Kote unavyoenda nje umekosa watu wa kushirikirikiana na Serikali kwa mfumo wa PPT?
Huyu Waziri wako mhujumu uchumi toa tupilia mbali fursa imefunguka anaongea ujinga matajiri kibao wa nje waweza kuja hata Kesho wakawekeza uwekezaji aa uhakika wana mipesa na teknolojia
E Mungu nini hiki kaongea Makamba
Naona ama unaongea kwa ushabiki au huna taarifa sahihi. Hebu tafakari yafuatayo:-
1. LNG Processing Plant peke yake itagharimu almost USD 30 Billion!!
Hivi una habari Market Capitalization ya Biashara zote kubwa Bongo zinaweza zisifike hata 50% ya hiyo USD 30 Billion?!
Nani anaweza kukukopesha almost Sh 70 Trillion kwa ajili ya ujenzi wa Plant ya kuchakata gesi TU?!
2. Kwavile hatuna skills wala technology labda tunaweza kufanya management contract with high skilled and expertize!!
Data zilizopo zinaonesha kiasi kikubwa cha gesi kipo deep sea (more than 2 km from the shore) huku zikiwa kwenye kina kirefu (again almost 1 km from sea surface)
Again, kama LNG Processing Plant tu inachukua almost 70 Trillion, umeshajiuliza investment cost za uchimbaji itakuwa trillion ngapi kabla hatujaanza kuuza tone la kwanza? Na ni nani anaweza kukukopesha hizo? Yule yule aliyekukopesha trillions za kujenga LNG Plant, ama?
2. Gas Exploration ilifanywa na Oil Companies kwa gharama zao. Umetumia pesa kidogo sana kwa kisima kimoja TU JUST for exploration, basi utatumia Sh 50 Billion! Unverified reports zinasema maandalizi yote hadi sasa yamekula zaidi ya TZS 5 Trillion.
That said, kama tunaamua kuchimba wenyewe basi tunatakiwa ku-refund hizo!!
Now tell me: Ni taasisi ngapi TZ zina uwezo ku-mobilize capital ya angalau hiyo 5 Trillion just for refund kabla hatujagusa hiyo LNG Plant?
Btw, ikiwa Kamanda Magu alishindwa kujenga hata Copper Smelter as a result of Mgogoro wa Makinikia. Utafiti wa mwanzo ulionesha thamani ya Smelter by the time ilikuwa USD 500 MILLION (TOP)!
Sasa ikiwa tumeshindwa kujenga hata Smelter isiyofika hata USD 1 Billion, ndo tutaweza kujenga plant ya USD 70 Billion?
Ngoja nikuambie! Pamoja na porojo mnazoambiana hapa JF na porojo zingine kutoka kwa wanasiasa, ukweli mchungu ni kwamba TAIFA LENU NI MASKINI WA KUTUPWA!! Eti Tajiri namba 1 nchini ana utajiri sawa na Jigga huku utaji wenyewe hata Wabongo wenzake wanatilia mashaka... halafu ndo muwe na ubavu wa ku-invest kwenye gesi?!