hakuna kupeleka watu wa dini hapo, kwasababu ukigusa kwenye dini tu itabidi uweke kila dhehebu, hao wawakilishi wa dini usifikiri huwa wanawakilisha kila mtu, mfano , padre akienda pale usije fikiri ananiwakilisha mimi, anawakilisha wakatoliki, bado kuna waprotestanti,wasabato n.k, futa hayo mambo. weka watu wa serikali. ambacho najua huwa kinatokea hapo wataweka mtu wa tiss, jeshi, polisi, mwanasheria,pccb, na wengine kadhaa. na kwenye timu kama hizo hakika huwa wanafanya kazi ya kueleweka kwasababu wao kwa wapo pia huwa wanakaa kwa machale ya kuchunguzana wao kwa wao na kila mtu ana report kwa boss wake hivyo ni ngumu kuconspire kudanganya. hapo najua kuna moto utawawakia hao wakubwa aliowasema baba wa marehemu polisi na hao waliosababisha kifo cha mfanyabiashara. hata hao walioko gerezani kwa tuhuma wakahojiwe vizuri. patachimbika, na waongezewe ulinzi huko gerezani.