Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Pamoja na kwamba rushwa ni changamoto kubwa katika siasa zetu, Jerry anastahili pongezi nyingi kwa kupambana kwa maneno na vitendo. Amesema hadharani kwamba alipelekewa rushwa akakataa na amewaachisha watumishi kazi.
 
Ndio maana kuna rushwa kubwa na rushwa ndogo. Tutajuaje kama hao watoto wa matajiri hawakula rushwa kuiuza ngorongoro na bandari yetu?
 
Ego inamwendesha na anasahu yupo hapo kwa muda kwanza hakuna mwanasiasa wa kukataa mil 300 huko ccm anatafuta kuongelewa na Attention
Wanasiasa waliotosheka na wapatacho kama mshahara ni wengi sana. Changamoto ni kwamba siasa zilifanywa biashara na hivyo bila pesa hupati uongozi, hivyo rushwa hutumika kama njia ya kurudisha.
Hata hivyo, Jerry ameonesha njia, mawaziri na viongozi wengine waige.
Hakuna aliye msafi 100%, lakini kujitokeza kwa mtu kama huyu, lazima apongezwe.
 
Anatafuta kiki ya kisiasa 2025. 2020 alihonga 25ml kushinda Ukonga.
 
Kudos waziri ingawa tungepata mwendelezo wa takukuru huyo tajiri achukuliwe hatua kwa kosa la kutaka kutoa rushwa,haya mambo yasikieni tu ndugu zangu je ni wangapi wenye kukubali rushwa haki za watu zipindishwe,yaliyonikuta ndugu zangu nimeiona nchi yangu kwa mtazamo tofauti sana na nilivyokuwa naiona mwanzo,hakika rushwa ni adui mkubwa wa haki na haki huinua taifa bali dhulma inaibomoa
 
Hivi wanaorusha chopper nao wanaitwa Marubani?
 
Kama ni kweli Abarikiwe !πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mkuu, hizi Million 300 ni za mmiliki wa kile kituo cha mafuta kicholalamikiwa na wakina Prof. Tibaijuka?
 
Mkuu, hizi Million 300 ni za mmiliki wa kile kituo cha mafuta kicholalamikiwa na wakina Prof. Tibaijuka?
Majirani hapo wanajielewa
Siyo wale wa tandale wameletewa vituo vya mafuta mpaka vibarazani
Ile njia tu kuna sehemu ya wazi kuna mtu alitaka fungua pub jamaa Alizuiwa sana sana serikali ya mtaa walikula pesa yake
Kipande kile kuna wazee wanajielewa

Ova
 
Maneno tu haya. Hata kwenye kanga moko yapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…