Waziri Lukuvi: Kuanzia sasa ukiwa na kiwanja kinatakiwa kiitwe kwa jina lako na la mke wako

Huyu jamaa anazeeka vibaya..Spouse consent inatosha...awe mke au Mume. Kama mmeweza kuiba kura katika uchaguzi mkuu mnadhani yakiwekwa majina mawili kuchakachuka kutaisha?>
 
Heading na maelezo vinatofautiana.

Waziri ameshauri hajalazimisha. Mleta mada amepotosha.
 
Wana Habari mnadhalilisha taaluma yenu.

Lukuvi wote tumemsikia, hajasema hayo maneno. Of course sijasoma habari yako yote nimeona imejaa upuuzi tu.

Alichosema Lukuvi ni kwamba anatoa wito kwa wamama kushawishi waume zao pale wanapomilikishwa viwanja basi Hati za viwanja hivyo viwe pia na majina yao.

Hivyo ni suala la wito tu.
 
Kama nimeelewa ni kwamba kwa sasa upo huo uwezekano wa kuandikisha Mke, Mume n.k.....sidhani kama amesema ni lazima maana nasoma baadhi ya comment naona Watu wanatanguliza tu mihemuko.
Halafu hilo suala halijaanza sasa. Limekuwepo muda mrefu sana. Tuna viwanja vina majina mpaka ya watoto (minors) vinakuwa chini ya waangalizi (guardians).
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema sheria inaruhusu kuandikwa majina yote mawili ya wenza katika hati za umiliki ardhi na Wizara ya Ardhi imekuwa ikisajili Hati nyingi zenye majina yote mawili ya wenza na wengine husajili na majina ya watoto wao.
 
Kwani unafikiri hata sasa hivi Bank inachukua hati bila kibali cha mke au mme kama mali ni ya familia? Fanya utafiti kidogo kabla ya kuja na comment hapa mkuu!
Kwani unafikiri hata sasa hivi Bank inachukua hati bila kibali cha mke au mme kama mali ni ya familia? Fanya utafiti kidogo kabla ya kuja na comment hapa mkuu!
Hilo kila mtu analijua " spouse consent" hoja yangu iko kwenye utitiri wa beneficiaries wote kuandikwa kwenye title ina sense gani?! Ni upuuzi tu!
 
Hapo kwenye kuweka jina la watoto sawa....ila kuweka jina la hawa viumbe wengine kunawatengenezea picha kichwan mwao ambazo hatuzijui kabisa.
 
Safi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…