Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema haya...

“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei”.

“Kauli ya uhakika ni ya Serikali. Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika. Pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada”.

Pia soma > TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15
Mimi hapo namuamini Mkurugenzi wa TPDC,
 
Wanatia kinyaaa sana maana huyo Makamba kaingia wizarani wakati ipo hali ya mafuta ipo stable.

Sasa ameingia akaanza fujo zake na sasa tunakaribia kuingia kwenye mdororo wa upatikanaji wa mafuta.

Kubali kataa hili ni tatizo la kutengeneza makusudi maana ufisadi wa kwenye nishati siku zote huwa ni wa matrillion
Ndio wanaanzaga kuyumbisha process taratibu na kutengeneza uhaba matokeo yake ni upigaji kwa njia ya kuleta rescue plan!

Ubaya wa huyu jamaa yani anaonekana ana mawenge anataka atege mabomu ya upigaji sector zote kwa mara moja yani! Ina maana kule JKNHPP kashaharibu na huku kwenye mafuta soon anaharibu. Halafu hatumii weledi yani kuandaa mashambulizi anakurupuka kiasi kwamba watu tunasanuka wazi kabisa kwamba kipigo kiko live!

Tutegeemee petrol kufika tsh.3000 ili kupenyeza channel yake ya kudokoa mapene humo
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema haya...

“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei”.

“Kauli ya uhakika ni ya Serikali. Mkurugenzi wa TPDC atatoa taarifa kuhusu taarifa yake hii manake aliitoa kwenye semina ya wanahabari lakini ni gazeti moja tu ndio limeandika. Pia atakuja ofisini kutoa maelezo kabla hatujachukua hatua za ziada”.

Pia soma > TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15
Mkurugenzi wa TPDC si mteule wa Rais sasa waziri yeye ana mamlaka gani ya kumuoji au ndo Yale ya Nape kumuundia tume mkuu wa mkoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio wanaanzaga kuyumbisha process taratibu na kutengeneza uhaba matokeo yake ni upigaji kwa njia ya kuleta rescue plan!

Ubaya wa huyu jamaa yani anaonekana ana mawenge anataka atege mabomu ya upigaji sector zote kwa mara moja yani! Ina maana kule JKNHPP kashaharibu na huku kwenye mafuta soon anaharibu.

Tutegeemee petrol kufika tsh.3000 ili kupenyeza channel yake ya kudokoa mapene humo
Exactly
 
Naona na hili wame likwepa kisiasa hawataki tujue ukweli

SUBIRI KIDOGO
 
Kwa akili zako huo ndo uthibitisho wako?

Kumbe naweza kuwa najaribu kumuelewesha au kuomba ushahidi kwa chizi humu
 
hizi kazi za kupewa kwa hisani ndo zinalirudisha nyuma taifa, kwenye wizara hiyo makamba ni kama debe tupu
 
Lengo la makamba nikutaka kumuondoa mataragio..kumbuka Samia siku anaingia ofisini alimuondoa na kumtangaza uvccm wa bsc community development kuwa DG wa TPDC baada ya watu kupiga kelele ndo akapatilisha..So bado amataragion wamemuwinda na soon ataondolewa
 
Pamoja na yoteyote binafsi ya Makamba Jr.

Naona yuko kwenye pressure sana, either kuna watu wanataka afeli au tayari mbio za Urais zimeanza kuna watu wanataka wamuharibie, maana kila kukicha linazuka jipya.

Makamba Jr kuwa mtulivu inaonekana upo kwenye vita kali, tumia akili kwenye kufanya mambo yako, hiyo wizara ni kubwa na ina mambo mengi, uko mtegoni.
Mkuu je anakusikia?
 
Ninashauri iundwe tume ya kuchunguza uwepo wa mafuta au la. Makamba anaingiza nchi ngizani kwa maneno yake mengi yasio na mwisho wala mwanzo.
Changamoto ninyo iona mie madam president hawez kutegua uteuz wake ever maaaana anakuja ataonekana katoa boko
 
Back
Top Bottom