Waziri Lukuvi: Kuanzia sasa ukiwa na kiwanja kinatakiwa kiitwe kwa jina lako na la mke wako

Kwani unafikiri hata sasa hivi Bank inachukua hati bila kibali cha mke au mme kama mali ni ya familia? Fanya utafiti kidogo kabla ya kuja na comment hapa mkuu!
Na bank wakijaribu kuchukua hati bila consent ya mke, mdaiwa akishindwa kulipa mkopo bank hawawezi kuichukua mali ya familia km itathibitika mahakamani mke hakuwa na taarifa juu ya huo mkopo.
 
Binafsi kwenye maelezo yake sijaona tamko lolote. Naona ameleta awareness tu kwenye sheria iliyopo kuwa iko flexible.
 
Mturuhusu na akina Joyce Mukya tuwaandikishe maana huku vyumbani ni balaa.
 
Shida ni kuna wanawake nyoka mfano wa hua(Njiwa)
 
Lukuvi anasema 'hati inaruhusu' sasa wasoma vichwa vya habari mnaanza kumponda mzee wa watu bure. Yeye anasema inaruhusiwa katika hati kuandika majina ya mke watoto n.k ili kuelusha migogoro. Akashauri hasa wanawake watumie fursa 'kuwashawishi' waume zao kiwaandika. Msimshambulie mzee wa watu jamani hajawalazimisha na wala sheria hailazimishi.
 
Waziri angefanya kwanza consultation
Sheria ya ndoa ya 1971 inaruhusu kila mwana ndoa kumiliki mali separate
How under this juncture be applicable
 
Jamani waheshimiwa hii sio lazima 😊

Waziri katoa ushauri tu
 
Kama nimeelewa ni kwamba kwa sasa upo huo uwezekano wa kuandikisha Mke, Mume n.k.....sidhani kama amesema ni lazima maana nasoma baadhi ya comment naona Watu wanatanguliza tu mihemuko.
 
Nnaona mna comment kwa mhemko, mamlaka ya kufanya hivyo yapo wazi na ni suala la wake zetu kutushawishi, hata kwa ndumba tukawaweke kwenye hati ila siyo lazima
 
Waziri ameghafilika tu hakuna hitaji la kisheria kama hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…