hii inaweza kuleta mabadiliko ya namna fulani baada ya miaka kadhaa, tukawa na taifa la vijana wenye maadili na wasio pelekwa na kila aina ya mitindo inayoibuka .

Kwako mh waziri Dkt. Gwajima D pole na hongera kwa uvumilivu wa maoni unayoyapata hapa Jf, sio leo wala kesho utaacha kukutana na maoni yanayovunja moyo, yanayokejeli , yanayoishi na kila namna isioleta furaha, kamwe hakuna jinsi utayakwepa haya maadamu upo hapa kwa utambulisho wa wazi, sio vyepesi kwa mtu wa nafasi yako kuwa kama wewe, wewe mwenyewe ni shahidi na sisi wote tu mashahidi.
Hii ni kwa sababu ya kuepuka kadhia za namna huo ndio maana wengi wa nafasi kama yako hawapo kama wewe.

Ombi langu kwako uendelee kuwepo hapa, uwepo wako hapa umekua mchango chanya mkubwa kuliko unvyo dhani, umekua mkubwa kiasi hakuna maelezo ya kutosha kusema .

Tuvumilie , tujibu kiustaarabu, nasi wengine tunakuunga mkono hatutaacha kukutetea kwenye hoja inayojenga , kukosoa panastahili, na kutoa maoni panapo hitajika.
Tunakushukuru sana .
 
Unaonaje turudi kuishi mapangoni na tukawashe vibatari vya kupekesha moto kwenye mchanga[emoji847] Ili turudie mambo yote ya kale....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Mh. Hiyo haikuwa hoja yangu hata kidogo, ni vyema ufahamu kuwa viduku, rasta, vimini nk. Hakijawahi kuwa kipimo cha uvunjifu maadili, haya engine upita na upepo wake na maisha yakaenda vizuri kabisa. Miaka yenu ya ujana vimini ilikuwa ni fashion, ikapotea na kurudi na itapotea tena.
 
Nipo pamoja nanyi hadi ukamilifu wa kazi hii niliyopewa.

Moyoni mwangu nilishatanguliza kusimika misingi ya hekima ya wenye hekima, Niko Nuruni tayari hakuna jipya tena la kuniweka mbali na maoni ya jamii Kwa sura zote maana nami ndiyo hapo ninapopenyeza ajenda halisi za wizara yao na penye kujifunza najifunza ila siwaachi jamii na mm ndiyo saiti zangu, tutazoeana tu [emoji28][emoji1666]

Ahsante Sana ubarikiwe kwa muda wako na maoni yako...

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana ya kubishana kwa hoja na matusi wala kejeli, kutukana na kutumia lugha mbaya inaonesha tu uwezo wako mdogo kichwani... mwenye uelewa wala hajapinic na anachangia mada vizuri tu, una la kujifunza hapo. Ukiangalia upande mzuri wa kitu angalia na upande mwingine wa shilingi
Wewe ni mpumbavu. Waziri kafafanua zaidi ya mara moja lakini bado unakaza fuvu kama mwendawazimu.
 
Mh. Hiyo haikuwa hoja yangu hata kidogo, ni vyema ufahamu kuwa viduku, rasta, vimini nk. Hakijawahi kuwa kipimo cha uvunjifu maadili, haya engine upita na upepo wake na maisha yakaenda vizuri kabisa. Miaka yenu ya ujana vimini ilikuwa ni fashion, ikapotea na kurudi na itapotea tena.
Ahsante Sana nashukuru kama hakika haikuwa hoja yako.

Sasa nadhani mm kwa maoni yangu Kila mara narudia kwamba: haya yote yaliyoanzishwa na jamii kwenye mjadala wao, kazi ya mifumo na wataalamu ni kuyajengea utaratibu wa mijadala waulizane waelewane wajue na mambo mengine kisha wahitimishe wao.

Na kwa kuwa hawatahitimisha kwa mtutu wa bunduki Bali fikra zao zitabadilika wao wenyewe kwa ridhaa yao, unaweza kukuta hata vijana wa huko wanaodhani sasa kufanya hivi au vile ni fasheni, wakaja hapa na ushuhuda kuwa, aisee tumeona haifai kabisa sijui ilikuwaje, hata kama linafaa kwingine.

Narudia tena kusema kuwa, hakuna sare sare Duniani na kilicho sare kule kinaweza tu kukataliwa kwingine bila shurti na jamii fulani ikawa na utaratibu wao usiovunja sheria wala katiba na ukapendwa tu na jamii ingine vilevile.

Mkinielewa point hii, mtavuta subira muone jamii hii iliyojadili haya mwisho itafika wapi. Je wakikubaliana hivyo kwa wema pasi na shurti atatokea mtu aende awaambie haya nyie nyoeni hivi vaeni vile?

Mm labda ndiyo sijawaelewa? , ila sisi tunachowapa ushirikiano huko ni kile nimekisema kwenye video....

Hii hapa sikiliza, wapi labda ndugu yangu mpendwa hujaelewa? Niko kwa ajili ya jamii nitakuja nijibu au nifafanue nk. Ahsante sana

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante Sana nashukuru kama hakika haikuwa hoja yako.

Sasa nadhani mm kwa maoni yangu Kila mara narudia kwamba: haya yote yaliyoanzishwa na jamii kwenye mjadala wao, kazi ya mifumo na wataalamu ni kuyajengea utaratibu wa mijadala waulizane waelewane wajue na mambo mengine kisha wahitimishe wao.

Na kwa kuwa hawatahitimisha kwa mtutu wa bunduki Bali fikra zao zitabadilika wao wenyewe kwa ridhaa yao, unaweza kukuta hata vijana wa huko wanaodhani sasa kufanya hivi au vile ni fasheni, wakaja hapa na ushuhuda kuwa, aisee tumeona haifai kabisa sijui ilikuwaje, hata kama linafaa kwingine.

Narudia tena kusema kuwa, hakuna sare sare Duniani na kilicho sare kule kinaweza tu kukataliwa kwingine bila shurti na jamii fulani ikawa na utaratibu wao usiovunja sheria wala katiba na ukapendwa tu na jamii ingine vilevile.

Mkinielewa point hii, mtavuta subira muone jamii hii iliyojadili haya mwisho itafika wapi. Je wakikubaliana hivyo kwa wema pasi na shurti atatokea mtu aende awaambie haya nyie nyoeni hivi vaeni vile?

Mm labda ndiyo sijawaelewa? , ila sisi tunachowapa ushirikiano huko ni kile nimekisema kwenye video....

Hii hapa sikiliza, wapi labda ndugu yangu mpendwa hujaelewa? Niko kwa ajili ya jamii nitakuja nijibu au nifafanue nk. Ahsante sanaView attachment 2781510

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Ubarikiwe sana Mh.
 
Hakuna cha msingi ulichomjibu mtoa mada, ameongelea uhalisia na namna ya kukabiliana na hizo changamoto. Kilichofanywa na hao viongozi wa kijiji husika hakipaswi kuungwa mkono kamwe, na ni uvunjifu mkubwa wa haki za raia. Wajaribu kutatua chanzo na wewe hukupaswa kuliunga hilo mkono.
Hicho kijiji si kisiwa ni kama ambavyo nchi yetu si kisiwa, nikitoka mjini ambako hakuna hiyo sheria na kwenda huko kuwa salimia wazee na nimevaa suruali ya jinzi iliyotobolewa magotini nitachukuliwa kama muhalifu na kutozwa faini. Nchi ya ajabu sana hii.
Kuweni serious na masuala ya msingi kwa maendeleo ya nchi hii na si bla bla kila siku

Mambo ya msingi kwa nchi hii ni pamoja na kulinda na kutunza maadili ya wananchi wa nchi hii.

Kila jamii inazo Mila, Desturi na Tamaduni zake na ni wajibu wa hizo jamii kuzilinda na wao wameamua kulinda Mila, Desturi na Tamaduni zao kwa style hiyo.

Kijiji kutokua kisiwa haina maana kiache kuzingatia taratibu zao za maisha kwa mujibu wa Mila na Tamaduni zao.

Tujifunze kuheshimiana na kuheshimu mipaka baina yetu.
 
Lina koneksheni gani na uhalifu au mmomonyoko wa maadili. Hadi Karne iliyopita tulikuwa tukicheza ngoma za asili huku wadada chuchu zikiwa nje.

Kwamba jamii zote za watanzania wa nchi hii walikua na Tamaduni za kucheza ngoma, tena wakiwa uchi?

Halafu ukosefu wa mavazi na uwezo wa jamii kuyapata hayo mavazi enzi hizo umezingatiwa kwa kiasi gani kwenye hoja yako hii?
 
Kwahiyo unashauri watoto wa kike watembee uchi,wanyoe viduku,na vijana wa kiume wavalie suruali mpaka kwenye magoti ?

Binafsi nimezipenda Sheria zilizo letwa na nampongeza waziri

lakini pia natamani zienee inchi nzima Kama ikiwezekana

Hivi inakuaje mtu una mguu size 5 afu unaenda kununua kiatu size 45 si bange hizo?

Af wanajisifu ndiyo mkoa wenye watu wa janja tz nzima😂😂😂
 
TATIZO MH UNALETA SIASA KWENYE MAISHA HALISI YA VIJANA WA KITANZANIA AMBAO TUNA UPEO WA KUELEWA MAMBO KIUELEDI.
VIONGOZI WETU HAWANA MAADILI NA NDIO VIOO VYA JAMII WANAOIGWA NA VIJANA .NA VIJANA WANAIGA YANAYOFANYWA NA VIONGOZI WETU AMBAO WANAOONGOZA KWA MMOMONYOKO WA MAADILI TENA WAZIWAZI BILA VIFICHO.
WA KULAUMIWA NI VIONGOZI WETU TULIOWAPA DHAMANA YA KUTUONGOZA WAMEKOSA MAADILI NA UKIWAKOSOA BASI WEWE NI JEURI NA HUNA NIDHAMU NA MHAINI UNASITAHILI KIFUNGO NA ADHABU KALI.
WATANZANIA WANAOGOPA KUSEMA NDIO MAANA WAPO KIMYA.

Kwamba kwa sababu kuna viongozi na vijana wa hovyo kila sehemu basi juhudi za kurekebisha zifutiliwe mbali na kusahaulika kabisa?

Ukitambua kwamba hao Viongozi unaowalaumu ni zao halisi la jamii zetu utaelewa ni kwanini hiyo jamii ya hicho kijiji imechukua hatua hizo katika jitihada za kulinda maadili na Tamaduni zao.

Watanzania hawawezi kuwalaumu hao viongozi kwa maana wao na hao ni zao kutoka shamba moja japo mbegu tofauti.

Hatua ya hiyo jamii kusimamia Mila, Tamaduni na Maadili yao ni Nzuri mno na yenye kufaa kuigwa na kila mwenye upeo unaojitegemea na mwenye kutambua umuhimu wa kesho yetu iliyosafi na utaifa wetu kwa Umoja wetu mbali ya tofauti zetu za kikabila na kiImani.

Tujifunze kushirikiana katika kheri tunapopata japo kiongozi mmoja mwenye nia thabiti ya kushirikiana na sisi kuyafikia malengo yetu na ya jamii zetu.

PS; Tafadhali acha kumfokea Doctor Gwajima na hizo CAPS zako, kuwa na Adabu.
 
Kila jamii ikiset rurels zake kulingana na invyotafsiri 'maadili' nini kinatengenzwa hapo?

Itatengenezwa heshima na ustaarabu miongoni na kati ya hizo jamii.

Hizo jamii zitatambua mipaka kati yake na kuilinda.

Jamii zitasimama imara kujilinda na kulinda mazingira yao na hatimaye utaifa utasimama tena ndani yetu na nchi kuimalika katika malengo na safari yake.

Jamii yoyote isiyotambua wala kuheshimu mizizi yake ni jamii mfu kwa maana inapotezwa na upepo tu uvumao kuelekea popote bila dira maalum.

Mizizi yetu ndio misingi yetu ndani ya family zetu, jamii zetu na taifa letu kwa ujumla.

Kumbuka; kila jamii hapa duniani ina identity (utambulisho) wake, haijalishi ni mdogo kiasi gani, lakini leo hii ukiulizwa utambulisho wa Mtanzania/ Mtanganyika ni upi, unaweza kuusema ama kuuonyesha?
 
Asante kwa mchango wako Mkuu, nina swali kidogo hapa... kuna jamii ambazo wanavaa vipisi vya nguo kama utamaduni wao na husikii mambo ya kumomonyoka kwa madili wala vitendo vya ukatili... suala la kumsababishia mtu ushawishi sababu fulani kavaa nguo fupi au iliyochanwa sio kwamba inatumika kama kisingizio cha kuhalalisha vitendo vibaya kufanyika? Unatenda kosa na kumtupia mtu lawama kwa kushindwa kutuliza tamaa zako?

Ukuaji wote huu wa technology bado tunashindwa kutafuta usahihi wa yale tuliyofundishwa na kukaririshwa hapo kabla?

Kwa mazingira ya kuishi nyikani (Tanganyika) kwa pamoja na wanyama wa porini, huyu binaadam anapata wapi duka la mavazi ili aache kuvaa vipisi vya nguo?

Huyo binaadam alikua karibu kiasi gani na kiwanda cha kutengeneza mavazi ya kujisitiri mwili wake?

Ni ipi tafsiri yako/ sahihi ya neno Tamaduni? Neno Mila? Neno Desturi?

Unayo taarifa yoyote ya maisha ya mtanganyika miaka kati ya 1500 na 1800?

Maasai anavaa shuka tupu, Mang’ati pia, lakini ni wapi umewaona waki modify mavazi yao na muonekano wao kuufanya uwe wa kisasa (sexualiteit) zaidi?

Haya mavazi ya bafuni wanayovaa wakina dada barabarani na sokoni sasa hivi ndio unafananisha na hivyo vipande vya magome ya miti na ngozi za wanyama?
 
Swali je, ni mitindo ya nywele na mavazi ndio mzizi wa mmomonyoko wa maadili?

Chimbuko la huo mtindo wa kunyoa wa kiduku ni wapi? Ni jamii ipi ina utaratibu huo?

Kwanini vijana wa Tanzania waige taratibu na mitindo kutoka jamii zingine? Hawana taratibu na mitindo yao ya nywele wakasimama nayo?

Kijana wa kiume wa Maasai hajawahi kunyolewa wala kulazimishwa kunyoa nywele zake ndefu. Hujiulizi ni kwanini?
 
Huo "mpango" jamii ilishirikishwa lini? Au mlijikalia wenyewe mkadanganyana mkaja na mpango ambao jamii hawaujui?

Hivi wanachi wangapi Tanzania hii wanaoijuwa google?

Ndiyo yaleyale nilisema, sana utakuja na ubunifu wa porojo na ngonjera (thesis), hakuna utekelezaji.

Unatakiwa uwepo kwenye jamii na uelewe "rootcauses" za matatizo ni nini. Siyo kuandaa maandiko yaliyojaa matatizo ambayo yanajulikana bila kuwa na ubunifu unaoonekana unashughulikiwa na wizara uanayiongoza. Ungekuwa na mipango mizuri usingeenda huko ulikoenda ili uonekane kwenye vyombo vya habari kuwa umeenda.

Ngoja nikusaidie, naona huna ubunifu, unaanza kutaka kunibadilishia kibao mimi na wananchi. Kama mimi na wanachi ndiyo unatuona tuna matatizo, basi ume fail wewe kutufanya tusiwe matatizo.

!) List down matatizo yote uyajuayo kayiaka wizara yako, halafu yatengenishe ya kidara (Administation) na kiuutendaji (Operations) Halafu ueleweuyayafikisha vipi kwa wateja wao (jamii) na uawauzia vipi ufumbuzi (Sales and Marketing.

Bila kujiundia mipango inayeaendana kwa principle hizo za Adminisration, Operation, Salase and Marketing Utabaki zima moto (reactive) maisha yako.

Kwa kuanza na hizo principals utaoata kuwa na plan, plan yako iwe ya muda mfupi, wa kati na mrefu.

Ukisha kuwa na plan hapoapo utakuwa unaingia kwenye kuwa (proactive).

Ukihitaji msaada wa ku plan, nipo hapa, uliza tu, tutakusaidia.

Kingine kabla sijakisahau. Sahau kabisa kuwa wewe hiyo ya uwaziri ni kazi. Usiwe na metality ya kama mwajiriwa uliyoizowea maishani mwako. Kuwa na metality ya kuwa huo ni mtihani wa Muum a wako, utawatumikia vipi waja wake.

Nafahamu, ni vigumu sana kwako ku "learn to unlearn", simply empty your cup and start afresh.

Kila siku asubuhi ukimaliza ablution zako na sala zako, uwe unafikiri, jana nimekibuni kipya cha kuwatumikia Watanzania. Ukiona vy0ote ni vilevile vya siku zote, elewa kuwa you are simply a reactive minded person.

Na huo waraka ulonambia ni-u-"google" nafanya hivyo sasa hivi.

Uwe na amani.

Kwamba wewe ndio mjuzi sana kuliko Waziri na team yake ya wasaidizi na wataalamu?

Kwamba haya uliyoweka hapo juu ni wewe pekee uyajuayo na kuyatumia katika kutimiza wajibu wako?

Ni rahisi sana kukand’ya juhudi za wengine na wakati huo huo tukitumia nafasi hiyo kudisplay Ego zetu na kujivua nguo hadharani.

Maandishi yako yanakutafsiri Kama mwanamke hasiyekua na stara katika kinywa chake na mwenye kutenda ili kufurahisha watu fulani. (If a parasite was a human….)
 
Back
Top Bottom