Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Mifumo mizuri ni kuwaondoa watumishi wote kazini waliohudika kusababisha migogoro ya ardhi Kwa RUSHWA,

Kulitimiza hili, anahitaji support ya mawaziri wenzie utumishi na Rais,

Lakini Hadi hapo, ni sawa kufanya ziara, lakini pia ni muhimu kuweka viongozi waadilifu watakaozuia dhuluma na kumsaidia kirahisi zaidi.

Ubarikiwe.
Utafukuzaa wangapi sasa????🤣🤣🤣
 
Unataka kusema wizara ya ardhi ndio ina mamlaka ya kutatua kesi za ardhi?
Hata Commissioner wa Aridhi anayo mamlaka ya kutatua mgogoro wa Aridhi iliyopimwa,maana yeye ndiyo mtowaji wa umiliki wa Aridhi, kwa mfano akigundua kua ulileta taarifa za uwongo ili akumilikishe kipande cha Aridhi, akijirizisha pasipo na shaka ana mamlaka ya kisheria kubatilisha umiliki wako! Sasa wwe tapeli ndiyo utakimbilia Mahakamani kushitaki, na hauta shinda ngoo!!
 
Sina shida ya yeye kama anachapa kazi, ila hakuna haja ya kusaka "cheap popularity" mara afanye kazi mbele ya kamera, kazi zake njema zitajitangaza haina haja kutangaza tangaza
Watu wakiona video za mambo kama hayo anayofanya Waziri wanapata tumaini kwamba na wao kero zao zinaweza kutatuliwa zikifika kwa waziri husika.
Ukiwa unafanya mambo kwa kujificha ni rahisi wabaya wako kupindisha ukweli kuhusu mambo unayofanya.
 
Ivi tuteendelea kuwa wajinga na wapinga haki mpaka lin kwan wewe hujui mahakama zetu hazina haki kaka kumejaa rushwa na ukilitimba
Mtu anadai haki yake mahakamani zaidi ya miaka 10 anazungushwa tu,anakuja waziri anamsaidia kupata haki yake WAPUMBAVU kama chiembe wanaanza kumtukana eti anatafuta kiki.
Unajiuliza hawa watu wana akili kweli?
 
Taaluma ya kupigwa pipe
Marinda huna, unatembea mzigo unamwagika
Mtu anadai haki yake mahakamani zaidi ya miaka 10 anazungushwa tu,anakuja waziri anamsaidia kupata haki yake WAPUMBAVU kama chiembe wanaanza kumtukana eti anatafuta kiki.
Unajiuliza hawa watu wana akili kweli?
Waziri anampamba tu, akienda mahakamani wanafuta, waziri hana maamuzi ya mwisho kuhusu haki, endelea kukenua masaburi tu
 
Unataka kusema wizara ya ardhi ndio ina mamlaka ya kutatua kesi za ardhi?
Hapana, hawana; lakini chukulia haya aliyoshughulika nayo Silaa moja kwa moja, bila ya kutazama hizo taratibu za kimahakama.
Kuna njia nyingi za kumaliza baadhi ya migogoro bila kuhusisha mahakama, na sidhani kuwa anayofanya Silaa ni mbadala wa mahakama.
Hao walionyang'anywa, bado wanaweza kwenda mahakamani kudai mali, kama ni yao. Kama hawaendi, itakuwa na maana wao ndio walikuwa na makosa. Walikuwa wamepora mali kwa uonevu.

Silaa asilaumiwe kwa kushughulikia migogoro ya uonevu kama hii.
Wengi mnaokimbilia mahakama mnajuwa huko hakuna haki kama huna chochote mfukoni.
 
Marinda huna, unatembea mzigo unamwagika

Waziri anampamba tu, akienda mahakamani wanafuta, waziri hana maamuzi ya mwisho kuhusu haki, endelea kukenua masaburi tu
Vichwa vya panzi kama hiki hapa ndivyo vinavyokubalika sana katika awamu hii ya maigizo. Mtu mwenye akili timamu hawezi kuandika upuuzi kama huu hapa jukwaani.
 
Salaam, Shalom!!

Nimefuatilia Kwa ukaribu jinsi waziri Jerry Slaa anavyofanya katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, japo Bado ni mapema sana kusema kuwa anafanya vizuri, lakini Kwa sasa itoshe kusema ana kitu kinachoonekana, na atafika mbali, tuendelee kumwombea.

Nimesikiliza Kwa Umakini jinsi alovyotatua case ya Tajiri aitwaye Mzee Mmassy aliyenunua nyumba Kwa marehemu aliyeko kaburini, yaani document zinaonyesha marehemu akiwa kaburini alisaini mauziano na kumuuzia nyumba tajiri Mmassy,na jinsi alivyotatua case Ile Kwa uwazi Kwa kutumia nyaraka halali katika ofisi ya ardhi, na jinsi alivyoweza kuwarudishia nyumba watoto na mke wa marehemu nyumba Yao, kiukweli Mungu aendelee kumjalia uhai na AFYA na baraka kiongozi huyu.

Nilifanikiwa pia kufuatilia jinsi alivyosaidia kutatua mgogoro ulioletwa na Msama, Kwa kutomtendea HAKI yake mama yule aliyedai kiwanja chake, pia nimeona ufuatiliaji, uthubutu na uchapakazi wa Waziri huyu kijana Jerry Slaa.

Ni maombi yangu, akae chini na viongozi wenzie katika wizara yake na kuja na mpango MIKAKATI wa kutatua migogoro ya ardhi Nchi nzima bila kuwepo haja ya kusafiri huku na huko, uwepo mfumo mzuri na WA haraka zaidi kuwafikia wananchi na kutatua migogoro hiyo ya ardhi.

So far, KAZI imeonekana inafanyika,

Mungu Mbariki Waziri huyu Jerry Slaa,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241]

Ameeen.

Source: Milard Ayo tv.

Karibuni[emoji120]
tabu ni kuwa aina hii ya mawaziri huwa hawakawii kutumbuliwa kwa majungu na fitina.

ukifanya kazi kama waziri Jery Slaa lazima utapigwa majungu na fitina, hivyo unatakiwa uwe umejitoa kwa lolote lile. usiwe muoga
 
tabu ni kuwa aina hii ya mawaziri huwa hawakawii kutumbuliwa kwa majungu na fitina.

ukifanya kazi kama waziri Jery Slaa lazima utapigwa majungu na fitina, hivyo unatakiwa uwe umejitoa kwa lolote lile. usiwe muoga
Kukaa miaka mitano Kwa HOFU na unafiki, na kukaa miezi SITA unafanya kitu kinachoonekana kipi Bora?

Nijuavyo, ukipewa Uwaziri, soma mamlaka na mipaka ya nafasi Yako Kisha fanya KAZI.

Nakumbuka Magu alikuwa anafukuza KAZI wezi anapoingia tu wizarani, Anamwambia Rais KIKWETE, wafuatao siwataki wizarani, watafutie pa kwenda.

Huo ndio uwajibikaji.
 
tabu ni kuwa aina hii ya mawaziri huwa hawakawii kutumbuliwa kwa majungu na fitina.

ukifanya kazi kama waziri Jery Slaa lazima utapigwa majungu na fitina, hivyo unatakiwa uwe umejitoa kwa lolote lile. usiwe muoga
Kujipambanua kwa namna hiyo ndiko kunakoitwa kuwa KIONGOZI.
Kiongozi anasimamia anayoyaamini na kuyatekeleza bila ya kujali yatakayomtokea yeye. Jambo la muhimu ni kujitolea kuwatumikia wananchi bila ya kumwonea au kumpendelea mtu.

Viongozi wa namna hii tunao wachache sana, na ni mara moja moja anajitokeza mmoja mwnye dhamira ya kweli na anayoyafanya. Inakuwa ngumu sana hawa watu kujitokeza mbele hasa wakati serikali wanayoitumikia yenyewe imeghubikwa na ufisadi.

Kuna wanaoigiza kwa muda mfupi. Wanapopata sifa uigizaji unatoka na wanaangukia tena kwenye tabia zao za kawaida. Mifano ninayo hapa; lakini sitaitoa kwa sasa.
 
Nijuavyo, ukipewa Uwaziri, soma mamlaka na mipaka ya nafasi Yako Kisha fanya KAZI.
Hakika; lakini pia tumia akili vizuri kujuwa upo kwenye mazingira yasiyokuwa rafiki.

Kumbuka Magufuli alivyokomaria kubomoa jengo la Tanesco pale Ubungo, na jinsi alivyofanya na watu wa Kimara na nyumba zao. Ni vizuri kwa kiongozi kuwa 'firm' ukijuwa unafanya kazi yako ndani ya mipaka, kisheria, na kibinaadam pia.

Najuwa hapa panaweza kuwa na utata; kwamba hiyo barabara hapo Kimara pengine hadi leo isingekuwa imejengwa!
'Catch 22.
 
Back
Top Bottom