Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

Huyu anaogopa kuoindukiwa Urais na wenzake 2025, kwahiyo anaanza kutoa rushwa kwa watu wenye mizizi mirefu JWTZ, aache uoga

Hapana bana hajaanza kugawa haya huyu mama ni utaratibu wa miaka mingi tu.

Tofauti ni kwamba mwaka huu yamefanywa mbele ya camera,walianza na general mabeyo siku anastaafu akapewa ufunguo picha,akaja sirro nayeye akapewa prado na camera.

Si kwamba yameanza mwaka huu.
 
Vijana tuendelee kusubiri taifa la kesho!
Mara uzee huo..., bila hodi unaibukia taifa la tasaf!
Tuendelee kusoma namba
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu kesho Mama anatuma mawaziri Ulaya kwa wafadhili kuomba hela za bajeti ya taifa....haibu sana.
 
Ni jambo zuri, lakini waangaliwe namna ya kujengewa na nyumba maana wastaafu wengi wanaishi nyumba zisizoendana na nafasi walizokuwa nazo ukuzingatia walihusika na ulinzi wa taifa hili
 
Mzee Ruksa alivyopewa zawadi ya gari kwenye birthday yake tulichonga sana, wakati yeye alikuwa Commander in Chief ambaye kiprotokali ni bosi wa wakuu wa majeshi😀
 
wanufaika wa magari hayo kwa mujibu wa sheria ni jaji mkuu, spika wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, wakurugenzi wa tiss, na kadhalika
mujibu wa sheria ipi

Waziri kasema ni agizo la Mama Samia

au kutaja hadharani sheria ya migawanyo ya ulaji wa viongozi ni kuvunja wa sheria ?
 
nyie gawaneni tu keki ya taifa.sie wengine tumesharidhika kula amani ya taifa.maana ukihoji tu unaambiwa unahatarisha amani ya nchi unataka tuwe kama sudan.
 
Nice
 
Wao wanayo bado mazuri hayajachakaa
 
Napendekeza Hali ikiwanzuri kiuchumi wapewe helicopter na wake zao wapewe meli Kisha watoto zao treni Halafu wajukuu wapewe mabasi ya mwendo Kasi , vitukuu Range Rover!?? Poor country
 
Sisi wastaafu pia lakini hatujaongezwa pension kwa miaka zaidi ya 20! Nchi hii ni ngumu sana!
 
Sirro wamemuonea sana kumpa prado ambacho hata raia tu anaweza kununua.wanatakiwa wote wapewe gari sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…