Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Chuo kwa Tanzania ni elimu rahisi sana
Ukisoma Past paper tu umetoboa bila kuwa na haja ya kusoma mambo mengine yote, wanafunzi 90% hawajui sababu zao wao kusoma modules fulani zaidi ya kufaulu

80% ya watu wanaomaliza chuo huanza upya kutafuta kitu cha kufanya kwenye maisha, ukikutana na Mwalimu wa chuo ambaye hajawahi kufanya kazi kwenye kile alichosomea, ni weupe and very narrow minded
 
Tsh ametoa hoja yenye mantiki sana. inatakiwa idatishwe kule juu ya bandiko!!
Shukran sana mkuu kwa kuisapoti hoja. Tuna tatizo kubwa sana boss, mara ya mwisho nimepokea binti wa chuo hajui hata cheque ni kitu gani, hajui kujaza slip ya cheque, anatetemeka, ni kitu kipya kwake, hajawahi kukiona, ni jambo linalomtisha ila somo la Finance amefaulu na huenda katika mitiani yake ameshajibu swali la what is cheque, types of cheques kwa ufasaha.
 
Shukran sana mkuu kwa kuisapoti hoja.
Nahisi wengi hawajaelewa kilichoongelewa. Mkenda katoa maagizo baada ya matukio yanayoonesha kuna watu wana shahada za vyuo vikuu zisizoakisi uwezo wao wa kazi kuongezeka. Sasa si bora umsaili kabla ya kumuajiri? Tatizo liko wapi??

Inawezekanaje mtu kamaliza chuo kikuu lakini hawezi kuandika barua yenye mantiki ya kuomba kazi? Au inakuwaje mtu aliyesoma masomo yake kwa kiingereza kwa miaka zaidi ya saba awe hawezi kuongea ama kuandika kiingereza kwa ufasaha? Mtu kama huyu ili ujue uwezo wake njia rahisi si kumsaili?
 

inategemea na wasaili uelewa wao na aina ya kazi inayoombwa... Kwenye usaili tunapima uelewa, atitude, commitment, behaviour nk..
kwenye uelewa itategemea aina ya kazi na uzoefu unaotakiwa... kama ni uzoefu wa zaidi ya 2yrs kwenye field fulani hapa unaweza kushangazwa na hata mwenye GPA ya 2.0....
 
Bado huelewi mambo mengi. Watafute wenye GPA kubwa zaidi unaowafahamu, halafu angalia mafanikio yao ukilinganisha na wenye GPA za kawaida, halafu utatuambia.
 
Boss upo sahihi 100% kwenye hii comment uliyonijibu nimeedit na kuongeza mfano halisi kabisa. Halafu ni kama hawajui kuwa sekta binafsi ambayo inaajiri sana hawapendi kuajiri, wakulipe ili wakufundishe kazi wanataka wakulipe ili uzalishe na waone matokeo ndo maana hawajali vyeti siku hizi.
 
Watu waelewe kuwa ukubwa wa GPA hauhusiani hata kidogo na uwezo wa mtu kufanya kazi tarajiwa. Hayo uliyoyataja ya uzowefu, tabia, hari ya kufanya hiyo kazi, mwenendo wa muombaji, utayari wa kuifanya hiyo kazi kwa mazingira tarajiwa, ndiyo huzingatiwa kwenye kuajiri mtu na siyo GPA yake.

Kuna usaili unafanyika wanaachwa wenye shahada wanachukuliwa watu wa kidato cha sita.
 
Malecturer wengi Tanzania ni Academician na sio watu wenye skills na exposure matokeo wanapump matheory.

Ni wakati wa Vyuo kujikita kwenye kuajili watu waliokaa kitaa kidogo na kupata life exosure + skills, mtu amemaliza say Electrical au Civil engineering then hajawahi kabisa kupractise alichosomea kwasababu ana GPA ya 4 unambakiza na kumfanya lecturer matokeo yake ni hasara kubwa kwa wanafunzi... Angalau muanze kuajili malecturer wenye experience ya kazi walizosomea nje uhadhiri.
 
Bado huelewi mambo mengi. Watafute wenye GPA kubwa zaidi unaowafahamu, halafu angalia mafanikio yao ukilinganisha na wenye GPA za kawaida, halafu utatuambia.
Acha uhuni tunazungumzia elimu. Mwenye GPA ndogo hana uwezo kielimu.
 
Kwanza isichukuliwe kwamba tunasema wachukuliwe wasio na sifa, hata Profesa Mkenda hakusema hivyo. Kinachosema ni kwamba zinawekwa sifa, wenye hizo sifa wanaomba kazi halafu wanasahiliwa ili kati yao wachukuliwe wale watakaothibitisha kwamba uwezo wao wa darasani haukuwa wa kukaririr bali ulitokana na wao kuelewa walichokuwa wanafundishwa.
 
Huo ni mfumo uliotengenezwa, lkn GPA kubwa itabakia kuwa na uwezo. Yaani mtu ana GPA kubwa ya mathematics alafu azidiwe kwenye namba na mwenye GPA ndogo. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€. Hizi ni chai.
Yaani mtu ana GPA kubwa ya coding alafu azidiwe coding na mtu mwenye GPA ya 3. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.
Nina GPA ya 3 lkn katika hilo siwezi amini.
 
Elimu ni nn? Maana hapa ndo tatizo linapoanza.

Mfano: Kujua Kusonga ugali ukaiva hiyo ni elimu.

Sasa mwenye A+ ya kusonga ugali kwenye makaratasi na anayesonga ugali kwa exposure na uzoefu nani ana elimu yenye uzalishaji halisi?
Hili swali lako haliendani na uhalisia. Shida ni kwamba huko makazini mnafanya kazi za kukusanya mafaili na kuweka kabatini. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Acha uhuni tunazungumzia elimu. Mwenye GPA ndogo hana uwezo kielimu.
Hii umekosea. Hebu nikupe mfano kwa kuuliza swali.

Mtoto aliyekariri akijibu swali la 2X2=4

Mtoto aliyeelewa akijibu swali la 2X2=4

Mtoto aliyechungulia kwa mwenzake 2X2=4

Mtoto aliyeuziwa mtihani naye akijibu 2X2=4

Hao wote si watakuwa wamefaulu, lakini je uwezo wao ni sawa? Ukiwasaili hautaona utofauti wao? GPA kubwa siyo kiashiria cha kweli kuoenesha ubora wa elimu aliyo nayo mtu.

Nikuibie siri. Vyuo vikuu vya Tanzania vinazingatia zaidi matokeo ya mwanafunzi kwenye mtihani wake wa Kidato cha nne.
 
Kipindi cha nyuma nimebahatika kuchaguliwa kuwa kwenye kamati za ajira za baadhi ya taasisi hapa Tanganyika, hichi unachokisema labda nje ya nchi ila hapa nchini? Aisee hapana. Ukiajiri pima IQ achana na makaratasi ya GPA.
 
Hili swali lako haliendani na uhalisia. Shida ni kwamba huko makazini mnafanya kazi za kukusanya mafaili na kuweka kabatini. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Sawa, wewe umesema na kuhitimisha. Basi ibaki kuwa hivi ulivyowaza.
 
A little too late...hii ya kulazimisha GPA kubwa wabaki vyuoni imetengeneza matatizo makubwa kuliko hata faida.
Tuna wasomi vilazi wametapakaa kila kona. Tunawaona wanavyoendesha mambo yao. Kama vile watu wasiosoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…