Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Ukitaka upate walimu wazuri vyuo vikuu, wenye GPA za juu wawe wanafanyiwa usaili wa kufundisha darasani kwa vitendo na si uasili wa mahojiano pekee. Ni vizuri kwamba GPA za juuu ziendelee kuwa ni kigezo kimojawapo, ila SECOND iwe usaili kwa njia ya vitendo, kufundisha darasani
 
Pamoja na kuwa ni muda; ILA nilisoma shule ya Sekondari ya serikali kubwa na yenye jina ila niliweza kukaa darasani mwaka mzima bila kuwa na mwalimu wa Hesabu; Namani changamoto ya upungufu wa waalimu wa Saiyansi ichukuliwe kwa uzito stahili. Mwanafunzi akifaulu hesabu ni rahisi sana kupata ufaulu wa hayo masomo mengine na kupata GPA nzuri...
Tatizo la wanafunzi kufeli masomo ya saiyansi naweza kusema 85% ni kukosa waalimu wa Saiyansi. (Maths, Phy, Chem & Biol). Tusitafute mchawi.... Akiwepo Mwalimu Mahiri hata kwa vifaa vichache wanafaulu
 
We ni km mtu aliyekata tamaa au una wivu wa kipuuzi. Kila kitu kukariri, kukariri maana yake nini. We usome PCM, mahesabu yote yale ya physics na Math ni kukariri? Kuakariri maana yake nini. Acha kupotosha watu.
 
Kipindi cha nyuma nimebahatika kuchaguliwa kuwa kwenye kamati za ajira za baadhi ya taasisi hapa Tanganyika, hichi unachokisema labda nje ya nchi ila hapa nchini? Aisee hapana. Ukiajiri pima IQ achana na makaratasi ya GPA.
Tumejaza vilaza kila sehemu. Wanakariri mambo halafu wanataka wao ndio watuongoze.Kwenda wapi?
 
Tuwekeze kwenye practical zaidi
Walimu Wawili Msaidizi wa walimu Mmoja darasa 350 wanafunzi ama zaidi, semester wiki 15, somo limepewa masaa manne na nusu kwa wiki. Vifaa vya practical vinafika sehemu husika kutoka kwa supplier wiki nne kabla semester Kwisha.... Mambo ni mengi muda mchache! Sijui nilikuwa naandika kitu gani ebu Meneja wa Makampuni fafanua mada ya bandiko lako.
 
We ni km mtu aliyekata tamaa au una wivu wa kipuuzi. Kila kitu kukariri, kukariri maana yake nini. We usome PCM, mahesabu yote yale ya physics na Math ni kukariri? Kuakariri maana yake nini. Acha kupotosha watu.
Kukariri hata njia za kufanya hisabati hukaririwa. Hiyo ni kawaida kwa mambo ya kusoma. Na hajasema kila mwenye GPA kubwa ameipata kwa kukariri lakini wapo pia waliopata GPA kubwa kwa kukariri.

Kuna mtu anafaulu sana HIsabati lakini ukimuuliza mantiki za hizo Hisabati hawezi kukwambia. Kwa ivo kukariri ni jambo la kawaida sana kiusomaji, kabla ya mtu kuelewa huanza kwanza kwa kukariri.
 
... huo usaili one of the criteria lazima gpa at least 3.8 then mengine yanafuata.
Kasheshe inakuja pale Kuna Mwanafunzi ana jpei ya 4.3 kutoka Chuo Fulani na mwingine ana jpei 3.4 kutoka Chuo kingine na wote wamesoma programme hiyo hiyo ya uhandisi, Sayansi ama Sanaa lakini wakiwekwa kwenye mizania ya uelewa na kufanya kazi yule wa jpiei ya 3.4 unatamani huyu ndiye apewe kazi na inatakiwa jpei yake isome 4.6 kwenye transcript.


Sijui naeleweka!!!!?
 
Tuseme tu ukweli wenye GPA ndogo ni vilaza boss.
I used to believe that...Ila kwenye haya maisha, tena baada ya kusoma degree moja, nimegundua kuwa wengi wa vipanga ndio vilaza wakutupwa.
Naamini mfumo wetu wa elimu uliwabeba waliokuwa na uwezo mkubwa wa kukariri, kuliko kufikiri. Tena pale chuoni, wale walioweza kuyaweka sawa madesa, waling'ara.
Haina maana wote wenye GPA walikuwa na matatizo, ila walio mengi. Ni vilaza kuliko tunavyofikiri.
 
Sijui naeleweka!!!!?
Unaeleweka.

Kenya mwezi jana kuna shirika lilitangaza kazi na sifa ikawa ni shahada ya uzamili (Masters' Degree) lakini kuna dada akaomba kwa kutumia Diploma na vyeti vingine ambatano. Baada ya mabishano ya muda kidogo, wasaili wakaamua kumweka kwenye orodha (shotlisted) ya watakaosailiwa.

Baada ya usaili huyo binti akawa wa pili kwa ubora kati ya waliosailiwa.. akapewa kazi.

Sijui nimeeleweka!!??
 
Tumejaza vilaza kila sehemu. Wanakariri mambo halafu wanataka wao ndio watuongoze.Kwenda wapi?
Kuwa na uwezo mkubwa wa kukariri na ku reproduce madesa, sio kuwa na IQ kubwa. Wale walio na uwezo wa kufikiri na kuona mambo ndio wanapaswa kukaa sehemu zote nyeti. Hata kama waqna GPA ndogo.
Albert Einsten alikuwa reject wa elimu yetu hii ya kukariri sababu he was a thinker.
 
Naam Sasa unaeleweka barabara.
===
Kuna kitu kinakosewa mahali fulani. Na hapo mahali Kuna baadhi hawataki kupagusa.
 
.... mchujo wa awali kabisa ni hiyo gpa; below 3.8 automatically havuki kwenda next stage. So, hakuna uwezekano wa 3.4 kukutana na wa 4.3 kwenye interview (face to face).
 
Zamani Kuandika kwenye gazeti unakuwa profesa? Aliyeelewa tafadhali
Sijaelewa pia, nilitarajia iwe majarida ya kitaaluma. Je, yeye sio Professa kupitia kuandika magazetini au yeye sio wa zamani? Hiyo zamani ni kuanzia mwaka gani?
 
.... mchujo wa awali kabisa ni hiyo gpa; below 3.8 automatically havuki kwenda next stage. So, hakuna uwezekano wa 3.4 kukutana na wa 4.3 kwenye interview (face to face).
Interview si zote za kuchuja wanaotakiwa kufanya kazi vyuo vikuu tu ndugu. Upo?
 
.... mchujo wa awali kabisa ni hiyo gpa; below 3.8 automatically havuki kwenda next stage. So, hakuna uwezekano wa 3.4 kukutana na wa 4.3 kwenye interview (face to face).
Wale watu wanaofanya chaguzi (Shotlistings)za watu watakaosailiwa huwa hawafuati njia hiyo moja kwa moja.. Kwa uzowefu wao wanajua kwamba pamoja na kuweka vigezo fulani mahsusi, huwa wanatokea watu wengine wasio na vigezo hivyo kinadharia lakini kivitendo wakawa navyo.

Hivyo kabla ya usaili kila barua ya maombi hupitiwa na kufanyiwa Tathimini kama inaweza kupewa fursa ya kujadiliwa na wanajopo kama na mwenye hiyo barua naye anaweza kuitwa kwenye usaili.

Mfumo huu hutumika zaidi kwenye mashirika ya UN.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…