Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

Polisi wakifanya ujambazi ajiuzuru waziri mkuu?
Unayo haki ya kushangaa kwasabb umekulia ktk jamii ovu hivyo umejazwa uovu. Mpk kwenye umri wako hujui kitu kinaitwa "uwajibikaji wa pamoja" (collective responsibility).

Hapa ndipo nchi za watu zinapotupiga gap
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
Kwanini ajiuzulu wakati muda wake wake wa kustaafu uko karibu? Ingekuwa yeye mwenyewe personally ana skandali za kumlazimisha kujiuzulu hapo kweli; lakini kama yeye mwenyewe yuko salama, ni afadhali asubiri muda wake wa kustaafu kwa hiari ufike.
 
labda akijiuzuru kuna baadhi ya haki za kimafao anapoteza kuliko akisubiri asataafishwe. umri wake nao umeenda. au wenye uelewa watuambie, manake ukiona hadi maza kasema polisi wajitathimini, ndio lugha yenyewe hiyo kwamba kama usipojitathimini unaweza kufurushwa kinguvu na kwa aibu, sema kwasababu polisi huwa na roho ngumu hilo sio la kuogopa kwao.

😜😜😜
 
Kwa umri wake hana cha kupoteza ningemuona ana busara sana akijiuzulu maana kama kama kuchuma kachuma sana na tayari keshaandika rekodi ya kuwa IGP.
Sio tu IGP bali wa hovyo kuwahi kutokea
 
Gangster Disciples, Black Stones, BDs The biggest street gang is the CPD!
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.

Tuna mfano gani wa IGP ambaye amewahi kulifanya Jeshi la Polisi liing’arishe Serikali ya awamu yoyote ile?
 
hakuna kupeleka watu wa dini hapo, kwasababu ukigusa kwenye dini tu itabidi uweke kila dhehebu, hao wawakilishi wa dini usifikiri huwa wanawakilisha kila mtu, mfano , padre akienda pale usije fikiri ananiwakilisha mimi, anawakilisha wakatoliki, bado kuna waprotestanti,wasabato n.k, futa hayo mambo. weka watu wa serikali. ambacho najua huwa kinatokea hapo wataweka mtu wa tiss, jeshi, polisi, mwanasheria,pccb, na wengine kadhaa. na kwenye timu kama hizo hakika huwa wanafanya kazi ya kueleweka kwasababu wao kwa wapo pia huwa wanakaa kwa machale ya kuchunguzana wao kwa wao na kila mtu ana report kwa boss wake hivyo ni ngumu kuconspire kudanganya. hapo najua kuna moto utawawakia hao wakubwa aliowasema baba wa marehemu polisi na hao waliosababisha kifo cha mfanyabiashara. hata hao walioko gerezani kwa tuhuma wakahojiwe vizuri. patachimbika, na waongezewe ulinzi huko gerezani.
Hapana, hauko sahihi.
Akiwepo Sheikh mmoja na Askofu mmoja walioteuliwa na Viongozi wenyewe wa Dini, wanaifanya Tume iwe Huru.
Na nimemsikia Rais akitamka kuwa amemwagiza Waziri Mkuu aunde Tume Huru.
Tena Mwenyekiti wa hiyo Tume anatakiwa kuwa Wakili Msomi Mwandamizi, 'Senior Counsel'.
Vinginevyo, haitakuwa Tume Huru.
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
Kivipi,,? Kwanini unambebesha siro mzigo si wake?, Hata nchi zilizoendelea kama US kuna uhalifu mkubwa tu,, [emoji23] badi IGP wa marekani wangekuwa wansjiuzulu kila wiki,
Ndugu zangu wakristo tupendane,,, chuki haijengi, wewe igp akijiuzulu urafaidika na nini?..
Ntakutana mzee oohoo[emoji57]
 
Nashindwa kuelewa Uwajibikaji wa WAZIRI wa Mambo ya NDANI na IGP SIRRO kwenye SAKATA la KUUWAWA Mfanya Biashara wa MADINI na Kuporwa Fedha zake na POLISI.
Leo Mh.RAIS SAMIA Ameshangazwa kuundwa kwa TUME ya Kuchunguza hilo SAKATA na POLISI wenyewe WANAOTUHUMIWA na Kumwagiza WAZIRI MKUU Kuunda KAMATI HURU ya KUCHUNGUZA TUKIO HIYO bila KUWAHUSISHA POLISI
Baadae WAZIRI MKUU Akamwagiza IGP SIRRO Awasimamishe kazi RPC na RCO na Maofisa Wengine.
Najiuliza
1.Kwanini WAZIRI mwenye Dhamani Hakumwagiza IGP SIRRO kuwasimamisha KAZI hao WAHUSIKA hao Mpaka WAZIRI MKUU Atoe AGIZO?
2.Kwanini IGP SIRRO binafsi hakuwasimamisha kazi hao Wahusika au ndio KUWALINDA hao WAKUBWA?
View attachment 2107931

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Nasikia mbatia anapanga kufungua kesi, akihoji kwanini waziri wa mambo ya ndani hakuunda tume,,,
Nduguzanguni wakristo, tujitahidi kuwa na upendo, ,
Bwana wetu yesu kristo amesisitiza sana hili,,
Tuacheni roho za kwanini, nduguzanguni[emoji1745]
 
Nilitegemea Waziri Mkuu atakuwa na Ujasiri wa kuteua Wajumbe wawili kutoka kwenye Kamati ya Haki na Amani ya Viongozi wa Dini. Awemo Sheikh mmoja na Askofu mmoja ili Ripoti ya hiyo Tume ikubalike, iwe 'credible'.
Kuweka Watumishi wa Serikali pekee kunatia shaka.
Na wazee hata wawili wa kiboloroni[emoji23]
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
Yani mpaka Rais ameingilia wakati hao watu kiutendaji wako chini yake na ipo wazi kabisa uwepo wao pale unaweka mashaka kuhusu upelelezi maana wale ni maofisa ingekuwa askari w chini wangewato kafara Ila hao maofisa Kuna walakini wangewafichia jinai.

Kwanza kabisa upelelezi ujikite kwenye kifo Cha huyo ofisa anayedaiwa kujinyonga. Haiingii kichwani mtu ajinyonge akiwa lock up kwanza aliwekwaje peke yake wakati wengine wamewekwa wapi??????

Wamemuua yule mmoja ili wapoteze ushahidi yawezekana yule hajahusika Ila ndio wanamuangushia jumba bovu marehemu ili hao wengine wajitoe.

RCO na RPC hawawezi kuachwa kwanza kitendo Cha wao kuchelewa kutoa amri ya kukamatwa hao maofisa ni kiashiria tosha kwamba walitaka kuficha huo uhalifu hawapaswi kuachwa actually hata kama hawajahusika directly lazima waadhibiwe kijeshi ikiwemo kushushwa vyeo na wasipandishwe kwa miaka kadhaa hata kumi.
 
CP Juma Awadh na DG Takukuru Hamduni mmoja kati ya hawa anatarajiwa muda wowote kurithi kiti cha IGP Sirro,
 
Back
Top Bottom