Uamuzi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, umekuja baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara walioitisha Mgomo wa kutofungua Maduka leo Mei 15, 2023
Majaliwa amesema ‘Task Force’ hizo zimekuwa zikitumika kufanya kamatakamata ya Wafanyabiashara na wakati mwingine kujihusisha na Vitendo vya Rushwa
Ameongeza “Kamishna wa Mapato ya Ndani TRA,naagiza Task Force isitishwe, Kanuni zipo, Sheria zipo zinatuelekeza namna ya kulipa Kodi, kamatakamata hii inafukuza Wafanyabiashara Kariakoo na mbaya zaidi mnawakamata hadi Wageni kutoka nje”