Huyo hamna kitu, ana-deal na kiki ambazo akikutana na mbabe anakwama, yaani uje mtaani umtoe mtu kwenye nyumba, hiyo ni kazi yako kama waziri? Anatafuta yale yaliyomkuta Mwamwindi wa Iringa.
Wizara ina mambo makubwa ya kisera ya kufanya, hayafanyii kazi.
Kuna tatizo kubwa la utawala wq ardhi (land administration) hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya nchi yetu haijapimwa. Sheria ya ardhi namba 4/1999 inajishughulisha na ardhi yenye hati, lakini wangapi mjini wqna hati? Wale wasio na hati wanakuwa regulated vipi? Wizara imetoa muongozo kwa uhamishaji wa miliki ambazo hazina hati?
Wizara ina mpango gani kuunga mifumo ya kibenki na usajili wa ndoa ili mali za dhamana wakopeshaji wajue hali ya mkopaji?
Kulikuwa na mradi wa hati za kidigitali, umekwama wapi?
Benki ya dunia walitoa bilioni 350 kufadhili mradi wa wizara ya ardhi ambao unajumuisha ujenzi wa majengo ya taasisi za ardhi kila mkoa, mbona bajeti inaisha, majengo hayapo? Na hata vifaa walivyosema watanunua kwa ajili ya kila mkoa ili kupima ardhi havipo? Hizo hela zimeenda wapi?
Mamlaka zinapoingiza vijiji mjini, wizara imetoa muongozo kuhusu ardhi iliyokuwa ya vijiji? Kuna namna au mfumo wa vijiji kukabidhi ardhi kwa Halmashauri? Au ndio inaachwa kwa viongozi wa mitaa mipya wajiuzie wanavyotaka?
Hatumuoni katika migogoro ya hifadhi za taifa na wananchi, anazurura mijini tu. Kapima vijiji vingapi mwaka huu? Amegawa hati za kimila ngapi?
He is just a petty politician ambaye alitakiwa ajenge josho ili kuosha wanyama kwq maelfu, yeye kaamua kuchambua manyoya ya mnyama mmoja mmoja ili awe anatoa kupe