Waziri Medard Kalemani anadharaulika sana kuliko Mawaziri wote

Waziri Medard Kalemani anadharaulika sana kuliko Mawaziri wote

Waziri aache kutoa maagizo ya kisiasa kwenye mambo ya kiufundi na rasilimali huwapi watendaji...
Style ya utendaji kazi ya awamu ya tano imeharibu sana mind set za wanasiasa wetu. Waziri anataka kufanya kazi za Katibu Mkuu wa Wizara

Katibu Mkuu atafanya kazi za Wakurugenzi wa Idara. Wakurugenzi watafanya kazi za maofisa wa kawaida na za watendaji wengine.

Sio ajabu kumkuta Waziri akitamani kufanya kazi za makarani au hata masijala na walinzi kama kubeba na kupitisha ma file na kusimamia daftari la ku sign wakati wa kuingia na kutoka kazini

Bahati mbaya sana Mkuu wa Nchi alifurahia hilo na akawa anaonyesha kwa ishara kua asiyefanya hivyo basi huyo haendani ni kasi yake
 
Sijajua Waziri Kalemani anakwama wapi, hivi sasa yeye ndiye Waziri anayedharaulika kuliko Mawaziri wote,

Maagizo yake mengi yamekuwa yakipuuzwa sijui anacheka cheka na Raia au tatizo nini?..
Wesha mtenga Wenye CCM yao huyu ni Zao la Mwendazake

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Mbona huku songwe agizo lake limetekelezwa,tulikuwa tunakatiwa umeme kila weekend sasa hivi mambo poa,alikuja kuzindua umeme wa REA akatoa hilo agizo.
 
Tatizo lake kubwa ni kila sehemu alipo anataka sifa kwa kutoa matamko ambayo anajua kabisa kuwa hayawezi kutekelezeka!!ndio maana maagizo mengi anayoyatoa hayatekelezwi kwani yanakuwa nje ya uwezo wa hao anawoambia!!na ndio maana huwa hata hawezi kuwachukulia hatua hao anawowapa maagizo kwani , anajua kabisa kuwa anaongea kisiasa.
Akiwa Geita nilimsikia akitamka kuwa mradi wa bomba la Mafuta umekwishaanza in full swing wakati mpaka ninapoondika waguswa wa mradi hajalipwa hata mtu mmoja.
 
Mkitaka kumtoa mtoeni as long tunaelewa njama zenu tangia na tunajua pia hiyo wizara mnaitaka sana kwa ajiri escrow part2
 
Sijajua Waziri Kalemani anakwama wapi, hivi sasa yeye ndiye Waziri anayedharaulika kuliko Mawaziri wote,

Maagizo yake mengi yamekuwa yakipuuzwa sijui anacheka cheka na Raia au tatizo nini?..
Umesahau kuwa na Yeye Kipindi cha Mpwae ( Hayati Rais Dkt. Magufuli ) yupo ndiyo alikuwa Waziri si tu mwenye Dharau bali anayeogopeka pia katika Mawaziri wote. Kutesa kwa Zamu Ndugu.
 
Sijajua Waziri Kalemani anakwama wapi, hivi sasa yeye ndiye Waziri anayedharaulika kuliko Mawaziri wote,

Maagizo yake mengi yamekuwa yakipuuzwa sijui anacheka cheka na Raia au tatizo nini?...
Ni mtu yupo yupo tu! Niliwahi sikia maisha yake na mke wake wa kwanza hadi kifo cha mke huyo, nikaona tuna watu madarakani ambao hawakustahili kuaminiwa kabisaaaaa! Hopeless person!
 
Mnataka maisha yake personal mnataka awe malaika ama serikali yenu hii ya kubebwa na katiba mnadhani mmetimia? Ishu yenyewe kama zari vile bado mnajifanya eti leo hafai.

Ni waziri gani leo ana lolote la maana mnafikiri yupo smart wakati wote waota jua tu kama bosi. Miaka 5 iliyopita hakuna sekta ilifanya vizuri kama nishati ila nyie mmeshindwa kumtumia jamaa ndo mnatuletea upumbavu, vijijini kwenu kwa bibi zenu nani alipeleka umeme? Ni wapi mliona mgao? Na why today?
 
Mama anajua sana kutazama watu wanaofaa na sitoshangaa kusikia Kalemani anarudia kazi yake ya sasa.
Yaani wewe bado una imani na huyo unayemwita 'mama'? Mama! Huyu anayesikia wa-TZ wakikamuliwa na kuambiwa wahamie Burundi, yeye bado anachekea maelezo kama hayo? Huyu anayepiga simu kwa Kikwete kuuliza kila kitu? Bado unaamini amejaza busara kichwani?
 
Umeamua kuyapekua makosa yake na huwezi kuyakosa.
 
Na huyu Mkuu wa Mkoa wetu Makala naona na yeye anadharaulika sana. Kila agizo hakuna anayezingatia
 
Back
Top Bottom