Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatakiwa kuwajibika kwa kudanganya Taifa lililokuwa na taharuki kubwa

Wakati tukiendelea na maombelezo ya kuondokewa na kiongozi wetu, ni muhimu pia kutafakari kwanini hatukufahamishwa rasmi juu ya kuugua kwake hadi kupelekewa kifo chake.

Maoni ya wananchi wengi juu ya msiba huu wa taifa yanaambatana na lawama kwa viongozi wa serikali kutokulifahamisha taifa juu ya kuugua kwa Rais wao.

Wanasema endapo wangejulishwa, wangemuomba Mungu amnusuru na maradhi yaliyopelekea kulazwa na hatimae kufariki na huenda Mungu angepokea maombi hayo au angalau angempa nafuu kidogo ya kuweza kutoa kauli ya kuwaaga. Zaidi waanalaumu kwamba serikali haikumtendea haki Marehemu ya kuombewa na wananchi wake aliokuwa akiwatumikia ikizingatiwa kuwa marehemu katika uhai wake alikuwa akiwaomba wananchi wamuombee kheri kwa Mungu.

Kwa mtazamo wangu juu ya jambo hili naamini serikali ilizingatia ule msemo "heri lawama kuliko fedheha" na kwahiyo ililazimika kuchagua LAWAMA badala ya FEDHEHA.

Kudhihirisha kwamba Rais ni mgonjwa ni jambo la fedheha/aibu hasa ikizingatiwa ukweli kuwa kuugua kwakwe kumetokea wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa korona ambao yeye na serikali yake wamekuwa wakikaidi kuonesha uwepo wake hapa nchini hata wakakwepa kuutambua kwa jina lake na badala yake kuubatiza jina la "changamoto ya upumuaji". Lakini kwakuwa tayari ilishaaminika na wanchi kuwa hiyo "changamoto ya upumuaji" inaambukiza na kusababisha watu kuugua au kufa kama korona na kwamba ikiwa changamoto hiyo tayari imeua wasaidizi wa karibu wa Rais, basi kivyovyote vile Rais hasingeweza kusalimika hasa ikizingatiwa kuwa hakuwa anachukuwa tahadhari yoyote kujikinga na maambukizi hayo.

Hakuna ubisha kuwa Rais alikuwa mkaidi kupindukia na ukaidi huo ulitokana na kupenda sifa aonekana yeye ni "MWAMBA" na hatishwi na chochote hata kile kinachoitwa "korona". Lakini pia alifanya hivyo ili aonekana yeye ni mchamungu na kwamba Mungu angemlinda na maradhi hayo.

Kwa misingi hii ni heri kwa Rais na seririkali wabebe LAWAMA hizi za wananchi kwa kuficha ukweli kuliko FEDHEHA ya kutangaza kuugua kwani kivyovyote vile ingeaminika kuwa maradhi hayo ameambukizwa na wasaidizi wake kutokana na ukaidi wake na kwamba korona ni mshindi dhidi ya misimamo ya serikali.

Ni hivyo tu.
Unastahili tuzo Kwa uchambuzi ulioshiba hongera sana kiongozi wangu hujabeza wala kudhihaki[emoji120]
 
Si umeambiwa tarehe 7 aliruhusiwa kurudi nyumbani kisha alirudishwa hospitali tarehe 13?
Kwahyo kumbe alipokua haonekani alikua anaumwa na kulazwa then akaruhusiwa kwa ajili ya recovery? Sasa kwanini aliruka fact kwamba KWELI ALIUMWA ila AMERECOVER??

Hapo ndio alipokosea...... Angekaa kimya tu kuliko kuongea asichokua na uhakika nacho
 
Hajadanganya, alitoa taarifa ya kufariji.

10 tena kwa PM.
 
We hukumsikia! Hata suala la hospitali hakulitaja. Alisema rais mzima anaendelea na majukumu yake. Kwenye hili pm atuombe radhi watz.
Kwenye taarifa ya VP alisema Rais aliruhusiwa kutoka hospital trh 7 na aliendelea na kazi zake kabla ya kuzidiwa tena, Kwa hiyo PM alikuwa correct aliposema kuwa Rais anachapa kazi zake hakudanganya wakuu unless kama tulichopewa kwenye taarifa siyo sahihi lakini kama ndivyo PM alisema kweli
 
For security purposes state ya ugonjwa wa Rais inakuwa confidential saa nyingine hata Waziri Mkuu sio lazima ajue au aliongelee and especially kwa nchi kama hii ya Tanzania ambayo kila kitu kila saa ni siasa tu
Only in Banana Republics,Kumbuka Trump alipougua covid19 mambo yakawekwa hadharani mpaka dawa alizopewa
 
Wanabodi najua kabisa tupo kwenye msiba mkubwa. Msiba ambao umemgusa kila mtu na mpaka sasa kila Mwananchi haamini kilichotokea.

Lakini yapata kama wiki moja iliyopita taifa zima lilikumbwa na taharuki kubwa. Kila raia mwenye mapenzi na mkuu wa nchi yetu alitaka kujua kama anaumwa au haumwi. Wapo waliojitolea kuwa wapiga mbiu. Wao walisema kuwa Rais anaumwa na yupo hoi

Ghafla akaibuka Waziri mkuu akiwa ziarani huko nyanda za juu kusini. Alitoa tamko ambalo sababu yeye ndio msimazi wa shughuli za serikali kila mwananchi alimuamini. Aliwahakikishia watanzania kuwa Rais haumwi na anachapa kazi kama kawaida.

Tamko la Waziri mkuu kuwa Rais alikuwa mzima linakinzana na taarifa tuliyopewa na makamu wa Rais kuwa tangu tar 6 March Rais amekuwa mgonjwa tena aliyekuwa amelazwa.

Je, kwa hali ya kawaida kuna raia ambae bado anaweza kumuamini Waziri Mkuu tena?
[/QUOTE

Na ajiuzuru tu sisi angesema mapema tunfafanya maombi Taifa zima angepona Rais wetu...
 
Walikuwa wanahakikisha usalama wa Taifa kwanza kabla ya kutangaza rasmi.
 
Waziri Mkuu alikuwa sahihi tena sahihi kabisa!! kutamka aliyo tamka naomba mnielewe!! taarifa km hii inaruhusiwa Kisiasa, kiutamaduni, na kiuchumi pia!! hata mie nilikuwa km wewe lkn nikafikiri tena kwa mtizamo tofauti baada ya kusikiliza hotuba yake fupi kwa kina kwa sababu zifuatazo;

1. Uongo mtakatifu unao fanana na ukweli, hii ina kubalika hta Mbinguni kwa Mungu!! mbali na hii kwani Majaliwa yeye ni Daktari kusema kwamba alimpima mgo njwa yeye akatoa hili jibu?

Yeye km muuguzaji aliwakilisha taarifa km ilivoletwa kwake na Madaktari wa zamu wa siku hiyo, wakati anajiandaa kweenda msikitini!! akaona atumie hiyo nafasi!! ,,, hata kusign baadhi ya nyaraka RAIS alikuwa anafanya kazi hizo akiwa akingali kwa Hosp!! akasema kwani alikufa siku aliyo sema hayo maneno au alikufa baadaye? Rais habebi vyuma kusema eti ata shindwa ku sign na kutoa maelekezo tuu!!

2. Imani kuu aliyo kuwa nayo dhidi ya Boss wake aliamini Mungu ana mlinda Rais! kwa gharama kubwa lkn Mungu kaamua vinginevyo akamchukua!! sasa waziri mkuu afanyeje akaamsute Mungu siyo?? kikubwa ni imani aliyojawa nayo muhusika.

3. Jopo la madaktari liliokuwa lina shughulika na tiba ya Rais aliliamini mno na lilikuwa likimtia Moyo na hii ni tabia za tabibu wote Duniani hata km mgonjwa wako amekufa hawawezi kukupa jibu la moja kwa moja, kwa nini kaulize wenye taaluma yao matabibu ndo kazi yao!

4. Huduma nzuri na za kisasa! alizopewa marehemu alijua zita msaidia tu.

5.Maombi aliyo piga Majaliwa na familia yake usiku na mchana ya kufunga na kuomba aliyaamini lkn Mungu kaamua vinginevyo, mkitaka muulizeni Mungu.a

6.Watanzania wenye Imani waliingia kwenye Maombi pamoja na waziri Mkuu! ili kumtia nguvu inaonyesha waziri alikuwa na imani thabiti lkn Mungu akaamua vinginevyo! alitamka ukweli kuhusu afya ya Rais kwa wakati ule lkn hali ilibadilika sasa amfufue?

7.W/Mkuu Anaamini Mungu akisema yeye kazi ya uwaziri Basi!! ni amesema, hawezi kupingana na kauli ya Mungu ambae amempa hiyo kazi, wewe ni nani mpaka uingilie kazi aliyo pewa na Maulana au unataka kuondoka na wewe umfuate Rais wako yule mtanashati??

8. W/Mkuu anaamini kila kitu kina mwisho wake, yeye ni nani asiwe na Mwisho? akasema wapo vigogo kuliko yeye waliopitia kwenye Moto km kina Saddam Husein nk na wakapotea mazima sembuse yeye W/Mkuu?

9;Anaamini km ipo!! ipo tu piga ua garagaza atabaki kuwa yeye! kama Mung akitaka. wangapi Mungu aliwakataa wako wapi! mfano Tafawa balewa Mungu alikataa waziwazi, Suka Buka Dimka Mungu alimkataa on the spot! anasema kwanza kufika hapo alipo ni Mungu tu! hakuwahi kuwazia hiyo nafasi kwanza ana mshukuru Mungu Na watanzania, kuwa km alivo leo! cheo ni dhamana alifundishwa hivo!

10, Kufa Boss wake siyo mwisho wa Safari yake kisiasa, Mungu alivo wa ajabu mnaweza kuniponda Leo kweli nikaondoka lkn Mungu akafungua milango zaidi Ikawa mwanzo mwingine mzuri kwangu na familia yangu na nikafanya Siasa za kimataifa na Bado mkanihitaji kuliko mnavoniona leo!!

Nasema hivi sioni tabu kuwajibika kama watanzania wakinihitaji kufanya hivo!! ni suala la muda tu!! utasema!!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa..... Aksanteni kwa kunisikiliza!!!!! alisema Majaliwa
 
Tena kibaya zaidi, kadanganyia kwenye nyumba ya ibada (msikitini)... shame on him... 🚮
Kassim Majaliwa kwa kusema uongo amepoteza imani kwa wananchi kwani kwa kusema uongo itakuwa vigumu kwa wananchi kumuamini kwa lolote lile atakalosema!! He has lost credibility; kwa busara tu naona angepisha mou mwingine achukue nafasi yake, asipofanya hivyo atakuwa kituko mbele ya wananchi popote atakapo fugua mdomo wake!
 
Msimuonee Majaliwa pekee. Kwani hata mama Rais mtarajiwa aliiambia dunia akiwa Tanga kuwa Rais alikuwa mzima akichapa kazi wakati alikuwa hoi. Kama ni kutenda haki basi tuwatendee wote. Ni ushauri tu.
 
For security purposes state ya ugonjwa wa Rais inakuwa confidential saa nyingine hata Waziri Mkuu sio lazima ajue au aliongelee and especially kwa nchi kama hii ya Tanzania ambayo kila kitu kila saa ni siasa tu
Security purposes zinalazimu ugonjwa wa Rais uwe siri kwa nini?

Tutavamiwa na maadui tukiwa na Rais mgonjwa????

Basi alipokufa wangeuchuna wamuapishe Samia kisiri siri the same freaking night ili kusiwe na power vacuum for security purposes...

Haya sasa kafa, hatuna Rais, mbona tuko njema??????

Kudanganya umma for security purposes is total nonsense, such foolish argument!
 
Security purposes zinalazimu ugonjwa wa Rais uwe siri kwa nini ?

Tutavamiwa na maadui tukiwa na Rais mgonjwa ????

Basi alipokufa wangeuchuna wamuapishe Samia kisiri siri the same freaking night ili kusiwe na power vacuum for security purposes...

Haya sasa kafa, hatuna rais, mbona tuko njema ??????

Kudanganya umma for security is total nonsense, such foolish argument!
Huelewi kitu wewe, kubishana na wewe ni kupoteza muda
 
Only in Banana Republics,Kumbuka Trump alipougua covid19 mambo yakawekwa hadharani mpaka dawa alizopewa
Tanzania sio US, wa TZ mnapenda sana kujilinganisha na mataifa yenya ustaarabu tofauti, uelewa tofauti nasi. Huku kwetu watau wanadanganyika kwa urahisi, wanaogopa kwa urahisi na nchi kuingia kwenye sitofahamu ni rahisi mno. Mnataka mfafanuliwe kila kitu kama watoto wa nursery?
 
Majaliwa na Mwigulu wamepoteza sifa kabisa, ni viongozi wasioweza kuaminiwa na wananchi tena! Waachie ngazi mara moja!
Wakuu wa Mikoa wa hovyo hovyo kama yule Chalamila wa Mbeya ,inabidi Mama Samia awapige chini maramoja!
 
Back
Top Bottom