Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

Kwa umri wake hana cha kupoteza ningemuona ana busara sana akijiuzulu maana kama kama kuchuma kachuma sana na tayari keshaandika rekodi ya kuwa IGP.
Akijiuzulu atazikwa kijeshi?
 
Waziri Mkuu mh Majaliwa amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO wa Mtwara na OCD na OCID wa Kilindi Tanga ili kupisha uchunguzi wa Tume aliyoiunda.

Pia, Waziri Mkuu Mkuu Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu 9 yenye watu kutoka ofisi mbalimbali za serikali ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, mkoani Tanga. Ameipa siku siku 14 kukamilisha kazi hiyo kuanzia kesho.

====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

“Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,” amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Mheshimiwa Rais amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati hiyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na askari polisi. Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 05, 2022 na mauaji ya Kilindi yaliyotokea Januari 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kamati hiyo ina maafisa wenye dhamana kutoka mamlaka tofauti za Serikali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Ofisi ya Mwanansheria Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mtwara na Kilindi ili kupisha uchunguzi wakati timu aliyoiunda ikifanya kazi yake.

“Viongozi hawa wanapaswa wakae pembeni, watahojiwa na hii timu wakiwa nje ya ofisi,” amesema Waziri Mkuu na kuwataja maafisa hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara (RPC), Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mtwara (RCO) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara cha eneo alilofia mfanyabiashara Mussa Hamisi Hamisi na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Greyson Mahenge anayedaiwa kujinyonga.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kilindi na Afisa Upelelezi wa Wilaya nao pia wakae pembeni kupisha uchunguzi

Pia soma:

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Mtwara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

Mauji ya wafugaji na wakulima wilaya ya Kilindi, soma Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji (Januari 30, 2022)

Mama kaupiga mwingi. Angekuwa mwendazake hao mapolisi wangepandishwa vyeo...

RIP Akwilina.... Mapolisi walikuua bila hatia na mwendazake akapiga kimya
 
Wengi walimchukia mzee magu lkn kiukwel alikuwa sahihi kwa mambo mengi.

Jambo kama hilo wala halihitaji kuchunguzana na kuunda tume za kuja kumaliza pesa, hapo ilitakiwa tamko litoke litakalo wa affect viongoz wote walioshindwa kufanya kazi zao mpka wasubiri rais wa nchi atoe tamko.

Kama huyo IGP hafanyi lolote mpka asubir amri, anafaida gan sas? Fukuza huyo weka mwingine atakae jari maisha ya watu.

Kama kesi inajulkana wauwaji ni polis, basi haraka sana washukiwa wasimamishwe kazi kwa kufanya unyama nje ya kazi zao,

..huyo PM na tume zake hanaga jipya
 
RPC wa Geita anaoneka mstaarabu sana na mtulivu akizungumza kwenye TV, system inaweza ikampromote au huyo Mama Kaganda kama wengi wanavyosema au achukuliwe mtu wa jwtz kwasababu jwtz hawana ubabaishaji.
 
Ijp hana malaka ya kuwasimamisha kazi mwenye mamlaka ni rais mwenyewe na tume ya utumishi ya polisi na magereza ambae mwenyekiti ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi
 
Ijp hana malaka ya kuwasimamisha kazi mwenye mamlaka ni rais mwenyewe na tume ya utumishi ya polisi na magereza ambae mwenyekiti ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Ndio wameshasimamishwa Sasa na kuchafanya hakuna.
 
RPC wa Geita anaoneka mstaarabu sana na mtulivu akizungumza kwenye TV, system inaweza ikampromote au huyo Mama Kaganda kama wengi wanavyosema au achukuliwe mtu wa jwtz kwasababu jwtz hawana ubabaishaji.
PCCB alipelekwa jamaa wa JW then kilitokea Nini?Alivuruga kishenzi,kapigwa chini akaletwa police mwenzako.
 
Nashangaa kwanini hawakuchunguza suala la Hamza. Hakuna utofauti.
 
Ndugu yangu Retired Sirro pesa ipo sema tu vile ving’ora vya kusafishiwa njia atavi miss sana ila hakuna namna atake asitake mwezi huu anapumzika rasmi.
Mh! anapumzika? Kwa kustaafu? mbona bado kama mika 2 hivi? Hizi ni habri za ndani si rahisi kuvuja kiasi hicho. figganigga ameandika kituko eti Kaganda ameshateuliwa!!!!!!! If wishes were horses, ..............Kituko kikubwa
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
Hamuhitaji kwa kutumia viashiria vipi? Wishes zako?
 
Waziri Mkuu mh Majaliwa amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO wa Mtwara na OCD na OCID wa Kilindi Tanga ili kupisha uchunguzi wa Tume aliyoiunda.

Pia, Waziri Mkuu Mkuu Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu 9 yenye watu kutoka ofisi mbalimbali za serikali ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, mkoani Tanga. Ameipa siku siku 14 kukamilisha kazi hiyo kuanzia kesho.

====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

“Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,” amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Mheshimiwa Rais amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati hiyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na askari polisi. Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 05, 2022 na mauaji ya Kilindi yaliyotokea Januari 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kamati hiyo ina maafisa wenye dhamana kutoka mamlaka tofauti za Serikali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Ofisi ya Mwanansheria Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mtwara na Kilindi ili kupisha uchunguzi wakati timu aliyoiunda ikifanya kazi yake.

“Viongozi hawa wanapaswa wakae pembeni, watahojiwa na hii timu wakiwa nje ya ofisi,” amesema Waziri Mkuu na kuwataja maafisa hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara (RPC), Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mtwara (RCO) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara cha eneo alilofia mfanyabiashara Mussa Hamisi Hamisi na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Greyson Mahenge anayedaiwa kujinyonga.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kilindi na Afisa Upelelezi wa Wilaya nao pia wakae pembeni kupisha uchunguzi

Pia soma:

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Mtwara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

Mauji ya wafugaji na wakulima wilaya ya Kilindi, soma Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji (Januari 30, 2022)

It is all rubbish as long as CCM ndio wanatoa amri! All mavi and rubbish!
 
Nashindwa kuelewa Uwajibikaji wa WAZIRI wa Mambo ya NDANI na IGP SIRRO kwenye SAKATA la KUUWAWA Mfanya Biashara wa MADINI na Kuporwa Fedha zake na POLISI.
Leo Mh.RAIS SAMIA Ameshangazwa kuundwa kwa TUME ya Kuchunguza hilo SAKATA na POLISI wenyewe WANAOTUHUMIWA na Kumwagiza WAZIRI MKUU Kuunda KAMATI HURU ya KUCHUNGUZA TUKIO HIYO bila KUWAHUSISHA POLISI
Baadae WAZIRI MKUU Akamwagiza IGP SIRRO Awasimamishe kazi RPC na RCO na Maofisa Wengine.
Najiuliza
1.Kwanini WAZIRI mwenye Dhamani Hakumwagiza IGP SIRRO kuwasimamisha KAZI hao WAHUSIKA hao Mpaka WAZIRI MKUU Atoe AGIZO?
2.Kwanini IGP SIRRO binafsi hakuwasimamisha kazi hao Wahusika au ndio KUWALINDA hao WAKUBWA?
View attachment 2107931

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo kwa hali ilivyo sasa. Kama Siri ndo katunga kesi ya MCHONGO inayomkabili Mbowe na kwa mambo yanavyokwenda yakimwendea Mrama, tutakuwa na haki ya kusema kuwa MWISHO WA UBAYA NI AIBU?
ngoja tuone picha linavuokwenda mpaka mwisho. Ila ikumbukwe kuwa STERLING HAUWAWI
 
kwa mienendo hii jeshi la polisi limepoteza credibility kwa wananchi.Hakuna haja ya kuchunguza wakati kuna hela zipo involved! Ni wazi tamaa ya pesa ilipelekea mauji hayo! Huhitaji kuwa mpelelezi kutambua nani mbaya katika hii kesi!
 
Unapoteza kazi Kwa tu milion tu, ovyo kabisa hawa policcm

Hiyo ni ajali kazini….unadhani wanaishije polisi toka mwaka 2015 hawajaongezwa mishahara huku gharama za maisha zikipanda!?

Wa kulaumiwa hapa ni serikali kutokuboresha maslahi yao…tuache utani hawa jamaa wapo busy sana,wanafanya kazi ngumu sana,hii mambo serikali inafanya mzaha sana….huwezi kuwatelekeza watu wanao shinda na silaha miaka kadhaa bila kuboresha maslahi yao,unategemea nn!?
 
Tajiri amefuga mbwa wakali Sana wezi hawawezi kuingia na wanatamani mbwa wote wauawe ili wapate fursa.

Sasa tajiri amepewa ushauri mbwa hawa wafungiwe ndani wasitoke Pia wasipewe chakula cha kutosha kwasababu hawasaidii chotote na tutakuwa na Amani wakiondolewa kabisa na tunaweza kuleta paka wengi wakafanya KAZI nzuri zaidi.

Maskini hawa mbwa tutakutana nao jalalani na uwezekano wa kupata kichaa ni mkubwa kazi wanayoiweza ni kuuma watu na watu hakuna lazima waombe KAZI DRC CONGO NA MSUMBIJI wengine wahamie Somalia wakistaafu warudi kutumiwa na wanasiasa.
 
Back
Top Bottom