Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasubiri nini ofisini au Afrika kujiuzulu ni dhambi?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anasubiri nini ofisini au Afrika kujiuzulu ni dhambi?

Kwa Tanzania PM siyo head of government, siyo appointing authority, siyo head of executive.
Kama ambavyo hawezi kumtengua mtu, hawezi kumteua mtu, basi pia hawezi kuwajibika kwa makosa ya watu wanaoteuliwa na mtu mwingine.
Rais aisimamie serikali yake.
Asijikite kuwaondoa Sukuma gang tu na kusahau kuwa macho na watu anaowaongoza ndani ya serikali.
Kwanza kwa jinsi watanzania walivyo huwezi kumwambia chochote kama hujamweka kwenye nafasi anaemwogope ni boss wake anaeweza kumwondoa kwenye ile nafasi kwaio kuanza kumletaPM kwenye hii issue ni kutafuta excuse ambazo hazina kichwa wala miguu
 
Licha ya madudu yote hayo yaliyooneshwa na CAG lakini bado anakalia ofisi tu? Hebu fikiria Waziri Mkuu wa Iingereza alijiuzulu kwa kosa tu la kucheza mziki kipindi Cha COVID 19 lakini sisi huku Waziri Mkuu ndo kwanza anachekelea. Hivi nchi za kiafrika tunelaaniwa?

Rais hawezi kumwambia Waziri Mkuu eti jiuzulu bali PM mwenyewe ndo nafsi inapaswa imsute. Jana Rais Samia kaongea very logical issues akimlenga pm kwamba hana lolote analojua kama mtendaji Mkuu wa Serikali.
HAKUNA UTARATIBU wa KUJIUZULU NCHI HII
MPAKA ULAZIMISHWE na WAKUANDIKIE BARUA WEWE NDIO USAINI TU
 
Anaongelea wizi halafu anacheka
Utajua kuna usanii kwenye hela zetu

Tutabaki masikini maisha yote
Haiwezekani mpaka leo eti hata kutatua mashimo ya vyoo mashuleni na hospitali wameshindwa

Kweli leo sisi wa kukubali watoto waende na majivu shuleni

Yaani wao wanafurahia udhalili wa mtz kwa kuwa hawezi kufanya kitu
Wao hakuna maisha wasiyoyaona yaani tunaishi tofaouti na wao
Huku wakicheka cheka tu
Hilo tabasamu linatusaidia nini kama majizi unakula nao?
Jamaa hakuna kitu
 
Kati ya PM na mwenyekiti wa chama na kiongozi wa nchi, je nani anapaswa kulalama?
 
waziri mkuu amekosa nguvu sababu wezi waliowekwa wamewekwa kwa kupitia rais mstaafu, huwezi kuwagusa hata mama kabaki kutukana tu hana ubavu wakuwatoa ila kawaomba waondoke, sasa waziri mkuu unamlaumu wa nini? hebu mpe nchi majaliwa awe rais halafu uone utajua kama hujui
 
Hapana we Sema Sasa hivi Kuna transparency ya Hali ya juu kupitia vyombo vya habari kwa mana kwamba vinaibua kila uozo na kuripoti ila kipindi kile kulikuwa Cha giza kiasi kwamba vyombo vilifiangwa na vichache vilivyobaki ni kusifu tu hata vikiona uozo hamna kuripoti kulipoti na ukifanya hivyo kwa lazima unatekw na kuuawa. Kwa Sasa Hali imebadilika ndo mana pm ule ujanja ujanja wa kwenda na makemera tumeone anafanya kazi umebuma mana na amejikuta kwamba hata kipindi kile uozo ndo ulikuwa too much ila nani wa kuripoti.
 
Kassim Achana Naye Ni Wa Aina Yake
Rais Anachapa Kazi Yupo Ofisini, Mnataka Kumuona Magomeni
 
Licha ya madudu yote hayo yaliyooneshwa na CAG lakini bado anakalia ofisi tu? Hebu fikiria Waziri Mkuu wa Iingereza alijiuzulu kwa kosa tu la kucheza mziki kipindi Cha COVID 19 lakini sisi huku Waziri Mkuu ndo kwanza anachekelea. Hivi nchi za kiafrika tunelaaniwa?

Rais hawezi kumwambia Waziri Mkuu eti jiuzulu bali PM mwenyewe ndo nafsi inapaswa imsute. Jana Rais Samia kaongea very logical issues akimlenga pm kwamba hana lolote analojua kama mtendaji Mkuu wa Serikali.
Kwa nini ajiuzulu Waziri Mkuu?

Waziri Mkuu Lowassa alishajiuzulu, kujiuzulu kwake kumesaidia nini?
 
Kassim Achana Naye Ni Wa Aina Yake
Rais Anachapa Kazi Yupo Ofisini, Mnataka Kumuona Magomeni
Pm hamna kitu alibebwa na jpm kwa sababu kipindi kile vyombo vya habari vilizimwa hivyo transparency haikuwepo ndo pm akang'aa lakini kipindi hiki kila mtu anahoji na ana haki tofauti na kipindi kile Cha giza
 
Tofautisha Kati ya waziri mkuu Wa Uingereza na waziri mkuu Wa Tanzania. Huyu waziri mkuu Wa Tanzania Hana uwezo kufukuza kazi hata mkurugenzi Wa halmashauri tu, Hana nguvu yoyote na Mara nyingi utendaji wake hutegemea nguvu na empowerment ya Rais aliyeko madarakani.
 
Sasa Kweli mama angu na wew kairuki anaweza kukusadia nn kwenye tamisemi jafoo mwenywe ilimshinda wee unakwenda kumteua mtu back wkt mle ndani Kuna wabunge mahiri tu wangekusadia

Ona Sasa Jana alikuwa anaangua kicheko

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kairuki ni mzigo sijui anabebwa na mbeleko ya nani?
 
Kuna udhaifu kuanzia juu kule, wacheni kuhangaika na PM, ndio maana mafisadi wameanza kuvimba tena sababu wanajua hayupo wa kuwafanya chochote mama yao yuko upande wao, wale kina Silent Ocean ni mfano wao.

Tatizo sio Juu wala chini tatizo ni CCM.
 
Licha ya madudu yote hayo yaliyooneshwa na CAG lakini bado anakalia ofisi tu? Hebu fikiria Waziri Mkuu wa Iingereza alijiuzulu kwa kosa tu la kucheza mziki kipindi Cha COVID 19 lakini sisi huku Waziri Mkuu ndo kwanza anachekelea. Hivi nchi za kiafrika tunelaaniwa?

wazungu muda mwengine wana vituko sana. Sasa walitaka muda wote awe analia?
 
Umetoa mifano miwili tofaut unatakiwa ujue muundo wa serikali. Uingereza ni mfumo wa kifalme ila msimamiz mkuu Wa serikali ni waziri mkuu na ndiyo mwenye nguvu kwahiyo lolote likitokea anawajibika yeye ila huku mfumo ni tofauti mwenye nguvu ni Raisi na waziri mkuu yupo kama kiongozi wa mawaziri tu na hata mawaziri Hawa report kwake ila wana report Kwa Raisi. Waziri mkuu ni kilanja tu miongoni mwa mawaziri. Hana kosa Kwa sababu Hana power ya kufanya maamuzi
 
Back
Top Bottom