Waziri Kabudi akanusha kuthibitisha kifo cha Mwanahabari, Azory Gwanda

Tuwape pole wana wa dodoma
Waziri amechemka on camera. Maelezo yake yaliacha mwanya kwa watu kuwa na tafsiri sahihi kuwa Aazory Gwanda amefariki.

Kakosea kwanza kwa kusema hivyo, halafu anaendelea kukosea kwa kushindwa kuomba radhi na kukubali kosa, analaumu tafsiri.
 
Unataka kutwambia kuwa watanzania woote 55m hawajui kiingereza?
Ujumbe tulioupata hapa ni kurudi darasani kujifunza lugha upya. Maana ni wengi tumemuelewa tofauti na alichokusudia kutueleza.
 
Huyo ndiye poropesa wetu nguri
Alipaswa kusema ‘waliopotea au kuuwawa’.

Siyo ‘waliopotea na kuuwawa’ maana hiyo inaacha mwanya wa tafsiri zingine.

Yeye kama mwanasheria nguli nilitegemea awe makini sana na uchaguzi wa maneno atumiayo.
 
Yeye ndiye anapaswa kurudi darasani kujifunza tofauti ya "disappeared and died" na "disappeared or died".

Kama hawa ndio watu wanaosimamia mikataba yetu, si ajabu tunapigwa changa la macho kila siku.

Ni kweli kabisa Mkuu,Neno moja hubadili maana ya Taarifa nzima katika tafsiri.Sisi tuna shika ile kauli ya Mwanzo.
 
"Disappear and died" hapa alimaanisha kuwa kila mpoteaji hufa, therefor Gwanda kashakufa. Wewe ni nani kumsemea?
 
Utatetea hata visivyo stahili yaani anakana hata matamshi yake maana clip ipo
 
"Disappear and die" tafsiri yake ni nini?
 
Aliyesema ni profesa na aliyefafanua ni daktari wa falsafa!
Hivi ukitoka kuwa Dk-PhD si ndio unakuwa profesa!? Tusaidiane maana wengine hatujui.
 
Mara ya kwanza niliamini sijamsikia akisema hivyo. Ikabidi nirudie kusikiliza mara 2 na bila shaka yeyote Prof. umpende usimpende aliyasema maneno hayo. Kitu cha kiungwana akubali tu kama amekosea na aombe radhi (ingawa sio kawaida yetu watanzania). Na kwa mwanasheria nilitegemea angekuwa makini zaidi. Hapa issue ya Mbowe na Sugu haingii kabisa Prof. ameharibu na Dr Abbasi angekaa mbali amuachie aliesema azungumze.
 
Ameonyesha umbilimbi wake
Alipohojiwa wakati ule wa Lissu ndipo nilipoamini kuwa uprofressor alinunua
Amelikoroga aandae vikombe kunywa uji mbichi
Karma is a bitch karibu mtasema ukweli
Sidhani kama alinunua uprofessor. Shida inakuja pale wanapoingia kwenye siasa wengi hawana experience na ndio yanapowakuta hasa wanapojaribu kutetea visiyo kuwa na utetezi. Asinge unganisha ya Azory na yaliyowakuta wengine labda asinge likoroga. Wote wakina Bashiru, Mwakyembe, Kitila haya yanawahusu. Na majaji wasiokuwa waangalifu pia wameingia mkenge wa kutumika na wanasiasa (Kaijage na Mutungi ni mifano mizuri). Ni vizuri hili limemkuta kama ni mahiri kama tunavyo ambiwa atajitafakari sana, kwa wastarabu leo angeachia ngazi.
 
Mkubwa huwa hakosei hasa kwa hadhi yake ya uwaziri na uprofesa wake. Tujifunze tu kumuelewa hata kama anachotueleza hatukielewi tumuelewe tu hivyo hivyo.
 
Sasa Kabudi kawa mwanasiasa kwelikweli. Hata anatakiwa kuchunga kauli zake.
 
....who disappeared and died/....who disappeared and who died/....who disappeared OR died....Kidhungu kigumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…