Waziri Kombo: Hatma ya maendeleo Afrika inategemea zaidi umoja wetu

Waziri Kombo: Hatma ya maendeleo Afrika inategemea zaidi umoja wetu

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) ameeleza kuwa hatma ya maendeleo ya kiuchumi Barani Afrika inategemea umoja ulio imara wa bara hilo.

Waziri Kombo ameeleza hayo alipochangia mjadala kuhusu “Kukua kwa Nafasi ya Afrika katika Siasa za Dunia” (The Rising Role of Africa in World Politics”) kwenye Mkutano wa 4 wa Diplomasia wa Antalya (Antalya Diplomacy Forum - ADF2025) uliofanyika Aprili 12, 2025 nchini Uturuki.

Akitoa mchango wake katika mjadala huo Mhe. Waziri Kombo ameeleza kuwa Afrika inahitaji kuwa na umoja thabiti utakaowezesha kujenga utamaduni wa kujadili kwa kina na uwazi masuala ya msingi ya maendeleo ili kupata ufumbuzi wa changamoto za kiuchumi zinazolikabili bara hilo kwa sasa.

Mbali na kuhimiza umoja, Mhe. Waziri Kombo ametoa mapendekezo kadhaa ya kuzingatiwa barani Afrika ili kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha ukuaji wa Uchumi yakiwemo maboresho ya mfumo wa elimu ambayo yatawawezesha vijana kujitegemea, kwa kutambua uwingi na thamani ya rasilimali zilizopo ili ziweze kutoa mchango chanya kwenye maendeleo ya uchumi.

Viongozi wengine waliokuwa katika mjadala huo ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Ivory Coast Mhe. Léon Kacou Adom, Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Maria Manuela Dos Santos Lucas, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Mhe. Samuel Okudzeto Ablakwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Liberia Mhe. Sara Beysolow Nyanti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Olivier Jean Patrick Nduhungirehe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin Mhe. Olushegun Adjadi Bakari, na Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Uturuki Prof. Mehmet Özkan.

Mkutano wa 4 wa Diplomasia wa Antalya ulifunguliwa rasmi tarehe 11 Aprili , 2025 na Rais wa Uturuki Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoğan, ambapo ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali, Mawaziri Wakuu, Mawaziri wa Mambo ya Nje, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, watunga sera, wafanyabiashara, wanataaluma, na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka sehemu mbalimbali duniani.

IMG-20250412-WA0130.jpg
IMG-20250412-WA0134.jpg
IMG-20250412-WA0138.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250412-WA0125.jpg
    IMG-20250412-WA0125.jpg
    112.3 KB · Views: 27
  • IMG-20250412-WA0144.jpg
    IMG-20250412-WA0144.jpg
    335.9 KB · Views: 28
  • IMG-20250412-WA0137.jpg
    IMG-20250412-WA0137.jpg
    319.1 KB · Views: 19
  • IMG-20250412-WA0131.jpg
    IMG-20250412-WA0131.jpg
    375.7 KB · Views: 25
  • IMG-20250412-WA0146.jpg
    IMG-20250412-WA0146.jpg
    401.4 KB · Views: 29
  • IMG-20250412-WA0140.jpg
    IMG-20250412-WA0140.jpg
    310.1 KB · Views: 25
  • IMG-20250412-WA0132.jpg
    IMG-20250412-WA0132.jpg
    395.3 KB · Views: 26
Tunaijua Afrika ,mkwamo wake unatokana na Viongozi wapuuzi wapuuzi .

Wewe una Makaa ya Mawe, una Chuma, alafu mpaka Leo unaagiza chuma Nje
 
Back
Top Bottom