Waziri Mkuu apokea orodha ya majina 453 ya wananchi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiyari yao

Waziri Mkuu apokea orodha ya majina 453 ya wananchi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiyari yao

Nadhani point hapa ni kuwa Wamasai wamekubali kuhamia Handeni.
Hoja kubwa zaidi ni kuwa huko Handeni ndiko wanapopakimbia kurudi Ngorongoro.
Huko Handeni walipakimbia lini..?
 
Hizo ndio siasa za bongo.
Naomba kuuliza Hakuna wakulima huko? Tusije anzisha tena vita vya wafugaji na wakulima tukawa tumetengeneza tatzo jipya.
Hiyo ni ardhi iliyotengwa kwa ajili ya mifugo
 
Shida Majaliwa kachanganyikiwa kuukosa urais baada ya mwenda kuzimu kuishia
 
Yale yale ya simulizi ya Machaku na njiwa

Wakati Machaku akitaka kumuua njiwa ndipo njiwa akamwaambia Machaku usiniue tumboni kwangu kuna dhahabu kubwa kuzidi ukubwa wa kichwa chako Machaku nae akaamini

Hivi hiki kitabu bado kipo shuleni[emoji23][emoji23]
 
Waziri mkuu wetu mbona mara nyingi anaongea vitu visivyokuwepo jamani? kha? km za mraba 400,000 handeni? kweli hiyo ni nusu ya ukubwa wa nchi hii iinayoshika nafasi ya 13 kwa ukubwa afrika ikiwa na km za mraba 960,000.

Anyway hongereni sana wamasai wa ngorongoro kupewa eneo lenye ukubwa wa nusu ya nchi wakati sisi tunasubiri reports za kuungua soko la karikaoo na mauaji yaliyofanyw ana polisi huko mtwara zote ni tume alizounda waziri mkuu
NARUDIA TENA , HONGERENI SANA WAMASAI MMEULA KWELIKWELI ingawa wilaya nzima ya handeni ina km za mraba 7000 tu
Labda alimaanisha mita za mraba
 
Kumbe bado waziri mkuu ni yuleyule kweli naichukia sisiemuu na serikali yake maana hata sifuatilii taarifa zao za habari, au ndio wanabust hivi ili wajulikane wapo?
 
Kunamambo serekali ikishaamua hakuna njia ya kuyakwepa. Walianza kimasiara kutekenya Sasa taratiiibu watu wanainua makwapa. Yaan kwa kifupi suala la Masai kuondoka kwenye hiyo hifadhi ni lazima ni Jambo la taratibu tu
Na unaweza shangaa serikali ilishaanza ujenzi wa nyumba kwenye eneo ambalo wataenda kuishi hata kabla ya makubaliano kuwa wataondoka au hawaindoki 😂!.

Yaani nimecheka sana, mtu anataka eneo lako hata kabla ya kuja mfanye bargain yeye anakuja na fundi wakiwa na ramani mpya jinsi ya kujenga asee, dunia simama nishuke 🤣!
 
Ngorongoro.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari huku wengine wakiendelea kujiandikisha....
😍
 
df6b8fed-3bc3-4319-9d50-a035cb3b5e32.jpg

Na Charles Mollel

Kwa mujibu wa Taarifa zilizopo, wakati wananchi wanaruhusiwa kuishi ndani ya Bonde la Ngorongoro idadi yao ilikuwa 8,000 na kila mkaazi alikuwa na idadi ndogo ya mifugo, wengi walikuwa wakimiliki kati ya Ng'ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Moja ya changamoto kubwa iliyosababisha haya ni idadi kubwa ya wahamiaji hasa kutoka nchi jirani ya Kenya. Ukweli huu mchungu ni vema ukafahamika na watu wote.

Ilifika wakati ongezeko la watu na mifugo katika Bonde la Ngorongoro kufikia 40% kwa mwaka. Kwa wakaazi wa Ngorongoro tulijua kwa vyovyote lazima kuna hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana na ongezeko hili lisilovumilika.

Kwa kipekee naipongeza serikali kwa kuchukua hatua za kiungwana kufanya mazungumzo na viongozi wa kimila na hatimaye tumepata suluhisho la kudumu na linalojali maslahi ya wananchi.

Kwa wasiojua zifuatazo ni baadhi ya faida tunazopewa kama mchango wa serikali katika suala zima la kukabiliana na changamoto iliyopo mbele yetu;

1.Kupewa Nyumba yenye vyumba vitatu ya tofali na iliyokamilika bure.

2.Kuhakikishiwa huduma zote za kijamii zikiwemo maji, umeme, shule na hospitali katika makazi mapya yenye ukubwa wa mita za mraba 400,000.

3.Kuingizwa rasmi kwenye miradi yote ya maendeleo ya serikali.

4.Kukabidhiwa hati ya viwanja ambavyo vimekwishapimwa ambayo ni fursa kwetu kutumia hati hizo kuweza kupata mikopo mbalimbali ya maendeleo katika taasisi za kifedha.

5.Kuepushwa na muingiliano na wanyama wakali kama Simba, Chui, Nyati na Faru ambao mara kadhaa wameleta kadhia kwetu na hata wanyama wapole kukimbilia nje ya hifadhi.

Kupatikana kwa suluhu hii juu ya muafaka wa bonde la Ngorongoro ni matokeo ya usikivu wa serikali kwa kuwapa kipaumbele viongozi wa kimila kutoa mapendekezo ya nini kifanyike badala ya kutumia nguvu.

Nichukue fursa hii kuwakemea wale wanaoendesha NGO’s mbalimbali kwa kuwatumia wakaazi wa Ngorongoro kuomba fedha kwa wahisani waache tabia hiyo kwani haina manufaa nchi yetu bali kuchafua taswira yetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA [emoji1241]
 
Ivi nikweli mtu akiwa hadhi ya waziri mkuu hana wahariri? Wasaidizi wa kazi hizo? Any way kwa elimu aliyikuwa nayo wakati Ana andaa hotuba yake hakufikiria kitu kama hicho? ... duh
Kinaitwa kiwewe cha kutaka mambo yaende fasta fasta
 
Viongozi ni "akisi" ya waongozwa. Ukiona kiongozi ni "mbumbumbu" ujue raia ni "mbumbumbumbumbumbu".

Hapo ukihoji/ukibisha hizo takwimu raia watakujibu "kwa hiyo tukuamini wewe au tumsikilize Waziri Mkuu?", na mimi huwa nawajibu "msikilizeni Waziri Mkuu"
 
Back
Top Bottom