Namfahamu Jery Slaa vyema. Naona ametamka kwamba apokei rushwa. Fine kwa sasa akiwa waziri anaweza akaamua kuridhika na anachopata akakaa mbali na watoa rushwa
Ila naomba kumkumbusha Jery kwamba ubunge wake aliupata kwa rushwa. Hivyo kama apokei rushwa anapaswa kwanza kuukataa ubunge wake. Rushwa ni rushwa tu....ni kitendo cha kupokea kisicho haki yako ambapo for sure ubunge siyo halali yako.
Lakini eneo la pili kwenye rushwa ya Ardhi namkumbuka mama Mabula, alijipambanua kwamba hapokei rushwa ila skendo za rushwa zilikuwa kumwondoa ofisini leo hana uwezo hata wakuwa tena mbunge.
Jeryy mapigano ya rushwa ni matendo siyo maneno.....wewe baba yako alikuwa rubani na tunakubali wewe ni familia bora ila hakuna familia imewahi kuridhika na kile walichonacho.....mwanao kufika hapo alipo katika Chipukizi kuna rushwa imetembea and you know.
Wapo watoto wazazi wao walikuwa marais na wengine watoto wa mawaziri lakini ndio vinara wa rushwa nchini.
Tuambie lini umeachana na rushwa ukiwa mwanasiasa? Labda useme umeacha kuchukua fedha za ardhi na viwanja