kagombe
JF-Expert Member
- Mar 1, 2015
- 3,615
- 1,805
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameamua kukutana na kuongea na Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo leo ambapo tayari amefika Kariakoo muda huu badala ya Jumatano May 17,2023 ambayo ilitangazwa hapo wali hii ni kutokana na uzito wa suala hilo.
Awali mkutano kati ya Waziri Mkuu na Kamati ya Wafanyabiashara hao pamoja na TRA na Mawaziri wa Sekta husika ulitarajiwa kufanyika saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni-Ikulu Dar es salaam Jumatano May 17, 2023 kwa uratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, lakini Waziri Mkuu ameamua aende leoleo Kariakoo.
Pia Soma:
- News Alert: - Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023
Oya hii habari mbona update yake inachelewa nini tatizo sie tuliombali na huko !?