Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Wanabodi najua kabisa tupo kwenye msiba mkubwa. Msiba ambao umemgusa kila mtu na mpaka sasa kila Mwananchi haamini kilichotokea...
Itabidi nawe ufunguliwe mashtaka uliamini vp bila Kuchunguza kwanza. Pole anyway
 
Hizo teknic za kudanganya umma kwa madai ya kuulinda na kuwa hawawezi kuhandle ukweli ni za kizamani na kishamba sana.
 
Wanabodi najua kabisa tupo kwenye msiba mkubwa. Msiba ambao umemgusa kila mtu na mpaka sasa kila Mwananchi haamini kilichotokea...
NDIYO> Wapo wengi tu watakaoendelea kumwamini Waziri Mkuu. Ila kwa wale wasiojua mfumo, utaratibu, na itifaki za uendeshaji wa nchi, ndio watakao acha njia panda kwani si kila kitu kinachomhusu kiongozi wa nchi, kinapaswa kuwekwa hadharani...

Hata weye kwenye level ya familia yako, sidhani kila jambo nyeti linalokuhusu, unawatangazia watoto na wategemezi wako!

Pale inabodi kutangazwa, hutangazwa sawia baada ya kufanya maandalizi muhimu ya kiitifaki, ili kuepusha taharuki katika jamii.
 

Siyo sahihi kabisa kudanganya,kwanza sidhani kama kuna mtu alimuuliza Rais yuko wapi pale msikitini. Hivyo angeendelea kukaa kimya kuliko kudanganya msikitini
 
Thread hii imeanzishwa na january2021 naona kama anamnanga pm akijipigia debe kiaina ingawa anasema ukweli
 
Ametakiwa akijuzuru na nani?

Kigezo gani unachokitumia kumtuhumu WM kwamba alidanganya?

Taarifa ya Mh Samia inasema hayati Mh Magufuli alilazwa tarehe 6/3/2021 katika hospitali ya Mzena jijini Dar Es Salaam, akatibiwa kisha akaruhusiwa kurejea na majukumu yake ya kazi.

Tarehe 12/3/2021 huko Njombe waziri mkuu alitoa dokezo kwamba aliongea na Mh Rais jana yake ambapo alimhakikishia kuwa ni mzima anaendelea na kazi.

Kwa mjibu wa taarifa ya Mh Samia alisema kwamba tarehe 14/3/2021 Mh hayati Dir Magufuli alisikia vibaya ambapo aliwahishwa hospitali ya Mzena, akalazwa ambapo madaktari walibaini tatizo kwenye mfumo wa umeme wa moyo; jitihada ilifanyika kutoka kwa madaktari bingwa lakini mnamo tarehe 17/3/2021 saa kumi na mbili jioni Mh hayati Dr. Magufuli alifariki dunia

Mh Samia alitangaza kifo cha Mh Hayati Dr. Magufuli baada ya kupata taarifa za uthibitisho kutoka mamlaka husika tarehe 17/3/2021 saa tano na dakika kadhaa usiku.

Mnaotoa msukumo wa WM kujiuzuru mtakuwa mmetumwa na watu fulani wenye uchu na cheo hicho kwa maslahi yao ya kisiasa lakini pia kutoa nafuu kwa upande wa pili kinzani kwa kuwa wamekuwa watoa siri wao.
 
Mmeanza mapema hivi? But Mungu ataipigania Tanzania.
Mashujaa wote hawawezi kuanguka siku moja
Kumbuka kwamba baada ya tamko lake lile kuna watu walikamatwa kwa kumzushia Rais ugonjwa.

Na siyo yeye tu. Yuko Chalamila (RC Mbeya) na Mwigulu Nchemba (Waziri wa Katiba na Sheria). Wote wanapaswa kujiwajibisha au kuwajibishwa kwa matamko yao ya uongo.
 
Hili jambo nimelifikiria sana, kwanini hawakutangazia wananchi ili tujue rais wetu ni mgonjwa
Kigogo ndiye anayetutangazia kwanini tusimuamini kuliko hawa viongozi wetu.
 
Siyo waziri mkuu tu, hata mama Samia akiwa Tanga alisema rais mzima anawasalimia. Msimwonee majaliwa.
 
Siyo sahihi kabisa kudanganya,kwanza sidhani kama kuna mtu alimuuliza Rais yuko wapi pale msikitini. Hivyo angeendelea kukaa kimya kuliko kudanganya msikitini
Kiprotocol alipaswa kulisemea hili, Pal msikitini palikuw mahali pa kusemea tu, kwa sababu pia wanapewaga nafasi hiyo ya kusema neno!! kumbuka wakati anayaongea haya alikuwa hajafa!!! umeelewa!! alikuwa anapiga story na kufanya baafhi ya majukumu mepesi!!

mgonjwa akiwa wardin anapiga mswaki anaangalia TV, na mambo meeengi sana sasa kwa nini aseme amekufa wakati hajafa? hata kama angekufa mapema kabla ya wakati inategemea Dr amemwambia nini kinaendelea!! , yeye alisema kwa mijibu wa Dr wa zamu, sijui unaelewa au.....

huwezi sema tu amekufa wakati siyo mael;ezo ya Dr...
 
Iko wazi na tumejionea jambo hili likitokea mara kadhaa ingawa limetamalaki zaidi katika kipindi cha karibuni hasa wakati ambao Jiwe hakuwa hadhari kwa umma.

Kwa kutojua au kwa kujua wasaidizi wake VP na PM wakawa wanajigamba hadharani bila woga wala hofu ya Mungu wanayemtanguliza mbele kila siku kuwa Jiwe yuko salama na anafanya kazi akiwa ofisini.

Nakumbuka katika wiki ambayo taharuki ya kuuliza wapi jiwe alipo ilizuka katika social media PM akiwa Msikitini, , , nasema akiwa Msikitini akatamka wazi kwamba Jiwe yupo salama anafanya kazi zake vema na amemtuma afikishe salamu zake, huku akiwatuhumu watu walio nje ya nchi kuwa wanaombea wenzao kufa na kuwa siyo wazalendo (Akimlenga Tundu Lissu) Kumbe wakati huo Jiwe yupo Mzena anapumulia mashine kwa kupambania luku isikate kwenye moyo.

Haya, huyu aliyekuwa VP naye akiwa tanga mbele ya Umma tena Umma uliyompa kura yeye na boss wake bila woga anadiriki kuudanyanga kwamba Jiwe anawasalimia sana tena anawashukuru kwa kumpa kura lukuki kumbe wakati huo huo Jiwe ndo anauma shuka.

Jamani mtuheshimuni basi hata kama si kwa umri basi kwa kura nyingi tulizowapeni maana ukiwa kiongozi wewe siyo wewe mwemyewe ( wewe siyo mali yako mwenyewe) bali mali ya waliokupa uongozi, na kwa maana hiyo wanao uhalali wa kuhoji mahali ulipo na nini unafanya, pia nawe unawajibika kujibu hoja zao.

Nikuulize PM kinachokuliza leo ni nini wakati pale Msikitini ulitamka wazi kwamba Boss wako ni mzima na anachapa kazi alafu siku tatu badaye akauma shuka. Au tulikuelewa vibaya ulikuwa una maanisha anachapia kazi Kitandani Mzena?

Sasa Kwanini Viongozi Wanadanganya, nitasema chache!

1: Kutunza/Kuficha udhaifu, Hii ndiyo sababu kubwa kuliko zote.
Kiongozi wa aina yeyote popote duniani awe wa kisiasa, kidini nk hapendi udhaifu wake uonekane wazi kwani kwa kufanya hivyo wapinzani wake wanautumia kama fursa ya kumuondolea imani kwa watu wake.

2: Usalama/ Ulinzi binafsi, Mf, Japo Jiwe alikuwa amelazwa hospital kwa muda wa karibu wiki mbili na mbali na kwamba anahakikishiwa ulinzi 24/7 bado haitoshi kuamini moja kwa moja kuwa kuna usalama 100% bila kujali hospital hiyo niya Jeshi au inaaminika kwa usalama kiasi gani.

3: Usalama wa nchi, Mf kwenye nchi zanye vita ikitokea kiongozi wa nchi hiyo anaumwa kiasi cha kushindwa kutekeleza majukumu yake au amefariki siyo rahisi kutangaza kifo chake kwani waasi/wadai haki watatumia mwanya huo kutimiza kusudio lao kwani nchi inakiwa haina kiongozi wa moja kwa moja wakati huo.

4:Hofu na Woga (Uoga) itaonekana kwamba wahakuwa makini ktk kuaminisha uuma juu ya mtu waliyemwamini katika utekelezaji wa malengo yao, hivyo imani ya watu juu yao itapungua.

5: Kupunguza taharuki [emoji23] (Haina mashiko ni 7bu ya kisiasa) Wanadai kwamba kuficha taarifa za kweli kwa wakati sahihi ni kuandaa watu Sycologically kuamini kwa kutokuwa na uhakika kwamba huenda jambo hilo ni kweli au sivyo.
Wanaeleza kuwa kwa kufanya hivyo watu wanakuwa tayari kwa lolote hivyo hata ikitokea kwamba jambo lililohisiwa ni kweli basi pressure inakuwa ishapungua kulinganisha ukweli kuwekwa wazi directly!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…