Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasubiri nini ofisini au Afrika kujiuzulu ni dhambi?

Kwanza kwa jinsi watanzania walivyo huwezi kumwambia chochote kama hujamweka kwenye nafasi anaemwogope ni boss wake anaeweza kumwondoa kwenye ile nafasi kwaio kuanza kumletaPM kwenye hii issue ni kutafuta excuse ambazo hazina kichwa wala miguu
 
HAKUNA UTARATIBU wa KUJIUZULU NCHI HII
MPAKA ULAZIMISHWE na WAKUANDIKIE BARUA WEWE NDIO USAINI TU
 
Jamaa hakuna kitu
 
Kati ya PM na mwenyekiti wa chama na kiongozi wa nchi, je nani anapaswa kulalama?
 
waziri mkuu amekosa nguvu sababu wezi waliowekwa wamewekwa kwa kupitia rais mstaafu, huwezi kuwagusa hata mama kabaki kutukana tu hana ubavu wakuwatoa ila kawaomba waondoke, sasa waziri mkuu unamlaumu wa nini? hebu mpe nchi majaliwa awe rais halafu uone utajua kama hujui
 
Hapana we Sema Sasa hivi Kuna transparency ya Hali ya juu kupitia vyombo vya habari kwa mana kwamba vinaibua kila uozo na kuripoti ila kipindi kile kulikuwa Cha giza kiasi kwamba vyombo vilifiangwa na vichache vilivyobaki ni kusifu tu hata vikiona uozo hamna kuripoti kulipoti na ukifanya hivyo kwa lazima unatekw na kuuawa. Kwa Sasa Hali imebadilika ndo mana pm ule ujanja ujanja wa kwenda na makemera tumeone anafanya kazi umebuma mana na amejikuta kwamba hata kipindi kile uozo ndo ulikuwa too much ila nani wa kuripoti.
 
Kassim Achana Naye Ni Wa Aina Yake
Rais Anachapa Kazi Yupo Ofisini, Mnataka Kumuona Magomeni
 
Kwa nini ajiuzulu Waziri Mkuu?

Waziri Mkuu Lowassa alishajiuzulu, kujiuzulu kwake kumesaidia nini?
 
Kassim Achana Naye Ni Wa Aina Yake
Rais Anachapa Kazi Yupo Ofisini, Mnataka Kumuona Magomeni
Pm hamna kitu alibebwa na jpm kwa sababu kipindi kile vyombo vya habari vilizimwa hivyo transparency haikuwepo ndo pm akang'aa lakini kipindi hiki kila mtu anahoji na ana haki tofauti na kipindi kile Cha giza
 
Tofautisha Kati ya waziri mkuu Wa Uingereza na waziri mkuu Wa Tanzania. Huyu waziri mkuu Wa Tanzania Hana uwezo kufukuza kazi hata mkurugenzi Wa halmashauri tu, Hana nguvu yoyote na Mara nyingi utendaji wake hutegemea nguvu na empowerment ya Rais aliyeko madarakani.
 
Kairuki ni mzigo sijui anabebwa na mbeleko ya nani?
 
Kuna udhaifu kuanzia juu kule, wacheni kuhangaika na PM, ndio maana mafisadi wameanza kuvimba tena sababu wanajua hayupo wa kuwafanya chochote mama yao yuko upande wao, wale kina Silent Ocean ni mfano wao.

Tatizo sio Juu wala chini tatizo ni CCM.
 

wazungu muda mwengine wana vituko sana. Sasa walitaka muda wote awe analia?
 
Umetoa mifano miwili tofaut unatakiwa ujue muundo wa serikali. Uingereza ni mfumo wa kifalme ila msimamiz mkuu Wa serikali ni waziri mkuu na ndiyo mwenye nguvu kwahiyo lolote likitokea anawajibika yeye ila huku mfumo ni tofauti mwenye nguvu ni Raisi na waziri mkuu yupo kama kiongozi wa mawaziri tu na hata mawaziri Hawa report kwake ila wana report Kwa Raisi. Waziri mkuu ni kilanja tu miongoni mwa mawaziri. Hana kosa Kwa sababu Hana power ya kufanya maamuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…