Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afika Kariakoo. Aagiza task force za TRA kusitisha shughuli zake haraka

Hatuna maono..watu waende kwa wenzetu wajifunze. Tatizo pia kuna mitandao ya rushwa..afisa anapewa laki mbili anahujumu kodi za mamilioni. We still have very long journey to go.
 
Wamekata umeme leo bungeni ili suala hilo lisijadiliwe kwa hofu ya baadhi ya wabunge kuliibua huko lijadiliwe kwa dharura.
 
Lipeni kodi , mnakwepa sana kodi
Baadhi ya mabango ni vigumu kuamini kwamba ni madai ya hawa watu.

Kwa mfano:
1. Kusajili 'Store' ni sheria kandamizi? Wanataka wao iweje?

2. EFD inaua biashara?

3. Wanataka "Uhuru" wa Biashara? wafanye watakavyo wao; bila kujali matakwa ya sheria zinazosimamia kazi zao?

Naona hapa kuna tatizo, na inawezekana wanakomaa kwa kujua alieko Ikulu ni mtu wa kusikia kila wanachotaka wao.
 
Eti bana, hawa wana janja janja nyingi
 
Ni haki yao kufunga au kufungua maduka na serikali haiwezi kuwalizimisha wafanyabishara kufanya kinyume na matakwa yao.

Tuliza akili.
 
Nadhani PM amekosa ushawishi, kwenye hili.

Maneno matamu, lakini vitendo zero.

Ndio maana wameendelea kugoma.
Serikali ilifanyie hili kazi kwa upya na uwazi zaidi ili shughuli na maisha virejee Kariakoo.

"Usipoziba ufa utajenga ukuta"
 

Unajua mfanyabiashara wa Tanzania analipa kodi ngapi?? Ungekua unafanya biashara usingeandina huu ujinga. Tokeni huko maofisin mje kwenye biashara ndo mjue tunavyokutana navyo.
 
Unajua mfanyabiashara wa Tanzania analipa kodi ngapi?? Ungekua unafanya biashara usingeandina huu ujinga. Tokeni huko maofisin mje kwenye biashara ndo mjue tunavyokutana navyo.
Ni wazi kabisa hapa "mjinga" ni nani kati yangu na wewe.

Ujinga wako unatokana na kutoelewa kilichoandikwa hata kama unajua kusoma.

Usingekuwa mjinga ungetambua kwamba swala linaloongelewa siyo "kodi ngapi" anazolipa huyo mfanya biashara.
Ungejua swala la msingi ni kila mhusika atimize wajibu wake unapowekwa utaratibu kisheria.

Hizo "kodi ngapi" unazozungumzia wewe huko ndiko kunakotakiwa kushikia bango kabla ya sheria husika hazijatengenezwa kuhalalisha kodi hizo.

EFD unaikataa wewe kama mfanya bisahara, wewe kweli ni mfanya biashara au jambazi tu huko mitaani?
Sidhani kamwe kwamba wewe unao uelewa kweli wa kufanya biashara ni nini hasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…