Waziri Medard Kalemani anadharaulika sana kuliko Mawaziri wote

Waziri Medard Kalemani anadharaulika sana kuliko Mawaziri wote

Nimekuwa Kigoma yapata wiki.
Umeme unakuwepo kwa interval ya kila baada ya nusu saa kwa baadhi ya maeneo au kutokuwepo kabisa baadhi ya maeneo.

Umeme ni ule unaopatikana kwa kutumia generators /Mafuta.

Kuna mahala kuna Jamaa mmoja katengeneza mradi wa Umeme Jua ili apate kuunganisha kwa Tanesco, haijulikani iliishia wapi, jamaa amebaki na Umeme wake tele.

Waziri angelifikiria wazo la kupeleka Umeme wa grid ya Taifa kupitia Tabora au ule wa Rusumo mradi ukiisha utakaopitia Kakonko-Kibondo-Kasulu-Kigoma na baadae usambazwe maeneo mengine ndani ya mkoa.

Wananchi wa Kigoma wakipata Umeme ndani ya muda mfupi Mkoa utapaa katika kukuza pato la Taifa.

Kwa kuanzia Serikali kupitia Wizara ya Nishati waanze mazungumzo na yule mwekezaji wa Umeme Jua ili Wananchi wa kigoma wapate Umeme wa kutosha.
 
Sijajua Waziri Kalemani anakwama wapi, hivi sasa yeye ndiye Waziri anayedharaulika kuliko Mawaziri wote,

Maagizo yake mengi yamekuwa yakipuuzwa sijui anacheka cheka na Raia au tatizo nini?..
Ukioona hivyo ujue ni mla rushwa
 
Kile kilikuwa kipindi cha propoganda zaidi, sasa hivi hana haja ya kufanya propoganda
 
Tatizo lake kubwa ni kila sehemu alipo anataka sifa kwa kutoa matamko ambayo anajua kabisa kuwa hayawezi kutekelezeka!!ndio maana maagizo mengi anayoyatoa hayatekelezwi kwani yanakuwa nje ya uwezo wa hao anawoambia!!na ndio maana huwa hata hawezi kuwachukulia hatua hao anawowapa maagizo kwani , anajua kabisa kuwa anaongea kisiasa.
Kama lile la kusema mwananchi asiuziwe nguzo... ukifika Tanesco wanakuambia kama unasubiri nguzo za serikali bado hazijafika budget yake no budget so wew utaamua kunyoa au kusuka
 
Kama lile la kusema mwananchi asiuziwe nguzo... ukifika Tanesco wanakuambia kama unasubiri nguzo za serikali bado hazijafika budget yake no budget so wew utaamua kunyoa au kusuka
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Je ni nani alikuambia hivyo

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Sijajua Waziri Kalemani anakwama wapi, hivi sasa yeye ndiye Waziri anayedharaulika kuliko Mawaziri wote,

Maagizo yake mengi yamekuwa yakipuuzwa sijui anacheka cheka na Raia au tatizo nini?...
Dogo hapo hadharauliwi Waziri bali anadharauliwa aliyempa madaraka. Hata aliyeteuliwa leo nae atadharauliwa kwasababu mteuzi nae anadharauliwa!
 
Nguzo zetu zilizotakiwa zije mtaan kwetu mtaa wa kagera...ziliuzwa kwa watu wengine..na mpaka Leo hatuna umeme...mungu Kuna siku atawalipua wote hapo ofisini..same Kilimanjaro..
 
Nguzo zetu zilizotakiwa zije mtaan kwetu mtaa wa kagera...ziliuzwa kwa watu wengine..na mpaka Leo hatuna umeme...mungu Kuna siku atawalipua wote hapo ofisini..same Kilimanjaro..
Tena umenikumbusha eti wananchi walimtukana diwani wao ndo maana ziliuzwa kwingine yaani wamekosa umeme na ile ndo eneo lenye watu wengi wenye kujiweza kiuchumi na wengi wana nyumba za kisasa
 
Mpwa mwingine wa Magu out mama anajitaidi ikifika 2023 Sukuma gang itakuwa 2%
 
Back
Top Bottom