Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Wenye GPA kubwa ndio muhimu tena wanatakiwa kuendelezwa kwa kutumia internship.
 
Reactions: Tsh
Vitendo unajifunza boss. Waziri aanzishe internship kwa watu wenye GPA kubwa ili waendelezwe wasaidie taifa letu.
 
Vitendo unajifunza boss. Waziri aanzishe internship kwa watu wenye GPA kubwa ili waendelezwe wasaidie taifa letu.
Hii sasa ni hoja lakini haihusiani na ile ya usaili kindakindaki. Nchi yetu mfumo wa kuwalea wasomi wetu ni mbovu. Mazoezi kwa vitendo (internship) ndiyo humkomaza msomi. wanaofanya ni madaktari tu.
 
Wanataka kutupeleka sehemu fulani mbaya! Mwalimu hapaswi kuwa ni mtu ambaye hakufaulu kwa kiwango cha juu kabisa cha vitu alivovisoma.

Tukumbuke mwalimu wa shule aliyepata divisheni 4, ana ufahamu wa kiwango gani?? Je hivo ndivo mataifa mengine hufanya? Au ni jambo letu sisi ambalo litapelekea hata waalimu wetu kutokubalika kufundisha katika vyuo vya nje???
 
Unajiliwaza tu mkuu. Kigezo ndio hicho. Minimum GPA ni 3.8. Hapo ndio unqualify walau kuwa shortlisted kwa ajili ya interview. Na hizo ni guidelines za TCU. Hata kama unahisi una uwezo wa kufundisha, maadam hujakidhi hicho kigezo kimojawapo, sahau kuitwa kwny interview. Halafu tuache excuses za kufeli kwetu kwa kubeza waliofaulu kutuzidi. Mnatumia kigezo gani kuwa mwenye GPA kubwa kafake na mwenye GPA ndogo ni genuine? Nani aliyeingiza hii mentality kwa jamii?
 
Umemjibu vizuri sana. Ila hapo mwisho naomba nitakuchallange kidogo.

Tuna hili tatizo la kuhadaa wanafunzi kuwa ukifaulu umefanikiwa na ukifeli ww ni KILAZA, Vijana wanalenga kupata GPA nzuri mavyuoni bila kujali iwapo hiyo GPA kweli ipo kichwani na itamsaidia kutengeneza kipato wakati VILAZA wanatoka nje na kuipata elimu halisi ya hii dunia na matokeo yake tuna VILAZA wafanyabiashara, VILAZA mafundi, VILAZA wanasiasa wanaotoa ajira na wenye vipato wengi kuliko graduates wenye GPA KUBWA walio na kazi zenye msaada kwa jamii na kuwapatia vipato.

Sasa hivi kuna VILAZA BODABODA wanakipato cha uhakika kuliko wenye degree na tayari wapo wenye degree na GPA zao wanavizia kazi wanazoamini ni za VILAZA kama ya boda boda. Hichi ndicho kilichopo kwenye jamii.

Naamini tukijikita kwenye utendaji kuliko ufaulu wa makaratasi tu tutasaidia wengi.
 
Weww jamaa una wivu na ujuaji mwingi Sana ,mbaya zaidi mmejaaa ofcin huko mnajiona Sana mnajua kuliko mtu yeyote ......

Tanzania imejaa watu wa namna hii ,si ajabu ndio maana nchi ni ngumu Sana uchawi na rushwa vimekua Kwa Kasi kubwa sababu ya watu wa aina hii [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Mkuu uwezo wa mtu wa kuhoji ,kujieleza na kuwa mbunifua utaujuje ? Kwenye interview ya masaa 3 au ?

Mtu unakutana nae amekuwa mtu mzima ,miaka 30+ utajuaje uwezo wake haraka haraka kama sio kujua background yake (elimu toka primary, secondary,Hadi chuo )....

Ukiona hajapita kote huko ,huyo hana lolote na hana analolijua niamin Mimi ...


Na usipoteze muda kumwamin ,maana atakusumbua tu Bure ,hata kazi za kuelekezwa hata weza achana na swala la kuwa mbunifu...

Hao wote uliotaja hapo juu shule wameenda mzee[emoji2]
 
Haupo sahihi. Badili huu mtazamo.

Kama kila atakayekosoa ataitwa mchawi kisha kila mmoja akanyamaza sijui tutakuwa na jamii ya aina gani?

Uzuri Hapa tupo na fake ID, mtu unakuwa huru kusema lile unaloliona ni sawa bila kuwa na hofu ya kukosolewa utendaji wako katika jamii sababu hujulikani. HUU NDO UZURI WA MAX NA JF YAKE..
 
Wenye GPA kubwa ndio muhimu tena wanatakiwa kuendelezwa kwa kutumia internship.
Mkuu Siku zote GPA ndo Hatua ya kwanza, waliofaulu ndo wanatazamwa kwanza na kutegemewa zaidi na ndio wanaopata nafasi kwanza,hata kipindi chetu ndivyo ilivyokuwa. Tatizo ya miaka hii kuanzia 2010 wenye GPA wanapoitwa ni kama wanawaambia watu mnachotegemea hamtakutana nacho, haya makaratasi yetu yasiwadanganye, jaribuni na wengine.
 
Umeongea kifalsafa sana. Sijui ni kwa nini wasomi wetu hii mantiki rahisi hawaielewi. GPA sawa, lakini kwenye usaili wenye hizo GPA wanashindwa kuthibitisha kwamba wanazo hizo GPA.

Huwezi kufanya usaili kwa watu wasio na sifa ya kusailiwa. Sasa wanaposhindwa kuthibitisha huo U- GPA wao, ndipo Waziri anapoona lazima marekebisho yafanyike kwenye hizo saili zao. Lakini linazuka jambo la kuonekana wenye GPA kubwa hawatakiwi kuajiriwa.
 
Reactions: Tsh
Kweli mkuu, halafu nadhani tuna tatizo la kuuchukia ukweli. Yaani kama nina GPA kubwa na sina kazi basi akitokea anayesema GPA si kigezo pekee anachukiwa wakati ni suala jepesi tu, hakikisha kilichopo kwenye karatasi zako kipo kichwani basi.
 
akitokea anayesema GPA si kigezo pekee anachukiwa wakati ni suala jepesi tu, hakikisha kilichopo kwenye karatasi zako kipo kichwani basi.
Hili neno sijui watu hawalijui maana yake!!??
 
Reactions: Tsh
Wangewekeza kwenye kuboresha viwango vya elimu inayotolewa katika vyuo vilivyopo. Matokeo ya Law School yanatakiwa kuwaamsha.

Amandla...
 
Hapo kwenye pisi kali nakubaliana Na ww kabisa, hizo pisi ukijenga nao mahusiano Mazur unatoboa kirahis mno
 
Hili neno sijui watu hawalijui maana yake!!??
Hahahaha. Wanalijua ila nadhani wapo ambao wakiwaza chuo alijifunza nn anaishia kukumbuka title ya kozi tu iliyoandikwa kwenye cheti sababu kilichopo kwenye printed results hakipo kichwani sasa huyu lazima aichukie hiyo sentensi GPA SI KIGEZO PEKEE.
 
Usaili wa nini? Mtu hapati ajira mpaka baada ya muda wa matazamio kupita. Muda huo ndio unatakiwa kutumika kuamua kama mtu anastahili hiyo ajira au la.

Amandla...
 
Naunga mkono hoja. Unajua sana.
 
Wangewekeza kwenye kuboresha viwango vya elimu inayotolewa katika vyuo vilivyopo. Matokeo ya Law School yanatakiwa kuwaamsha.

Amandla...
Si lazima kwanza ubadilishe mfumo wa kuwapata watoa elimu ndipo upate matokeo bora!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…