Ugumu Wala sio kununua, ugumu ni kujaza pale inapoisha. Maana kununua ni mara moja tu, Ila kujaza ni kila inapoisha.
Gesi sio rahisi kulinganisha na mkaa. Mkaa gunia kwa mjini hapa ni 60000 Ila huu mkaa utakaa nao sana. Gesi ya kg 30 ambayo kujaza ni 55000 kwa mtu mwenye familia kubwa hutoboi wiki mbili. Acha kabisa kuhusu gesi, inakwenda balaa.
Gesi nzuri kwa mtu bachelor, hata mm nilipokua bachelor niliweza kutumia gesi siku zote na ilikuwa inakaa miezi hadi mitatu.
Wengi wenye familia ambao Wana kipato cha kawaida huwa wanatumia vyote kwa pamoja, gesi na mkaa. Usifikiri wanapenda