Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanza wangehakikisha maviwanda yote Nchini yanatumia hiyo gesi kama nishati kuu, kisha wazalishe LPG ishuke bei 50% ilivyo hivi sasa. Mara baada ya hapo ndo wafikirie kioeleka Nairobi, kampalaa na kwengineko
Piga kazi bwana January
Kama ndiyo hivyo, Mkuu, mbona unashawishi (joking) tusiwashe umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo inawezekana hata miaka miwili haitakaisha kama tukiwa serious kulimalizia?BAADA YA Miaka 6, sawa...
Pre-FEED about 2 years
FEED... at least 2 years
Project Execution... about 5 years
Kuna uwezekano kama SSH atarudi tena madarakani 2025 basi anaweza kuondoka huku akiacha tukiwa hatujauza hata tone moja!!
Hila ndugu yangu wewe unatakiwa kupewa ukuu wa chuo kipya kitakachojengwa maalumu kwa taaluma ya......Mambo ni mengi muda ni mchache!
Iliagizwa Ukraine!Mwambie asihangaike na hiyo gesi kwanza pesa ya kuchimba wanayo? Au ndio wanasubiri "mikopo nafuu"?
Atuambie ile winchi ya tani 26 aliyoagiza kwa ajili ya Nyerere Dam toka nje iko wapi?
Unataka ligi isiyo na msingi...Uliyesema “Mabenki ambayo yote kwa ujumla wake deposits zao hazifiki hata…” ni wewe, sio mimi. Kwani deposits huwa ni pesa gani kama sio pesa ya wateja. Haikugharimu kitu kusema ulikuwa mistaken kwenye comment yako on bank deposits!
Mkuu wangu,Kama ndiyo hivyo, Mkuu, mbona unashawishi (joking) tusiwashe umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo inawezekana hata miaka miwili haitakaisha kama tukiwa serious kulimalizia?
LOL! Yaani ndugu yangu ungejua jinsi ilivyonitesa kuitafuta ile post yako! Siku naitafuta nikakumbuka siku niliyokueleza kwa tambo kwamba "...window ya ile nimeiacha active ili niweze kuirejea"!Halafu siku hizi Mkuu wangu unasusia maswali yangu sijui nikuudhi nini. Ha ha haaa!
Siku kina Sunday wakiwa Monday, January naye atakuwa FebruaryBado tu ni January ??! hajawa February ??!
Ha ha haaa! Tupo pamoja mkuu. Yawezekana, kuna anayetuhujumu tusiwekaribu zaidi...sasa sijui mimi na wewe Mkuu wangu tukiwa karibu tunahatarishaje maslahi yake.Sasa ilitokea tokea vipi hadi nikaifunga, only God Knows
Sasa wewe njemba mbona umefunga PM bwanaaa, mdogo wako nakutafuta sana!Mkuu wangu,
Mimi msimamo wangu kuhusu JNHPP upo wazi kabisa, na nilishawahi kuuzungumzia hapa na ndugu yetu MALCOM LUMUMBA wiki chache tu zilizopita! Kama hukuona uzi wangu ule, basi msimamo wangu kwa meneno machache ni huu:-
1. Mwanzoni nilikuwa naipinga JNHPP kwa sababu tulikuwa na best option ya kupata umeme mapema zaidi.
JK alimrahisishia sana kazi JPM pale alipofanikisha kuvuta gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi. Lengo la JK Administration ilikuwa ni kujenga 4 Power Plants pale Kinyerezi kutokana na ile gesi lakini kwavile muda wake ulishaisha, alifanikiwa kujenga moja ambayo ilizinduliwa October 2015, na akaacha Mchakato wa Kinyerezi II.
JPM alipoingia madarakani alimalizia tu ile Kinyerezi II lakini akapiga chini KInyerezi III na IV. Hizi Kinyerezi III na IV zisingehitaji investment kubwa wala muda mwingi kama JNHPP! Which means, kama JPM angeamua kujenga KInyerezi III na IV, angekuwa ametangulia mbele za haki wakati tayari Kinyerezi III na IV zimeshakamilika na kuongeza AT LEAST 300MW.
NB: Gesi ya kuzalisha umeme TAYARI IPO... ni ile ya Msimbati na Songosongo kwahiyo haihusishi hiyo miaka 10 niliyotaja hapo juu!
2. Kwavile JPM alisha-opt kujenga JNHPP, binafsi nitakuwa mtu wa mwisho kuunga mkono jaribio lolote la kuachana na JNHPP! We've already invested a lot of money kwahiyo itakuwa ni ujinga wa SGR kutelekeza JNHPP. Hatuwezi kufanya yale yale ya JPM ya kupiga stop Miradi wa NSSF kama vile Eco Village wakati tayari mradi ulishameza billions of Tanzanians Employees!
That being said, kwa sasa sina namna... LAZIMA niunge mkono umaliziaji wa JNHPP lakini but am not optimistic when it comes to people's believe kwamba ni mradi wa umeme wa bei rahisi, na nilishaelezea kwanini tusitarajie kwamba tutaanza kupata umeme wa bei rahisi hata JNHPP ikishaanza kutoa umeme UNLESS TANESCO waanze ku-act KIUCHUMI ZAIDI.
Na hata wakishaanza ku-act KIUCHUMI ZAIDI, nilishaelezea kwamba hiyo itakuwa itawezekana ndani ya miaka kadhaa tu, isiyofika hata 5, na matokeo yake inaweza ku-boost matumizi makubwa marudufu na hatimae kuamua kupandisha bei tena ili ku-discouarage matumizi makubwa ya umeme!
LOL! Yaani ndugu yangu ungejua jinsi ilivyonitesa kuitafuta ile post yako! Siku naitafuta nikakumbuka siku niliyokueleza kwa tambo kwamba "...window ya ile nimeiacha active ili niweze kuirejea"!
Sasa ilitokea tokea vipi hadi nikaifunga, only God Knows
Unataka ligi isiyo na msingi...
Hizo taarifa za CRDB sijaanza kuziweka jana, wala leo kwahiyo ninapojadili masuala ya kibenki huwa najua ninachojadili. Sasa kama hutaki kuamini habari za typing error, that's up to you lakini rudi kwenye hoja yangu ya msingi ambayo inazungumzia kutowezekana kwa Local PPP kwenye miradi mikubwa kama ya uchimbaji gesi!!
Jadili hiyo hoja niliyo-bold hapo juu ukihusisha hizo customer deposits zako!!
Ukweli ni kuwa "bwana yule" alitibua kila kitu kuhusu gas, mpaka wachimbaji wakaamua wakaitobolee kupitia Msumbiji.Akihojiwa na BBC leo kuhusu uwezekano wa Tanzania kuchukua fursa hii ya vita baina ya Russia na Ukraine kuuza gesi yake nje ya nchi Waziri wa Nishati Mhe. Makamba amesema uwezekano huo haupo labda baada ya miaka 6 kuanzia sasa ndiyo miundombinu wezeshi inaweza kukamilika na kuanza kazi.
Watanzania bado tuna safari ndefu kuanza kutumia na kufaidi uchumi wa gesi.
Na nimekuambia jadili hoja kwa kutumia hizo customers deposits zako, mbona umeshindwa?!Unayeendekeza ligi ni wewe. Huwezi kusema “customer deposits zako” wakati wewe ndiye uliyeingiza swala la deposits.
Hivi umesoma nilichaondoka?!Local PPP haina maana kwamba financing lazima ifanywe na local banks pekee yake. Local and foreign banks can work together (as a consortium) to offer a syndicated loan. Kama wapo (again, kama wapo) local investors ambao wanaweza kupata mikopo even from consortiums of local and foreign banks au kutoka taasisi zingine za fedha duniani (e.g., AfDB, IFC), hiyo bado itakuwa local PPP.
Hawa JF siku wanajijua wenyewe....Sasa wewe njemba mbona umefunga PM bwanaaa, mdogo wako nakutafuta sana!
Hahahaaaa!!!Ha ha haaa! Tupo pamoja mkuu. Yawezekana, kuna anayetuhujumu tusiwekaribu zaidi...sasa sijui mimi na wewe Mkuu wangu tukiwa karibu tunahatarishaje maslahi yake.
Na nimekuambia jadili hoja kwa kutumia hizo customers deposits zako, mbona umeshindwa?!
Tuwekee huo mchanganuo hapa kwa sababu hoja ni local investors na hizo TRILLIONS of Customers' Deposits!!
Hivi umesoma nilichaondoka?!
NI wapi nimesema Local PPP ni LAZIMA ifanywe na Local Banks?!
Nimetaja local entities kama vile Mifuko ya Kijamii na TPA kwa sababu ndio wanaonekana wana pesa! Aidha nilitaja local banks sio kama Lenders bali kama Investors kuonesha tuchukue local entities ZOOOTE tunazoamini kwamba zina pesa bado haziwezi kuwa na ubavu wa kufanya such massive investments!!!
Na hata tukichukua Banks as Lenders, hivi unafahamu hapa tunazungumzia mradi unaozungumzia investments yenye ukubwa kiasi gani?
LNG Processing Plant peke yake inatarajiwa kugharimu USD 30 BILLION... na hizo ni 2014/2015 estimations.
Kiasi kikubwa cha gesi kinapatikana deep sea... baadhi ya vitalu vipo over 100KM from OFFSHORE!
Ukishafika hizo +100KM, unaenda more than 2KM below the sea surface only to find the seabed, kisha unaenda tena more than 1KM below seabed!
Sasa ulishawahi kujiuliza gharama za uchimbaji wa gesi iliyo more than 100KM Offshore, and more than 3KM from water surface?
NI Foreign banks zipi zinazoweza kutoa mkopo kwa local investors (including the government) ambao kwa uchache ni ZAIDI YA SH TRILLION 100?!
Ni Local Investor yupi Tanzania mwenye sifa za kukopeshwa japo USD 1 Billion?!
Ni International Lender yupi duniani anayeweza kuikopesha Serikali ya Afrika angalau USD 10 Billion?!
Do I need to remind you kwamba unapokopesha serikali hususani kama ya Africa moja ya mambo unayotakiwa kuangalia ni Government Policies?!
Nani anaweza kutoa mkopo mkubwa kama huo kwa nchi ambayo huwezi kuwa hata na clue Rais ajaye priority yake itakuwa ipi?!
Wewe ungekuwa ni Bosi wa moja ya hizo benki ungekuwa tayari kutoa hizo pesa kwa mradi ambao huna uhakika kama serikali zote zitakazofuata zita-support project husika?!
Do I need to remind you wakati priority za JK zilikuwa Bagamoyo Port na Gas Industry lakini alipotoka tu madarakani aliyekuja baada yake hizo hazikuwa priorities zake?!
Do I need to remind you kwamba yule vyote alivyokuwa ameahidiwa Dangote na JK, Magu alivipiga chini?!
Unadhani hao international lenders hawaangalii mambo kama hayo ni kuyaona kama THREATS kwao especially kwa mkopo ambao biashara yake itaanza kuzalisha mapato at least in the next 8 years?!
Mnapenda sana kuongea mambo kirahisi rahisi!!