Waziri Kombo afikisha salamu za Rais Samia kwa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres, na kusisitiza dhamira ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, amani na maendeleo endelevu.

Baada ya mazungumzo yao, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) alimkabidhi Mhe. António Guterres zawadi ya kitabu kuhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua kuvutiwa kwa muda mrefu kwa Katibu Mkuu huyo na maono, uongozi na mchango wa Mwalimu Nyerere katika kuhimiza amani, maendeleo na ushirikiano wa kimataifa.

Chanzo: Instagram Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Juni 16, 2026
 
well done waziri balozi Kombo,
unafanya kazi nzuri sana Baba kwa niaba ya DR.Samia Suluhu Hassan na taifa letu kwa ujumla
 
Rais Fake Kapatikana kwa kura Fake na kapatikana kimiujiza yani kura zilipigwa Milioni 32.7 kwa muda wa saa 6 pekee.
Zikahesabiwa ndani ya saa 72 .

maana yake kura 126 zilihesabiwa kwa sekunde 1 na kura 7569 kwa dakika moja tu.
 
Rais Fake Kapatikana kwa kura Fake na kapatikana kimiujiza yani kura zilipigwa Milioni 32.7 kwa muda wa saa 6 pekee.
Zikahesabiwa ndani ya saa 72 .

maana yake kura 126 zilihesabiwa kwa sekunde 1 na kura 7569 kwa dakika moja tu.
Hiyo ndiyo abracadabra/the cadava itself!Ufala uliojaa pomoni kwenye kibuyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…