polokwane
JF-Expert Member
- Dec 16, 2018
- 3,361
- 5,842
Hadi sasa vilaza ndio walioko huko sasa sijui unafikirijeMnataka kupeleka vilaza wakafundishe vyuo vikuu. Hii nchi imekosa dira kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hadi sasa vilaza ndio walioko huko sasa sijui unafikirijeMnataka kupeleka vilaza wakafundishe vyuo vikuu. Hii nchi imekosa dira kabisa
Zamani Kuandika kwenye gazeti unakuwa profesa? Aliyeelewa tafadhali
Shukran sana mkuu kwa kuisapoti hoja. Tuna tatizo kubwa sana boss, mara ya mwisho nimepokea binti wa chuo hajui hata cheque ni kitu gani, hajui kujaza slip ya cheque, anatetemeka, ni kitu kipya kwake, hajawahi kukiona, ni jambo linalomtisha ila somo la Finance amefaulu na huenda katika mitiani yake ameshajibu swali la what is cheque, types of cheques kwa ufasaha.Tsh ametoa hoja yenye mantiki sana. inatakiwa idatishwe kule juu ya bandiko!!
Nahisi wengi hawajaelewa kilichoongelewa. Mkenda katoa maagizo baada ya matukio yanayoonesha kuna watu wana shahada za vyuo vikuu zisizoakisi uwezo wao wa kazi kuongezeka. Sasa si bora umsaili kabla ya kumuajiri? Tatizo liko wapi??Shukran sana mkuu kwa kuisapoti hoja.
Kweli nchi inaenda kubaya sana. Kwa hiyo wakifanyiwa usaili ndio elimu inakua bora. 😀😀😀😀😀.
Mtu mwenye GPA kubwa kwa vyuo kama SUA, MZUMBE na UDSM huyo anauwezo mkubwa, haina haja ya kujiuliza mara mbili.
Nenda uendako, kwenye usaili watu wanakalili na kufaulu baada ya hapo wanasahau. Ila mwenye GPA kubwa ni mtu mwenye uwezo.
Haiwezekani mtu kidato cha Nne abamize one ya saba, kidato cha sita one ya nne na chuo GPA ya 4.6. Useme hana uwezo badala yake utegemee kumpima kwenye usaili Ili kupima uwezo wake.
Tuwekeze kwenye practical zaidi
Bado huelewi mambo mengi. Watafute wenye GPA kubwa zaidi unaowafahamu, halafu angalia mafanikio yao ukilinganisha na wenye GPA za kawaida, halafu utatuambia.Kweli nchi inaenda kubaya sana. Kwa hiyo wakifanyiwa usaili ndio elimu inakua bora. 😀😀😀😀😀.
Mtu mwenye GPA kubwa kwa vyuo kama SUA, MZUMBE na UDSM huyo anauwezo mkubwa, haina haja ya kujiuliza mara mbili.
Nenda uendako, kwenye usaili watu wanakalili na kufaulu baada ya hapo wanasahau. Ila mwenye GPA kubwa ni mtu mwenye uwezo.
Haiwezekani mtu kidato cha Nne abamize one ya saba, kidato cha sita one ya nne na chuo GPA ya 4.6. Useme hana uwezo badala yake utegemee kumpima kwenye usaili Ili kupima uwezo wake.
Tuwekeze kwenye practical zaidi
Boss upo sahihi 100% kwenye hii comment uliyonijibu nimeedit na kuongeza mfano halisi kabisa. Halafu ni kama hawajui kuwa sekta binafsi ambayo inaajiri sana hawapendi kuajiri, wakulipe ili wakufundishe kazi wanataka wakulipe ili uzalishe na waone matokeo ndo maana hawajali vyeti siku hizi.Nahisi wengi hawajaelewa kilichoongelewa. Mkenda katoa maagizo baada ya matukio yanayoonesha kwamba watu wana shahada za vyuo vikuu zisizoakisi uwezo wao wa kazi kuongezeka. Sasa si bora umsaili kabla ya kumuajiri? Tatizo liko wapi??
Inawezekanaje mtu kamaliza chuo kikuu lakini hawezi kuandika barua yenye mantiki ya kuomba kazi? Au inakuwaje mtu aliyesema kwa kiingereza kwa miaka zaidi ya saba awe hawezi kuongea ama kuandika kiingereza kwa ufasaha? Mtu kama huyu ili ujue uwezo wake njia rahisi si kumsaili>
Watu waelewe kuwa ukubwa wa GPA hauhusiani hata kidogo na uwezo wa mtu kufanya kazi tarajiwa. Hayo uliyoyataja ya uzowefu, tabia, hari ya kufanya hiyo kazi, mwenendo wa muombaji, utayari wa kuifanya hiyo kazi kwa mazingira tarajiwa, ndiyo huzingatiwa kwenye kuajiri mtu na siyo GPA yake.inategemea na wasaili uelewa wao na aina ya kazi inayoombwa... Kwenye usaili tunapima uelewa, atitude, commitment, behaviour nk..
kwenye uelewa itategemea aina ya kazi na uzoefu unaotakiwa... kama ni uzoefu wa zaidi ya 2yrs kwenye field fulani hapa unaweza kushangazwa na hata mwenye GPA ya 2.0....
Acha uhuni tunazungumzia elimu. Mwenye GPA ndogo hana uwezo kielimu.Bado huelewi mambo mengi. Watafute wenye GPA kubwa zaidi unaowafahamu, halafu angalia mafanikio yao ukilinganisha na wenye GPA za kawaida, halafu utatuambia.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatareeee tupu.H
Hiyo kitaalamu inaitwa," Ungaunga Mwana Tusonge na kwa kizalamo tunasema Academic Networking"
Elimu ni nn? Maana hapa ndo tatizo linapoanza.Acha uhuni tunazungumzia elimu. Mwenye GPA ndogo hana uwezo kielimu.
Huo ni mfumo uliotengenezwa, lkn GPA kubwa itabakia kuwa na uwezo. Yaani mtu ana GPA kubwa ya mathematics alafu azidiwe kwenye namba na mwenye GPA ndogo. 😀😀😀😀😀. Hizi ni chai.Watu waelewe kuwa ukubwa wa GPA hauhusiani hata kidogo na uwezo wa mtu kufanya kazi tarajiwa. Hayo uliyoyataja ya uzowefu, tabia, hari ya kufanya hiyo kazi, mwenendo wa muombaji, utayari wa kuifanya hiyo kazi kwa mazingira tarajiwa, ndiyo huzingatiwa kwenye kuajiri mtu na siyo GPA yake.
Kuna usaili unafanyika wanaachwa wenye shahada wanachukuliwa watu wa kidato cha sita.
Hili swali lako haliendani na uhalisia. Shida ni kwamba huko makazini mnafanya kazi za kukusanya mafaili na kuweka kabatini. 😀😀😀Elimu ni nn? Maana hapa ndo tatizo linapoanza.
Mfano: Kujua Kusonga ugali ukaiva hiyo ni elimu.
Sasa mwenye A+ ya kusonga ugali kwenye makaratasi na anayesonga ugali kwa exposure na uzoefu nani ana elimu yenye uzalishaji halisi?
Hii umekosea. Hebu nikupe mfano kwa kuuliza swali.Acha uhuni tunazungumzia elimu. Mwenye GPA ndogo hana uwezo kielimu.
Kipindi cha nyuma nimebahatika kuchaguliwa kuwa kwenye kamati za ajira za baadhi ya taasisi hapa Tanganyika, hichi unachokisema labda nje ya nchi ila hapa nchini? Aisee hapana. Ukiajiri pima IQ achana na makaratasi ya GPA.Huo ni mfumo uliotengenezwa, lkn GPA kubwa itabakia kuwa na uwezo. Yaani mtu ana GPA kubwa ya mathematics alafu azidiwe kwenye namba na mwenye GPA ndogo. 😀😀😀😀😀. Hizi ni chai.
Yaani mtu ana GPA kubwa ya coding alafu azidiwe coding na mtu mwenye GPA ya 3. 😀😀😀😀😀😀
Sawa, wewe umesema na kuhitimisha. Basi ibaki kuwa hivi ulivyowaza.Hili swali lako haliendani na uhalisia. Shida ni kwamba huko makazini mnafanya kazi za kukusanya mafaili na kuweka kabatini. 😀😀😀
A little too late...hii ya kulazimisha GPA kubwa wabaki vyuoni imetengeneza matatizo makubwa kuliko hata faida.Kuanzia sasa Serikali itaanza kuzitazama ajira za vyuo vikuu badala ya kuangalia ubora wa ufaulu yaani GPA pekee sasa waajiriwe kwa kupimwa uwezo wao kwa kufanya usaili.
Kuangalia ufaulu pekee wa wanafunzi haitoshi kuboresha elimu badala yake ni muhimu kuongeza vigezo hivyo katika mapitio ya sera na mabadili ya mitaala jambo hilo litatazamwa kwa weledi mkubwa.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba 2022 mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango wakati wa mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania iliyofanyika Kinondoni Jijini Dar es Salam.
Amesema wakati serikali inaongeza udahili wa wanafunzi haitakuwa tayari kuona ubora unapungua hivyo serikali inaendelea na mkakati wake wa kuhakikisha ubora wa elimu hususani katika vyuo vikuu unaimarika.
"Zamani ilikuwa rahisi kuwa Profesa ukiandika tu kwenye magazeti unakuwa Profesa lakini kwa sasa vigezo vya kuwa Profesa vimezidi kuwa vigumu kwa sababu tunataka maprofesa wetu wawe sawa na wale wa nchi zingine," amekaririwa Prof Mkenda.
Amesema katika mageuzi ya elimu yanayokuja ambapo wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipo katika mapitio ya sera na mitaala miongoni mwa mambo yatakayofanyiwa kazi itakuwa ni pamoja na kuhakikisha wanaoajiriwa ni wanafunzi wenye sifa zinazotakiwa.
Pia, Waziri Mkenda amesema kuwa serikali kwa sasa inaendelea na Ujenzi wa Kampasi mpya za Vyuo Vikuu katika mikoa 14 Tanzania pamoja na upande wa Zanzibar (Unguja na Pemba) katika maeneo ambayo hayana vyuo vikuu ukiacha vyuo huria.
Mikoa hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na kampasi za vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini ni pamoja na Tabora, Katavi, Kigoma, Kagera, Singida, Manyara, Lindi, Rukwa, Mwanza, Simiyu, Tanga, Ruvuma, Shinyanga na Dodoma.