Na Charles Mollel
Kwa mujibu wa Taarifa zilizopo, wakati wananchi wanaruhusiwa kuishi ndani ya Bonde la Ngorongoro idadi yao ilikuwa 8,000 na kila mkaazi alikuwa na idadi ndogo ya mifugo, wengi walikuwa wakimiliki kati ya Ng'ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Moja ya changamoto kubwa iliyosababisha haya ni idadi kubwa ya wahamiaji hasa kutoka nchi jirani ya Kenya. Ukweli huu mchungu ni vema ukafahamika na watu wote.
Ilifika wakati ongezeko la watu na mifugo katika Bonde la Ngorongoro kufikia 40% kwa mwaka. Kwa wakaazi wa Ngorongoro tulijua kwa vyovyote lazima kuna hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na ongezeko hili lisilovumilika.
Kwa kipekee naipongeza serikali kwa kuchukua hatua za kiungwana kufanya mazungumzo na viongozi wa kimila na hatimaye tumepata suluhisho la kudumu na linalojali maslahi ya wananchi.
Kwa wasiojua zifuatazo ni baadhi ya faida tunazopewa kama mchango wa serikali katika suala zima la kukabiliana na changamoto iliyopo mbele yetu;
1.Kupewa Nyumba yenye vyumba vitatu ya tofali na iliyokamilika bure.
2.Kuhakikishiwa huduma zote za kijamii zikiwemo maji, umeme, shule na hospitali katika makazi mapya yenye ukubwa wa mita za mraba 400,000.
3.Kuingizwa rasmi kwenye miradi yote ya maendeleo ya serikali.
4.Kukabidhiwa hati ya viwanja ambavyo vimekwishapimwa ambayo ni fursa kwetu kutumia hati hizo kuweza kupata mikopo mbalimbali ya maendeleo katika taasisi za kifedha.
5.Kuepushwa na muingiliano na wanyama wakali kama Simba, Chui, Nyati na Faru ambao mara kadhaa wameleta kadhia kwetu na hata wanyama wapole kukimbilia nje ya hifadhi.
Kupatikana kwa suluhu hii juu ya muafaka wa bonde la Ngorongoro ni matokeo ya usikivu wa serikali kwa kuwapa kipaumbele viongozi wa kimila kutoa mapendekezo ya nini kifanyike badala ya kutumia nguvu.
Nichukue fursa hii kuwakemea wale wanaoendesha NGO’s mbalimbali kwa kuwatumia wakaazi wa Ngorongoro kuomba fedha kwa wahisani waache tabia hiyo kwani haina manufaa nchi yetu bali kuchafua taswira yetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA [emoji1241]