Waziri Kigwangalla awacharukia wanaomsema hajui Kiingereza

Atakuwa Prof Karim Manji huyo?
 
Elimu yote ya juu inafundishwa kwa Kiingereza sasa utakuwaje msomi Kama hujui Kiingereza? Na uliwezaje kufaulu Kama Kiingereza hujui?
 
Ngeli ya Nyerere ilikua ni usipime mzee baba,watu waliosoma masters za huko edenburg mwaka1958 huwezi kuwalinganishana na PH.d za hawa masela wa pale mabibo.
 
Sasa ulitaka wachina wajuaje kiingereza wkt wao from elementary schools to university wamesoma kwa kichina,huoni ajabu mtu from form 1 to university(degree,masters,PH.d) anatumia kiingereza lkn mpk leo hakijui?
 
Tukizungumzia Kwa Africa peke yake yake, Kilimanjaro is both the tallest mountain and highest mountain.
 
Matatizo ya kuongea kiswahili kimoyo moyo na kubadilisha kwenda kingereza kumbe tunayo wengi. Siku prof ndalichako anamfokea mkandarasi wa kichina kwa kingereza nilitamani nizikwe kwa vichekoooo
 
Umeongea kitu niliwahi kusikia sehemu, éti hawafurahii sana mtu kuongea lugha yao huku akijitahidi kufata accent yao. Wanasema wanafurahi kukusikia ukiongea kwa accent ya kwenu. Kweli kabisa
 
Bora asingewajibu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Umeongea kitu niliwahi kusikia sehemu, éti hawafurahii sana mtu kuongea lugha yao huku akijitahidi kufata accent yao. Wanasema wanafurahi kukusikia ukiongea kwa accent ya kwenu. Kweli kabisa
Yeah boss ipo hivyo. Nawakubali sana hapo hawa watu.
 
People argue geography, others know English, dadeq!!
 
Haya ni matokeo ya "kujifunza lugha na kujifunza kuhusu lugha"
 
Akaazime kile Cha Mama wa Elimu,
"Put him inside"
 
Afu huyu kigwangala sio ndio madon wa qnet hapa bongo. Leo qnet wamepatwa....😂😂😂
 
.................................................................[snip]
Baadaye kikakaa kichwani,japo si kivile.Sasa WaTz wenzangu huu ujasiri wa kuchekana kwenye lugha za kigeni sijui tunautoa wapi.
Hiyo ni kawaida ya watu waliotawaliwa na kudhalauliwa. Huwa wakiachiwa uhuru bado wanapenda kuwa karibu na mtawala wao; kwa lugha, kwa kuvaa, kwa kutembea, n.k. TZ akina Kambona walikuwa bado wanachana nywele na kuzipasua kichwani kama mwingereza. Lugha ndo kabisaa! Hadi leo unaweza kupewa ajira kwa kuwakoga watu kwenye interview, hata kama taaluma ni sifuri.

Hapa JF utaona bado kuna watu wanazoza kwa kutamani sifa hiyo ingawa ukiwajaribu kwa thrd ya english, utaona wachangiaji wanapungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…