Waziri Makamba: Tanzania kuanza kuuza gesi nje "labda" baada ya miaka 6 kuanzia sasa

Ndio husisha taasisi za nje pesa huna, teknolojia huna pesa ipo nje na teknolojia ipo nje

Si uende PPP upate kodi wao wapate na wewe upate kodi foreign

Makamba alichojibu BBC ajitathimini kama anatosha
 
Hatari sana, kazi ya kutoa nchi hii kwenye umaskini haina tofauti na kazi ya Sisyphus
Acha kumsikiliza huyo..

Tanzania kuna a total of almost 57 Trillion Cubic Feet of Gas.

Gas ya Msimbati na Songosongo ambayo ni takribani 7.5 Trillion Cubic Feet ndiyo tayari imeanza kuchimbwa, na ndiyo ambayo, kwa ile ya Msimbati kama sikosei TPDC wana 20 or 25% share, ile ya Songosongo sikumbuki!

Mbali na hizo 7.5 Trillion Cubic Feet, 50 Trillion Cubic Feet bado zipo!!! Kiwango gani tunaweza kumiliki itategemea na uwezo wetu wenyewe manake kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta na Gesi ya 2015, mmiliki wa Vitalu ni TPDC ambae anatakiwa kuwa na AT LEAST 25% Production Sharing Agreement na percent inaongezeka with time!

Kama Taifa tutakuwa na pesa, tunaweza kuwa na zaidi ya 25%!
 
Makamba kajibu kitoto mno
McHale,ngano,sukari nkmbona tunaagiza nje wakati ndani tunao

Sembuse kama hatuna uwezo wa hizo gesi kwa nini tusitumie PPP?
Kajibu BBC kiswahili kama mswahili wa uswahilini ambaye hata shule hajawahi kanyaga
 
Ndio husisha taasisi za nje pesa huna, teknolojia huna pesa ipo nje na teknolojia ipo nje

Si uende PPP upate kodi wao wapate na wewe upate kodi foreign

Makamba alichojibu BBC ajitathimini kama anatosha
Ndo maana nikahoji hizo taasisi ni zipi?!

Nchi hii, nchi zingine nyingi, mifuko ya kijamii ndo huwa na pesa ya kutosha kwa sababu wao huwa wanafanya kazi ya kuingiza tu!!

Now tell me: Hivi mifuko ambayo hata kulipa wastaafu bado inakuwa mgogoro, hivi unaamini wanaweza kuwa na ubavu wa ku-mobilize angalau USD 1 Billion?

Hivi ukiondoa NSSF, ni mfuko gani mwingine wenye pesa ya maana?!

Acha hiyo mifuko ya kijamii... taasisi nyingine ni ipi? TPA?! Mabenki ambayo yote kwa ujumla deposits zao hazifiki hata USD 1 Billion?

Man...

Hakuna anayependa kampuni za nje ndo zije kuchimba gesi!

Back in 2000's niliwahi kuandika makala ndeeefu kwenye Gazeti la Rai kuhusu ni namna gani Tanzania tungeweza kuitumia NICOL kama capital mobilization basket ili investments kubwa kubwa ziwe zinatumia domestic capital na hatimae klu-enjoy multplier effect, kumbe NICOL yenyewe ilikuwa na mkono wa "Wajanja"

Back 2015 nilishaandika post ndeeefu kuhusu namna gani TUNAWEZA KUSHIRIKI kwenye Upstream Segment of Gas Industry.

Yote hiyo ni katika kuona na kuelezea umuhimu wa kuwekeza sisi wenyewe lakini siwezi kujitia upofu na kuamini eti Serikali kupitia PPP Locally tunaweza kufanya kwa 100%... hatuna huo ubavu at least for now!!
 
Mkuu, hata ukipata mwekezaji leo akaanza kazi 24/7 nakwambia atahitaji miaka zaidi ya 5 kuanza kusafirisha hiyo gesi nje akiwahi sana sana.

Nickel mwekezaji yupo site tayari ila productuon tunaambiwa itaanza 2025 kama atafanya kazi 24/7

So Makamba yupo sahihi, kuchimba nishati si biashara ya kitoto kama ya kuagiza kontena china kesho yake unatafuta fremu kariakoo.
 
Tatizo tuna mawaziri rafiki na rais, hawawezi kuwajibika kwa kulindwa hata wahoyange. Hili halikuwa jibu kwa mtu kama yeye.

Makamba ni kama taahira hivi. Wizara ya nishati ni kama inazidi kupoteza mwelekeo. Tumerudi kulekule kukatikakatika umeme kila mara.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Mpaka tuuze nje hapa nyumban imetosheleza mahtaj?

Tanesco wenyewe umeme ukikata wanawasha jenereta lao la dharula

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Chifu,

Kwa TANESCO hii, na miundombinu yake hii, chukua umeme WOOOOOOOOTE unaotumika Ulaya na America, kisha uhamishie Tanzania, bado tatizo la umeme HALITAISHA...

Nchi hii tukitaka stable power supply basi over 50% ya miundombinu ya umeme ifumuliwe vinginevyo, Grid ya Taifa inaweza kuwa na 10000000000000000 MW lakini mtaani kwenu mnakuja kukosa umeme wiki mzima kisa tu kunguru katua juu ya nguzo ya umeme, na hapo hapo nguzo ikala mwereka hadi chini...
 
Wanatusingizia sisi kunguru
 
Kwanza wangehakikisha maviwanda yote Nchini yanatumia hiyo gesi kama nishati kuu, kisha wazalishe LPG ishuke bei 50% ilivyo hivi sasa. Mara baada ya hapo ndo wafikirie kioeleka Nairobi, kampalaa na kwengineko
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…