Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Atakuwa Prof Karim Manji huyo?
Sky Eclat pitia hapa
Tulikuwa na tabia ya kupika wali kwenye ‘rice cooker’. Aliyekuwa Mrajis Msaidizi wakati huo alipiga marufuku, kwa sababu za kiusalama. Hatukuacha. Tulijificha zaidi.
Siku moja akafanya ukaguzi wa kushtukiza. Dogo alikuwa anapika. Mimi sipo. Watu wakakimbia wakaambizana. Dogo naye akapata taarifa. Akatorosha vyombo na misosi yote kwa dirishani, baada ya kufunga mlango kwa ndani na yeye akatoroka. Sijui alitorokaje. Ilikuwa floor ya kwanza!
Harufu ya wali iliyojaa chumbani ilisaliti. Profesa alikagua chumba hadi chumba huku akinusa harufu. Akabaini ni chumbani kwangu. Alikijua fika maana kilikuwa cha Rais mstaafu. Akafungua kwa ‘Master Key’ yake. Hakukuta mtu. Akaweka ‘lock’ ili nikirudi nikaripoti ndipo nifunguliwe.
Nikaarifiwa nikawahi maana la sivyo dogo angepata shida pa kulala. Mimi nilikuwa nishaoa na nimepanga Msasani. Kipindi hicho nilikuwa mwaka wa tano. Nililala chumbani pale mara chache tu nilipokuwa najisomea usiku wodini pamoja na wenzangu.
Nilipomfuata Prof., aling’aka kwa hasira, kwa kuwa hakuwa na ushahidi, na kwa kisirani, akanirudishia funguo zangu huku akiapa kunikomesha! Alianza kunitafuta darasani. ‘Akanikamata!’ #NjeYaBox #HK