Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Slahaa, Msajili wa.Hati pamoja na Commissioner wa Aridhi ndiyo wenye mamlaka na Aridhi na siyo Mahakama, Mahakama yake ni migogoro! Commissioner na Msajili wa Hati ndiyo wenye final say kwenye swala zima la Aridhi kuhusu umiliki wa Aridhi iliopimwa!!
Wanajitoa ufahamu kupotoasha,

Wanaodhani wananchi ni mbumbumbu hatuelewi kitu.
 
Migogoro mingi ya ardhi chanzo ni wizara yake,

Na nafasi ya Waziri na maamuzi yake kupitia vikao na taarifa Ofisini kwake Ina umuhimu mkubwa.

Wengi hukosa HAKI wizara ya ardhi ndipo huenda mahakamani.

Kwa case ya Mmassy, tayari imetatuliwa Kwa 50%, mama yule atatumia utatuzi wa Waziri kama mojawapo ya ushahidi na kupata ushindi.

Si lazima kupinga Kila kitu.
Swali ni kwamba huyo mmasy hiyo hati kaitoa wapi?
Je hiyo hati ni halali?
Ana uhakika gani kwamba huyo mama hadanganyi?je kabla ya kwenda site alisikiliza pande zote mbili? Au ameenda na maelezo ya upande mmoja halafu ya upande wa pili anaysikilizia pale pale?
Amefanya intensive background search ili kujua historia halisi ya huo mgogoro?
Na hao maofisa wa wizara waliompa mmasi hio hati,wamechukuliwa hatua gani?
Kwa sababu anachokifanya silaa ni kuwalinda maafisa ardhi,na kuwaadhibu wananchi kwa kivuli cha kutetea wanyonge.
Halafu anatumia kigezao gani cha kuchagua kesi anazoenda kuzitatua site?
Na je kati yake yeye na mahakama, tumuamini nani? Mbona asilimia kubwa ya kesi anazotatua site wanaoitwa wanyonge ni jinsia. Ya aina moja tu?
 
Anachokifanya Slaa ni kizuri mno.

Kwa kuwa anakuwa amezungukwa na wataalamu wake,

Ile inakuwa case ya wazi na ya kirafiki zaidi,

Mashahidi wote wanakuwepo Hadi balozi anakuwepo.

In short, Slaa ana Nia njema,

Aungwe mkono.
 
Hapana,anachokifanya ni siasa.yaani katika hali ya kawaida atawarudishia hao walalamikaji maeneo yao,then aliyenyanganywa ataenda mahakamani atashinda kesi,then atamtoa tena mlamikaji.silaa hatokuwepo miaka yote.
Hii imetokea kariakoo.
Maneno ya waziri sio sheria.
Alichotakiwa kufanya ni kitengeneza platform nzuri ya utatuzi wa migogoro ya ardhi,na sio kuruka ruka kama kuku.
Huu ni ujinga,ni siasa za kizamani za kimagufuli.
Basi tufunge mhakama,na tuwaambie mawaziri wote wawe majaji
 
Unacholalamikia wewe hapa hata hakieleweki, bila shaka nawe ni hao hao majambazi. Silaa hajazuia mahakama kufanya kazi. Matatizo aliyoshughulikia hadi sasa yapo wazi kabisa kuwa yalikuwa ni ya uonevu na unyang'anyi.
Sasa kama unategemea hayo mahakama ukatoe rushwa huko wewe jambazi, hilo ni tatizo jingine.
Taratibu, hata huko mahakamani pataanza kuibuka akina Silaa wengine wasiopenda uchafu wenu.
 
Ana
Salaam, Shalom!!

Nimefuatilia Kwa ukaribu jinsi waziri Jerry Slaa anavyofanya katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, japo Bado ni mapema sana kusema kuwa anafanya vizuri, lakini Kwa sasa itoshe kusema ana kitu kinachoonekana, na atafika mbali, tuendelee kumwombea.

Nimesikiliza Kwa Umakini jinsi alovyotatua case ya Tajiri aitwaye Mzee Mmassy aliyenunua nyumba Kwa marehemu aliyeko kaburini, yaani document zinaonyesha marehemu akiwa kaburini alisaini mauziano na kumuuzia nyumba tajiri Mmassy,na jinsi alivyotatua case Ile Kwa uwazi Kwa kutumia nyaraka halali katika ofisi ya ardhi, na jinsi alivyoweza kuwarudishia nyumba watoto na mke wa marehemu nyumba Yao, kiukweli Mungu aendelee kumjalia uhai na AFYA na baraka kiongozi huyu.

Nilifanikiwa pia kufuatilia jinsi alivyosaidia kutatua mgogoro ulioletwa na Msama, Kwa kutomtendea HAKI yake mama yule aliyedai kiwanja chake, pia nimeona ufuatiliaji, uthubutu na uchapakazi wa Waziri huyu kijana Jerry Slaa.

Ni maombi yangu, akae chini na viongozi wenzie katika wizara yake na kuja na mpango MIKAKATI wa kutatua migogoro ya ardhi Nchi nzima bila kuwepo haja ya kusafiri huku na huko, uwepo mfumo mzuri na WA haraka zaidi kuwafikia wananchi na kutatua migogoro hiyo ya ardhi.

So far, KAZI imeonekana inafanyika,

Mungu Mbariki Waziri huyu Jerry Slaa,

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Ameeen.

Source: Milard Ayo tv.

Karibuni🙏
Anafanya vizuri ila anachangamoto pia ya namna ya kushughulikia hiyo migororo Kwa baadhi ya maeneo apunguze mihemko atulize jazba awe mtulivu wakati anapotatua hiyo migororo...
 
Unacholalamikia wewe hapa hata hakieleweki, bila shaka nawe ni hao hao majambazi. Silaa hajazuia mahakama kufanya kazi. Matatizo aliyoshughulikia hadi sasa yapo wazi kabisa kuwa yalikuwa ni ya uonevu na unyang'anyi.
Sasa kama unategemea hayo mahakama ukatoe rushwa huko wewe jambazi, hilo ni tatizo jingine.
Taratibu, hata huko mahakamani pataanza kuibuka akina Silaa wengine wasiopenda uchafu wenu.
[/QUOT
Wewe ndio hueleweki, kama tatizo ni uonevu, mbona hao waliotoa hizo hati hawadhibiwi?
Halafu mbona hao waliokamatwa hawafikishwi mahakamani? Au anataka awafunge moja kwa moja?
 
Salaam, Shalom!!

Nimefuatilia Kwa ukaribu jinsi waziri Jerry Slaa anavyofanya katika utatuzi wa migogoro ya ardhi, japo Bado ni mapema sana kusema kuwa anafanya vizuri, lakini Kwa sasa itoshe kusema ana kitu kinachoonekana, na atafika mbali, tuendelee kumwombea.
Labda 2025 akagombee jimbo lingine, sio tena Ukonga
 
Swali ni kwamba huyo mmasy hiyo hati kaitoa wapi?
Je hiyo hati ni halali?
Ana uhakika gani kwamba huyo mama hadanganyi?je kabla ya kwenda site alisikiliza pande zote mbili? Au ameenda na maelezo ya upande mmoja halafu ya upande wa pili anaysikilizia pale pale?
Amefanya intensive background search ili kujua historia halisi ya huo mgogoro?
Na hao maofisa wa wizara waliompa mmasi hio hati,wamechukuliwa hatua gani?
Kwa sababu anachokifanya silaa ni kuwalinda maafisa ardhi,na kuwaadhibu wananchi kwa kivuli cha kutetea wanyonge.
Halafu anatumia kigezao gani cha kuchagua kesi anazoenda kuzitatua site?
Na je kati yake yeye na mahakama, tumuamini nani? Mbona asilimia kubwa ya kesi anazotatua site wanaoitwa wanyonge ni jinsia. Ya aina moja tu?
Ndg tafuta hukumu ya Mahakama kuu iliorudisha nyumba kwa familia ya Mfumia, imeelezea vizuri sana Mmasi alivyopata hiyo hati ya Marehemu Mfumia na huta uliza tena haya maswali yako!!
 
Kwa hiyo kwako wewe migogoro ya ardhi isipelekwe mahakama za ardhi ipelekwe kwa Slaa atatue yeye kwa sheria zake binafsi?
Ukiona umebomelewa au umenyanganywa nyumba na Waziri wa Aridhi ujuwe wwe ndiyo hukufuata sheria za Aridhi, sasa unataka kukimbilia mahakamani ili upate huruma ya Mahakama kupitia sheria tata za Mahakama!!
 
Hapana,anachokifanya ni siasa.yaani katika hali ya kawaida atawarudishia hao walalamikaji maeneo yao,then aliyenyanganywa ataenda mahakamani atashinda kesi,then atamtoa tena mlamikaji.silaa hatokuwepo miaka yote.
Hii imetokea kariakoo.
Maneno ya waziri sio sheria.
Alichotakiwa kufanya ni kitengeneza platform nzuri ya utatuzi wa migogoro ya ardhi,na sio kuruka ruka kama kuku.
Huu ni ujinga,ni siasa za kizamani za kimagufuli.
Basi tufunge mhakama,na tuwaambie mawaziri wote wawe majaji
Wizara ya ardhi ikinyooka na kufanya kazi zake kwa weledi, basi Mahakama zitakosa kazi,maana kutakua hakuna tena migogoro ya Aridhi Nchini!!
 
Huyo hamna kitu, ana-deal na kiki ambazo akikutana na mbabe anakwama, yaani uje mtaani umtoe mtu kwenye nyumba, hiyo ni kazi yako kama waziri? Anatafuta yale yaliyomkuta Mwamwindi wa Iringa.

Wizara ina mambo makubwa ya kisera ya kufanya, hayafanyii kazi.

Kuna tatizo kubwa la utawala wq ardhi (land administration) hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya nchi yetu haijapimwa. Sheria ya ardhi namba 4/1999 inajishughulisha na ardhi yenye hati, lakini wangapi mjini wqna hati? Wale wasio na hati wanakuwa regulated vipi? Wizara imetoa muongozo kwa uhamishaji wa miliki ambazo hazina hati?

Wizara ina mpango gani kuunga mifumo ya kibenki na usajili wa ndoa ili mali za dhamana wakopeshaji wajue hali ya mkopaji?

Kulikuwa na mradi wa hati za kidigitali, umekwama wapi?

Benki ya dunia walitoa bilioni 350 kufadhili mradi wa wizara ya ardhi ambao unajumuisha ujenzi wa majengo ya taasisi za ardhi kila mkoa, mbona bajeti inaisha, majengo hayapo? Na hata vifaa walivyosema watanunua kwa ajili ya kila mkoa ili kupima ardhi havipo? Hizo hela zimeenda wapi?

Mamlaka zinapoingiza vijiji mjini, wizara imetoa muongozo kuhusu ardhi iliyokuwa ya vijiji? Kuna namna au mfumo wa vijiji kukabidhi ardhi kwa Halmashauri? Au ndio inaachwa kwa viongozi wa mitaa mipya wajiuzie wanavyotaka?

Hatumuoni katika migogoro ya hifadhi za taifa na wananchi, anazurura mijini tu. Kapima vijiji vingapi mwaka huu? Amegawa hati za kimila ngapi?

He is just a petty politician ambaye alitakiwa ajenge josho ili kuosha wanyama kwq maelfu, yeye kaamua kuchambua manyoya ya mnyama mmoja mmoja ili awe anatoa kupe
mke wa Msama
 
Kwa hiyo kwako wewe migogoro ya ardhi isipelekwe mahakama za ardhi ipelekwe kwa Slaa atatue yeye kwa sheria zake binafsi?
Una kichwa kizito sana kuelewa kitu kidogo sana kama hicho! Nakupa mfano mdogo sana, kama umeenda kupima DNA kwa Mkemia,na majibu ya katoka kua mtoto siyo wako, je utaenda mahakamani ili kupinga matokeo ya DNA!? Je Mahakama ikisema mtoto ni wako kwa sababu tu wwe ndiyo ulilea mimba utakubali!?
 
Huyo hamna kitu, ana-deal na kiki ambazo akikutana na mbabe anakwama, yaani uje mtaani umtoe mtu kwenye nyumba, hiyo ni kazi yako kama waziri? Anatafuta yale yaliyomkuta Mwamwindi wa Iringa.

Wizara ina mambo makubwa ya kisera ya kufanya, hayafanyii kazi.

Kuna tatizo kubwa la utawala wq ardhi (land administration) hasa kwa kuwa asilimia kubwa ya nchi yetu haijapimwa. Sheria ya ardhi namba 4/1999 inajishughulisha na ardhi yenye hati, lakini wangapi mjini wqna hati? Wale wasio na hati wanakuwa regulated vipi? Wizara imetoa muongozo kwa uhamishaji wa miliki ambazo hazina hati?

Wizara ina mpango gani kuunga mifumo ya kibenki na usajili wa ndoa ili mali za dhamana wakopeshaji wajue hali ya mkopaji?

Kulikuwa na mradi wa hati za kidigitali, umekwama wapi?

Benki ya dunia walitoa bilioni 350 kufadhili mradi wa wizara ya ardhi ambao unajumuisha ujenzi wa majengo ya taasisi za ardhi kila mkoa, mbona bajeti inaisha, majengo hayapo? Na hata vifaa walivyosema watanunua kwa ajili ya kila mkoa ili kupima ardhi havipo? Hizo hela zimeenda wapi?

Mamlaka zinapoingiza vijiji mjini, wizara imetoa muongozo kuhusu ardhi iliyokuwa ya vijiji? Kuna namna au mfumo wa vijiji kukabidhi ardhi kwa Halmashauri? Au ndio inaachwa kwa viongozi wa mitaa mipya wajiuzie wanavyotaka?

Hatumuoni katika migogoro ya hifadhi za taifa na wananchi, anazurura mijini tu. Kapima vijiji vingapi mwaka huu? Amegawa hati za kimila ngapi?

He is just a petty politician ambaye alitakiwa ajenge josho ili kuosha wanyama kwq maelfu, yeye kaamua kuchambua manyoya ya mnyama mmoja mmoja ili awe anatoa kupe
Huna akili tapeli wewe
 
Mahakamani zinafanywa analysis nyingi kabla ya hukumu, huyo Silaa anayekaa vichochoroni usiku ana muda wa kutoshaha kufanya hivyo, kama jamaa aliingia kwa nguvu ya mahakama, huyo mama hatamaliza mwezi ndani ya nyumba hiyo, mahakama itamtoa, na Jerry akikoroma ataitwa mahakamani ajieleze kwa nini asifungwe kwa kudharau mahakama.

Mambo ya alikufa lini, kama hakuyasema mahakamani, ni kazi bure kwa sasa

Nvhimbi na Makala wamesema mambo ya Mahakamani yasiingiliwe, yeye anajitoa akili
Tapeli
 
Watanzania ambao ni miongoni mwa waafrika wengi wajinga waliozaliwa katika bara la wajinga hawajui wanataka nini.

Nchi hii inasheria, taratibu za ununuzi na umiliki wa ardhi ila taratibu hizo hazifuatwi na watumishi wa wizara husika na baadhi ya wanachi pia hawafuati hizo taratibu tena makusudi.

Sasa mnataka waziri akae ofisini atengeneze mifumo ipi tofauti na hii iliyopo? Tatizo sio mifumo ni watumishi wasio na weredi sasa hawa unadeal nao vipi bila kuwafikia hukohuko waliko na kuwanonesha kwa vitendo wajibu wao ni upi, maana wakifukuzwa kazi bado mtakuja hapa kulalamika wameonewa.
Anakuja mtu mmoja na kumuita Slaa ni mpumbavu wakati mtu anadai haki yake miaka 20 anapigishwa mark time tu huko mahakamani😁!

Ukifuatilia sababu unakuta hakimu yuko kwenye payroll ya kibopa ambaye amedhulumu ardhi.
 
Back
Top Bottom