Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Kukariri hata njia za kufanya hisabati hukaririwa. Hiyo ni kawaida kwa mambo ya kusoma. Na hajasema kila mwenye GPA kubwa ameipata kwa kukariri lakini wapo pia waliopata GPA kubwa kwa kukariri.

Kuna mtu anafaulu sana HIsabati lakini ukimuuliza mantiki za hizo Hisabati hawezi kukwambia. Kwa ivo kukariri ni jambo la kawaida sana na kiusomaji, kabla ya mtu kuelewa huanza kwanza kwa kukariri.
we hujaenda shule, km umeenda shule basi umejichanganya na utapata shida sana kwa hayo mawazo yako. Pengine urudi shule utofautishe kati ya kukumbuka na kukariri. Katika Reading skills kuna kitu kinaitwa SQ3R - Survey, Question, Thorough Reading, Recall and Review. Ku-recall siyo kukariri ni kukumbuka ulichofundishwa siyo kila kitu ni kukariri. Wed shule imekupita pembeni. Binafsi A-level masomo mawili nilifundishwa na walimu wamarekani, moja hakuwa kungia na hata kiratasi kila kitu alikuwa anaflow kichwani tena somo la Sayansi, je huku ni kukariri au we ungeitaje. University walimu kama watatu nao hawajawahi kuingia na kipisi cha karatasi na wote foreigners, je nao tuwaiteje kwa utaratibu wako walikuwa wamekariri au? Ndugu yangu usiwe na mawazo hais kama hayo. Huwezi kupata GPA kubwa kwa kukariri, GPA ni majumuisho ya masomo yote kwa miaka yote uatafutiwe wastani. Tuwe positive tupongeze wenzetu wenye uwezo mkubwa kutuzidi. Acha kung'ang'ania ubishi eti watu wanakariri wanakariri utakuwa huna tofauti na watu wa mitaani ambao wao uelewa wao unaeleweka.
 
Kipindi cha nyuma nimebahatika kuchaguliwa kuwa kwenye kamati za ajira za baadhi ya taasisi hapa Tanganyika, hichi unachokisema labda nje ya nchi ila hapa nchini? Aisee hapana. Ukiajiri pima IQ achana na makaratasi ya GPA.
Uko sahihi.
 
Interview si zote za kuchuja wanaotakiwa kufanya kazi vyuo vikuu tu ndugu. Upo?
Hoja inapotoshwa. Mkenda kazungumzia vyuo vikuu. Huku kwingine tumetanua tu wigo ili tuweze kuelewana. sasa watu wanataka kufanya ndiko mjadala uliko.

Jee wahadhiri wengi wa Vyuo vikuu wanazo sifa za kuwa waadhiri zaidi ya GPA zao zilizowafanya wawe wahadhiri? Nadhani huu ndiyo mjadala aliotaka Profesa Mkenda ujadiliwe.
 
Huo ni mfumo uliotengenezwa, lkn GPA kubwa itabakia kuwa na uwezo. Yaani mtu ana GPA kubwa ya mathematics alafu azidiwe kwenye namba na mwenye GPA ndogo. 😀😀😀😀😀. Hizi ni chai.
Yaani mtu ana GPA kubwa ya coding alafu azidiwe coding na mtu mwenye GPA ya 3. 😀😀😀😀😀😀.
Nina GPA ya 3 lkn katika hilo siwezi amini.
Kwenye coding na Math umekosea, labda hujawahi kukaa na hawa watu..
 
Acha kung'ang'ania ubishi eti watu wanakariri wanakariri utakuwa huna tofauti na watu wa mitaani ambao wao uelewa wao unaeleweka.
Kwanza kabla ya kuwepo aina hizi za shule watu walikuwa wanapimwaje uwezo wa uelewa wao. Leo hii Plato, Socrates, au Aristotle, ungewapa GPA ngapi? Na hao wanatambulika ulimwenguni pote kama manguli wa falsafa.

Kufaulu mitihani na kuwa na uwezo wa kielimu ni mambo mawili tofauti ingawa yanaweza kufuatana. Umejinasibu kwamba wewe ni msomi, basi jibu kisomi ili sisi tusio wasomi tuone kwamba kweli tunajadiliana na msomi.
 
Kuna mtu anafaulu sana HIsabati lakini ukimuuliza mantiki za hizo Hisabati hawezi kukwambia. Kwa ivo kukariri ni jambo la kawaida sana na kiusomaji, kabla ya mtu kuelewa huanza kwanza kwa kukariri.
Nadhani issue inaanzia kwa yule aliyemfundisha hesabu hizo. Je. Alimfafanulia mantiki ya hesabu hizo kwa lugha nyepesi?

Hapa nakumbuka hesabu za fizikia!! Nasoma mwenyewe mfano wa kwenye kitabu sielewi. Kumbe nilikosa mantiki ya hesabu zenyewe kwa lugha nyepesi.

Ha hahahaha AAA!

Prof Mkenda ana hoja lakini hii hoja isijekuwa imebeba na visivyotakiwa kama kufuta somo la kemia kipindi Fulani kwa shule za sekondari.
 
Bado hatujamuelewa!! patawekwa maximum GPA kama 3.8 na kuendelea hata wa 4.3 anaweza kushiriki katika usahili hii Inakuwa kama shortlings ya kwanza then inafuata interview ambayo hata mweny GPA ya 3.8 anaweza kumpita wa 4.3 kama ataonyesha uwezo sio kuwaajiri direct wale weny kubwa.

Maana vyuo vingi wale weny GPA kubwa wanabaki hawana interview wala nn.. wanakuwa wahadhili moja kwa moja.
 
Kwanza kabla ya kuwepo aina hizi za shule watu walikuwa wanapimwaje uwezo wa uelewa wao. Leo hii Plato, Socrates, au Aristotle, ungewapa GPA ngapi? Na hao wanatambulika ulimwenguni pote kama manguli wa falsafa.

Kufaulu mitihani na kuwa na uwezo wa kielimu ni mambo mawili tofauti ingawa yanaweza kufuatana. Umejinasibu kwamba wewe ni msomi, basi jibu kisomi ili sisi tusio wasomi tuone kwamba kweli tunajadiliana na msomi.
sipendi aina ya mjadala wako, we inaonekana ni mbishi na upaenda personal atacks, we endelea na utaratibu wako uliouzoea. Mi naamini kuna watu wana uwezo mzuri sana kitaaluma na nawahusudu, siyo kuwakebehi eti wamekariri tu. Hapana!
 
We ni km mtu aliyekata tamaa au una wivu wa kipuuzi. Kila kitu kukariri, kukariri maana yake nini. We usome PCM, mahesabu yote yale ya physics na Math ni kukariri? Kuakariri maana yake nini. Acha kupotosha watu.
Unapotoshwa na mtu mwenye wivu na aliyekata tamaa?
You re too feeble to understand my intimation. Fanya mambo mengine.
 
sipendi aina ya mjadala wako, we inaonekana ni mbishi na upaenda personal atacks, we endelea na utaratibu wako uliouzoea. Mi naamini kuna watu wana uwezo mzuri sana kitaaluma na nawahusudu, siyo kuwakebehi eti wamekariri tu. Hapana!
Nisamehe kama kuna mahali unaona nimefanya "Personal attack". Hii ni "Public Domain" hulazimishiwi kujadiliana na mtu, hiyari ni yako.

Hakuna mahali nimesema wote wenye GPA kubwa wanatokana na kukariri lakini kukariri pia kunaweza kumsaidia mtu kupata GPA kubwa. Na kuna watu wanao ushahidi pia kuwa kuna watu wengine GPA zao kubwa "waligawiwa" na wahadhiri.

Mmojawapo wa mtu aliyepambana na GPA za "Kugawiwa" ni dada Vicensia Shule.
 
Kuanzia sasa Serikali itaanza kuzitazama ajira za vyuo vikuu badala ya kuangalia ubora wa ufaulu yaani GPA pekee sasa waajiriwe kwa kupimwa uwezo wao kwa kufanya usaili.

Kuangalia ufaulu pekee wa wanafunzi haitoshi kuboresha elimu badala yake ni muhimu kuongeza vigezo hivyo katika mapitio ya sera na mabadili ya mitaala jambo hilo litatazamwa kwa weledi mkubwa.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba 2022 mbele ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango wakati wa mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania iliyofanyika Kinondoni Jijini Dar es Salam.

Amesema wakati serikali inaongeza udahili wa wanafunzi haitakuwa tayari kuona ubora unapungua hivyo serikali inaendelea na mkakati wake wa kuhakikisha ubora wa elimu hususani katika vyuo vikuu unaimarika.

"Zamani ilikuwa rahisi kuwa Profesa ukiandika tu kwenye magazeti unakuwa Profesa lakini kwa sasa vigezo vya kuwa Profesa vimezidi kuwa vigumu kwa sababu tunataka maprofesa wetu wawe sawa na wale wa nchi zingine," amekaririwa Prof Mkenda.

Amesema katika mageuzi ya elimu yanayokuja ambapo wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ipo katika mapitio ya sera na mitaala miongoni mwa mambo yatakayofanyiwa kazi itakuwa ni pamoja na kuhakikisha wanaoajiriwa ni wanafunzi wenye sifa zinazotakiwa.

Pia, Waziri Mkenda amesema kuwa serikali kwa sasa inaendelea na Ujenzi wa Kampasi mpya za Vyuo Vikuu katika mikoa 14 Tanzania pamoja na upande wa Zanzibar (Unguja na Pemba) katika maeneo ambayo hayana vyuo vikuu ukiacha vyuo huria.

Mikoa hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na kampasi za vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini ni pamoja na Tabora, Katavi, Kigoma, Kagera, Singida, Manyara, Lindi, Rukwa, Mwanza, Simiyu, Tanga, Ruvuma, Shinyanga na Dodoma.
Waziri Prof Mkenda kaonesha jinsi ambavyo haujui wizara yake vizuri. Hakuna chuo kinaachoajiri bila interview toka zamani. Yaani wanafanya mpaka written exam, presentation na oral interview. Hicho alichokiongea na cha nchi gani????????????? Yaani hakika ameonesha uelewa mdogo sana. Halafu waziri unaanza kukandia GPA kama vile na ya kwake ni magumashi. Hizo habari za mtaani yeye kama waziri hakupaswa kuziongea ni mtu mwenye uelewa mdogo pekee ndiye anayeweza kubeza mambo ya GPA. Ni muhimu sana kuwa na semina elekezi ya viongozi kama enzi za JK
 
University walimu kama watatu nao hawajawahi kuingia na kipisi cha karatasi na wote foreigners, je nao tuwaiteje kwa utaratibu wako walikuwa wamekariri au?
Mkuu niliwahi kupata kisanga kutoka kwa mwanafunzi aliyebahatika kusoma digrii ya kwanza hapa nchini. Sasa yeye alikuwa anasoma materials ya Mwalimu na Kwenda library kutafuta vitabu vinavyohusu somo husika. Mtihani ukija anaambulia makisi za katikati lakini wenzake wengi ambao wanakula bata wanapata maksi zaidi Tena wengine mia kwa mia. Akawa anajiona kilaza balaa, maana nguvu kubwa alikuwa anaitumia kusoma!!!

Sasa yupo mwaka wa pili akiwa library akasikia walimu aliokuwa anawafahamu lakini hawamfundishi wakinong'ona kuwa limetoka tangazo kuwa walimu wote lazima watunge Mitihani mipya. Hakuna kurudia maswali yaliyopita. Akagutuka!! Kumbe wenzangu walikuwa wanasoma Mitihani iliyopita?

Toka semester hiyo walipoletewa Mitihani mipya na kuendelea mwanafunzi huyo ndiye alikuwa anaongoza kwa jpie darasani kwake.
===
Kikubwa unatakiwa kukariri na kuelewa kile ulichokikariri. Ukikariri tu bila kuelewa ukibadilishiwa maswali unaangukia pia. Kwa kazini utashindwa kutatua changamoto ikitokea Hali ambayo hukuwahi kukumbana nayo hapo kabla.

Nasisitiza kuelewa unachokariri ni Muhimu.

Mchana mwema.
 
Waziri Prof Mkenda kaonesha jinsi ambavyo haujui wizara yake vizuri. Hakuna chuo kinaachoajiri bila interview toka zamani. Yaani wanafanya mpaka written exam, presentation na oral interview. Hicho alichokiongea na cha nchi gani????????????? Yaani hakika ameonesha uelewa mdogo sana. Halafu waziri unaanza kukandia GPA kama vile na ya kwake ni magumashi. Hizo habari za mtaani yeye kama waziri hakupaswa kuziongea ni mtu mwenye uelewa mdogo pekee ndiye anayeweza kubeza mambo ya GPA. Ni muhimu sana kuwa na semina elekezi ya viongozi kama enzi za JK
Vyeti feki vinazalishwa huko machuoni. Mbinu za ufaulu zimekuwa nyingi, kucopy, kulipwa ufanyiwe mitihani, rushwa ya ngono, Walimu wasio na uwezo wala mbinu za kurithisha elimu na ufahamu n.k n.k

Matokeo tunayaona kwenye utendaji katika uhalisia. Graduates wana GPA zisizofanana na utendaji wao. Tusipobishana katika hili tukarekebisha tatizo hakuna atakayenufaika.
 
Hoja inapotoshwa. Mkenda kazungumzia vyuo vikuu. Huku kwingine tumetanua tu wigo ili tuweze kuelewana. sasa watu wanataka kufanya ndiko mjadala uliko.

Jee wahadhiri wengi wa Vyuo vikuu wanazo sifa za kuwa waadhiri zaidi ya GPA zao zilizowafanya wawe wahadhiri? Nadhani huu ndiyo mjadala aliotaka Profesa Mkenda ujadiliwe.
Prof Mkenda kwa ufupi kaonesha uelewa mdogo wa mambo ya elimu ya juu. Iko hivi duniani kote mtu anayechukuliwa kufanya kazi chuoni lazima awe na uwezo mkubwa. Inawezekana kabisa hana uwezo wa kujieleza ila ana speciality fulani. Hicho alichokisema mi nakiita yaani Prof Mbeya maana hakuna evidence ya hayo madai yake kwa sababu vyuo vyote ni lazima ufanye interview. Labda yeye alikuwa ana refer enzi anaajiliwa yeye labda hakufanya interview. Cha ajabu waziri mzima unaanza kukandia GPA ambayo hata yeye ilimuweka hapo alipo???? Yaani ni colonial mentality. Haya tuseme basi hata ma prof wa tanzania hawana uwezo??? Kwa sababu na yeye ni prof aliye tokana na GPA mbovu?????
 
Wanaoponda wote gpa humu ni wajinga na vilaza wenye gpa za 2.0 ,wengine hata chuo hawajafika ....

Na wanosema lecture vyuoni wamekalili ni wivu wa kijinga na hawana tofauti na mazuzu ...

Mtu mwenye gpa ya 4.7 huyu anauwezo mkubwa Sana ,mheshimu taaluma za watu ....

Kuna wapumbavu humu wamejikita kwenye kukariri ,wameshindwa kuelewa kuwa kuwa na uwezo wa kumbuka vitu ulivyofundishwa ni akili kubwa Sana [emoji3],humu ndani kumejaa watu wenye wivu ,husuda ,ujuaji na uchawi mwingi ....

Wanataka watu wenye taaluma zao waliosoma na kufika vyuo vikuu ,degree ,masterz Hadi PhD wawe kama wao ,kiufupi ni kuwa Hao wako mbali na hamuwezi kuwafikia ....

Huku mtaani kunaonekana Kama umesoma umesoma tu huwezi linganishwa na darasa la saba ,hata kama huyo la Saba anapesa kiasi gani [emoji3][emoji3]....elimu ,...elimu ...elimu ...

Humu ndani wamejikusanya wajinga waliofeli shule wamejazana kwenye uzii kujipa Moyo et gpa za kukariri .....ndio ..... kama mwenye maisha huwezi kukariri wewe ni zezeta ,huwezi kumbuka kitu ulichoambiwe huna tofauti na zuzu ....
 
Vyeti feki vinazalishwa huko machuoni. Mbinu za ufaulu zimekuwa nyingi, kucopy, kulipwa ufanyiwe mitihani, rushwa ya ngono, Walimu wasio na uwezo wala mbinu za kurithisha elimu na ufahamu n.k n.k

Matokeo tunayaona kwenye utendaji katika uhalisia. Graduates wana GPA zisizofanana na utendaji wao. Tusipobishana katika hili tukarekebisha tatizo hakuna atakayenufaika.
Nakukatalia pamoja kuwa mi sijui sana mambo ya chuo maana nilipita tu huko nikachukua ki degree changu. Huu ujinga ndiyo mmekaririshwa kila kitu kikiharibika mnasingizia serikali. Chuoni kila mtu anapaswa kupambana, wala siyo rushwa ni uongo.
 
Back
Top Bottom