Waziri Makamba: Tanzania kuanza kuuza gesi nje "labda" baada ya miaka 6 kuanzia sasa

Waziri Makamba: Tanzania kuanza kuuza gesi nje "labda" baada ya miaka 6 kuanzia sasa

Huyo kawekwa hapo ili nuone kwamba urais hauwezi kama anavyopigiwa debe na vipofu wa nchi hii!
 
Akihojiwa na BBC leo kuhusu uwezekano wa Tanzania kuchukua fursa hii ya vita baina ya Russia na Ukraine kuuza gesi yake nje ya nchi Waziri wa Nishati Mhe. Makamba amesema uwezekano huo haupo labda baada ya miaka 6 kuanzia sasa ndiyo miundombinu wezeshi inaweza kukamilika na kuanza kazi.

Watanzania bado tuna safari ndefu kuanza kutumia na kufaidi uchumi wa gesi.
Bure tu huyo mission town. Kimagufuli ingewezekana miaka hata mitatu tu tungeweza kuanza kuuza gesi nje.
Unafikiri ukiwasikiliza na kufuata ushauri wa wenye maslahi tayari soko la gesi utafanikiwa?
 
Issue sio kuuza tu hata ikichukua miaka 10, issue tutakula percent ngapi?

Pia tukianza hii LNG competitor sio Russia tena Bali ni USA na soko sio Ulaya tu hata China na Japan
 
Hatuna brain ya kufikiria kufanya project kubwa, hii ilikuwa fursa nzuri sana na soko lipo kubwa sana, Ila twende mbele turudi nyuma hatujui walikubaliana nini na wachina
 
Katoa jibu lipi?

Kama kazungumzia Wawekezaji kutoka nje, huo ndo ukweli wenyewe! Hata uwe na hasira vipi ukweli huo huwezi kubadilika kwa sababu kama taifa hamna ubavu wa ku-mobilize hiyo capital unless tuendelee na usemi "Tuiache tu ardhini kwa sababu haiozi"

Huo ndo ukweli mchungu unaotakiwa kuumeza, na kama utalazimika kuutema basi usieteme kwa chuki na hasira!

Ni uchungu ule ule ambao Msema Mbovu Muhongo alisema wazi kwamba "Wafanyabiashara wa Tanzania mna pesa za kutengenezea juisi tu lakini sio ya kuchimba gesi"
Tatizo watu wanamkosoa makamba wakiwa wanaongozwa na chuki juu yake,
 
Bure tu huyo mission town. Kimagufuli ingewezekana miaka hata mitatu tu tungeweza kuanza kuuza gesi nje.
Unafikiri ukiwasikiliza na kufuata ushauri wa wenye maslahi tayari soko la gesi utafanikiwa?
Magufuli alikuwepo kwa zaidi ya miaka 5 hakuweza, Kimagufuli gani hicho?
 
Kuna Msukuma alituchelewesha sana.... maana yake kama tungeanza 2015 + 6 years = 2021

Hata hivyo bado fursa zipo, EU imeamua kuiweka gas kwenye "clean energy" category pia mpaka mwaka 2030 wanataka waachane kabisa na gesi ya Urusi.

Piga kazi bwana January
 
Na ile gas waliosaini kenya Rais wetu na Uhuru ni ipi? Nasikia kuna Gas Mtwara, Lindi, Kilwa sijui ni ipi masoko au kivinje au kipatimu na mkoa wa pwani!!!! Na ile gas walipewa Wachina ni ipi?
 
Akihojiwa na BBC leo kuhusu uwezekano wa Tanzania kuchukua fursa hii ya vita baina ya Russia na Ukraine kuuza gesi yake nje ya nchi Waziri wa Nishati Mhe. Makamba amesema uwezekano huo haupo labda baada ya miaka 6 kuanzia sasa ndiyo miundombinu wezeshi inaweza kukamilika na kuanza kazi.

Watanzania bado tuna safari ndefu kuanza kutumia na kufaidi uchumi wa gesi.
Yaani bila aibu anazungumzia kuhusu kuuza gas nje ya nchi ilhali hata hapa Nchini tu, tena Hapa Dar es Salaam hiyo gesi haijafikia hata 3% ya Population.
BBC wawe wanauliza Maswali ya Maana
 
Ndo maana nikahoji hizo taasisi ni zipi?!

Nchi hii, nchi zingine nyingi, mifuko ya kijamii ndo huwa na pesa ya kutosha kwa sababu wao huwa wanafanya kazi ya kuingiza tu!!

Now tell me: Hivi mifuko ambayo hata kulipa wastaafu bado inakuwa mgogoro, hivi unaamini wanaweza kuwa na ubavu wa ku-mobilize angalau USD 1 Billion?

Hivi ukiondoa NSSF, ni mfuko gani mwingine wenye pesa ya maana?!

Acha hiyo mifuko ya kijamii... taasisi nyingine ni ipi? TPA?! Mabenki ambayo yote kwa ujumla deposits zao hazifiki hata USD 1 Billion?

Man...

Hakuna anayependa kampuni za nje ndo zije kuchimba gesi!

Back in 2000's niliwahi kuandika makala ndeeefu kwenye Gazeti la Rai kuhusu ni namna gani Tanzania tungeweza kuitumia NICOL kama capital mobilization basket ili investments kubwa kubwa ziwe zinatumia domestic capital na hatimae klu-enjoy multplier effect, kumbe NICOL yenyewe ilikuwa na mkono wa "Wajanja"

Back 2015 nilishaandika post ndeeefu kuhusu namna gani TUNAWEZA KUSHIRIKI kwenye Upstream Segment of Gas Industry.

Yote hiyo ni katika kuona na kuelezea umuhimu wa kuwekeza sisi wenyewe lakini siwezi kujitia upofu na kuamini eti Serikali kupitia PPP Locally tunaweza kufanya kwa 100%... hatuna huo ubavu at least for now!!

Unatumia vyanzo gani vya takwimu? Customer deposits za CRDB pekee yake, kwa mfano, zinazidi US$2 billion, lakini wewe unadai customer deposits za mabenki yote hazifiki hata US$1 billion!
 
Kwani wenye gesi huko kusini akina Mmawia wanasemaje?
Bwashee alaaniwe fisadi Kikwete kwa kutudanganya kuwa kusini itakuwa kama Dubai kumbe alikuwa anapora gesi yetu kuwamilikisha wachina. Kwa ufupi gesi tulipigwa, na aliyetupiga ni Jakaya Mrisho Kikwete
 
Yaani bila aibu anazungumzia kuhusu kuuza gas nje ya nchi ilhali hata hapa Nchini tu, tena Hapa Dar es Salaam hiyo gesi haijafikia hata 3% ya Population.
BBC wawe wanauliza Maswali ya Maana
Si unajua nao BBC wanatafuta uteuzi katika serikali, hivyo hawawezi kuuliza maswali ya kuivua nguo!
 
Unatumia vyanzo gani vya takwimu? Customer deposits za CRDB pekee yake, kwa mfano, zinazidi US$2 billion, lakini wewe unadai customer deposits za mabenki yote hazifiki hata US$1 billion!
Hapo kwenye deposit ya $ 1 Billion ni typing error! Ukiangalia nilitangulia kwa kusema kwa kusema hawawezi kuwa na ubavu wa ku-MOBILIZE USD 1 Billion!!!

Hiyo uliyotaja wewe ni Pesa ya Wateja na sio ya Benki na kwahiyo huwezi kuziitia kwenye long term investment ambayo haiwezi kukupa return ndani ya muda mfupi!!! Kwa project kama ile, average time kuanza kuingiza pesa ni at least 8 years!!
 
Uliyesema “Mabenki ambayo yote kwa ujumla wake deposits zao hazifiki hata…” ni wewe, sio mimi. Kwani deposits huwa ni pesa gani kama sio pesa ya wateja. Haikugharimu kitu kusema ulikuwa mistaken kwenye comment yako on bank deposits!
 
Mwambie asihangaike na hiyo gesi kwanza pesa ya kuchimba wanayo? au ndio wanasubiri "mikopo nafuu"?

Atuambie ile winchi ya tani 26 aliyoagiza kwa ajili ya Nyerere Dam toka nje iko wapi?
Muhimu hilo, crane la tani 26 liko wapi?
 
Back
Top Bottom