Sijasema treatment iwe sawa, ila nauliza kama watumishi wengine hawastahili allowance kama hizo......yaani watumishi wengine hawadaiwi bili ya maji, umeme, kodi ya pango, usafiri kwenda na kurudi kazini, chakula wakiwa kazini (meal allowance), leta jibu lililojitosheleza......mbona sekta binafsi tunaona hizo allowance zikiwa zimeainishwa kwenye mshahara. Au kuondoa allowance ni njia ya kuficha ufinyu wa mashahara............maana laki tatu ukiichanganua uweke allowances za maji, umeme, pango, usafiri, chakula na ubaki hapo na mshahara itakuwa kichekesho.....