Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Hio mifumo yote msingi si ni katiba ambayo mnaikataa? Kungekuwa na serious punishment kwa wanaokiuka katiba usingekuwepo ujinga ujinga tunaoshuhudia leo.
 
Ana uthubutu mkubwa wa kufanya maamuzi..Ni trait na attribute muhimu Kwa kiongozi..

Yamkini anayo mapungufu lakini anaonyesha njia ktk kuwapa haki Wasio na uwezo wa kupambana na wenye bila Za ukwasi..

KATIBA MPYA YAWEZA KUJENGA TAASISI IMARA ZA UTOAJI HAKI..Mfumo imara wa upatikanaji wa Mahakimu,Majaji,Waendesha mashitaka na Wanasheria waadirifu.
 
Kwa hiyo kwako wewe migogoro ya ardhi isipelekwe mahakama za ardhi ipelekwe kwa Slaa atatue yeye kwa sheria zake binafsi?
We jamaa usichoelewa ni nini? Mfano Sheria inasema penye Zebra usimame wewe umepitiliza umegonga mtu ukakimbia, baada ya kushikwa unajifanya hukugonga mtu unamvuta traffic pembeni na kumuhonga pesa ili asawazishe, aliedhurika akienda mahakamani anakuta jaji kahongwa tayari anazungushwa tena ili kunyimwa haki. Ikitokea kiongozi mwenye dhamana ya juu bila kutegemea mahakama akilisimamia hili kwa sheria kabisa unafikiria aliedhulumu haki atapona?
 
Ni ngumu sana kupata haki kwenye nchi corrupt kama yetu hii, alijisemea mzee Rostam kuwa huwezi kutegemea mahakama ambayo kiongozi akipiga simu na kutoa amri tu hukumu inabadilishwa.
 
Ana

Anafanya vizuri ila anachangamoto pia ya namna ya kushughulikia hiyo migororo Kwa baadhi ya maeneo apunguze mihemko atulize jazba awe mtulivu wakati anapotatua hiyo migororo...
Apunguze Kweli munkari, lakini sometimes hata ingekuwa wewe lazima ukasirike,

Imagine mtu amepora nyumba ya mtu kimabavu Kisha anakwambia, waziri ningependa nikuone kidogo pembeni tuzungumze tuyamalize, mbele ya umma, ungefeel aje?
 
Apunguze Kweli munkari, lakini sometimes hata ingekuwa wewe lazima ukasirike,

Imagine mtu amepora nyumba ya mtu kimabavu Kisha anakwambia, waziri ningependa nikuone kidogo pembeni tuzungumze tuyamalize, mbele ya umma, ungefeel aje?
Huwezi jisikia vizuri ila kama kiongozi lazima kutumia hekima na Busara hasa kwenye umati mkubwa wakati mwingine unapimwa tuu namna unavyoweza kutongoza.
 
Huwezi jisikia vizuri ila kama kiongozi lazima kutumia hekima na Busara hasa kwenye umati mkubwa wakati mwingine unapimwa tuu namna unavyoweza kutongoza.
Leo tena alikuwa kariakoo,

Mtoto amemtimua manake na nduguze kwenye ghorofa la URITHI,

Waziri, Ametoa maelekezo ya BUSARA sana, hapakuwa na mihemko,

Nadhani anajirekebisha.
 
Huwezi jisikia vizuri ila kama kiongozi lazima kutumia hekima na Busara hasa kwenye umati mkubwa wakati mwingine unapimwa tuu namna unavyoweza kutongoza.
Hekima na busara zinatakiwa pande zote mbili, kama Mzee Mmasi alishindwa kuonesha heshima na busara kwa Waziri, ulitegemea Waziri ndiyo amnyenyekee Mmasi kisa tu yeye ni kiongozi!?? Mmasi ni muhalifu kumbuka hilo!!
 
Hivi kuna jimbo Dsm ambalo halina maendeleo kuzidi Ukonga? Sasa Jerry ndio mbunge wa Ukonga na hana lolote analofanya mbali na kutafuta kiki
 

Ivi tuteendelea kuwa wajinga na wapinga haki mpaka lin kwan wewe hujui mahakama zetu hazina haki kaka kumejaa rushwa na ukilitimba
 
Waziri yupo vizuri kichwani kabla hajakupiga nyundo anakupa ufafanuzi wa kisheria jamaa anabusara sana. Yaani mtu anapokonywa kiwanja alichodhulumu kimya kimya anaishia kutoa macho na kukuna upara, halafu wengi walio dhulumu watu viwanja ni wanene warefu na wana upara.
 
Hao unaoomba akae nao chini na kuongea ndio wanaosababisha migogoro ya ardhi, by all means watamkwamisha tu. Hao watu wa ardhi ulaji, rushwa na ufisadi ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Solution nzuri ni kuwaamuru tu, wala siyo kujadiliana nao.
 
Unataka kusema wizara ya ardhi ndio ina mamlaka ya kutatua kesi za ardhi?
 
Wenye mamlaka ya kutatua malumbano na migogoro ya ardhi kati ya wahusika wawili ni Mahakama peke yake, sio waziri wa ardhi!
 
Utapeli wanaofanyaa hao wanaotapeli watu Viwanja sio kwamba hakuna sheriaa.. Rushwaa imetawalaa sanaa sasa hakuna namna hata sheria iwe Ngumu vipi itaweza kufanya kaziii lazimaa Mtu aingie Field na kupambana na huu upuuzi direct... Hakuna rais alishawahi kufanya ziara nyingi za ndani ya nchi kama magu nadhani tuliona kazi aliyoifanyaa.. mtu mweusi bila kumfata nyuma nyuma kama mbuzii tegemea Madudu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…