Waziri Katambi: Vijana ambao hawajapata mikopo ya Halmashauri pengine ni Wakenya

Usiume sana kijana,piga mahesabu tu,nchini hapa tupo jumla ya watu milioni 60!kama vijana ni milioni 30,hizo bilioni 150,ukizigawa kwa vijana kila mmoja anapata buku Tano tu!!!hata kilo ya nyama hainunui!!
 
Serikali ya Tanzania imedai bungeni leo kwamba imekwisha mwaga kitita cha Tsh Bilioni 150 kwa Halmashauri zote nchini , kwa lengo la kutoa Mikopo kwa Vijana ( MAMA ANAUPIGA MWINGI ) , Na kwamba Vijana wote wa Kitanzania waliohitaji Mikopo hiyo wamekwisha pata na wanaendelea na shughuli zao za ujasiria mali kama kawaida , na KWAMBA KAMA KUNA KIJANA ALIYEHITAJI PESA HIZO NA HAJAPATA BASI LABDA NI MKENYA .

Taarifa hiyo Nzuri , kabambe na ya kutia moyo imetolewa na Naibu Waziri Mh Katambi kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea Dodoma .

Mungu ibariki Tanzania .
 
Nchi hii ngumu sana wasukuma wanalewa madaraka mapema sana
 
Hiyo mikopo inaishiaga mifukoni mwao. Procedure zenyewe za kuipata ni shughuli pevu.
 
Wapiga makofi/wagonga meza nao hawakuwa nyuma kama kawaida yao.
 
Nchi hii basi imejaa wakenya, watanzania wajitokeze tuwajue!
Aaaagh nimechokaaah! Seriously mwenye njaa hawezi tambuliwa na mwenye shibe!
 
Huyu inabidi akamatwe na kutiwa ndani au hata kupigwa vidole tu ili ashike adabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…