Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
Hahahaha hilo nalo nenoVipi makamu wa Rais kule Tanga aliyetuambia kuwa anatusalimia,,,,,,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha hilo nalo nenoVipi makamu wa Rais kule Tanga aliyetuambia kuwa anatusalimia,,,,,,
Huyu jamaa sijui anatumia kilevi gani
Unastahili tuzo Kwa uchambuzi ulioshiba hongera sana kiongozi wangu hujabeza wala kudhihaki[emoji120]Wakati tukiendelea na maombelezo ya kuondokewa na kiongozi wetu, ni muhimu pia kutafakari kwanini hatukufahamishwa rasmi juu ya kuugua kwake hadi kupelekewa kifo chake.
Maoni ya wananchi wengi juu ya msiba huu wa taifa yanaambatana na lawama kwa viongozi wa serikali kutokulifahamisha taifa juu ya kuugua kwa Rais wao.
Wanasema endapo wangejulishwa, wangemuomba Mungu amnusuru na maradhi yaliyopelekea kulazwa na hatimae kufariki na huenda Mungu angepokea maombi hayo au angalau angempa nafuu kidogo ya kuweza kutoa kauli ya kuwaaga. Zaidi waanalaumu kwamba serikali haikumtendea haki Marehemu ya kuombewa na wananchi wake aliokuwa akiwatumikia ikizingatiwa kuwa marehemu katika uhai wake alikuwa akiwaomba wananchi wamuombee kheri kwa Mungu.
Kwa mtazamo wangu juu ya jambo hili naamini serikali ilizingatia ule msemo "heri lawama kuliko fedheha" na kwahiyo ililazimika kuchagua LAWAMA badala ya FEDHEHA.
Kudhihirisha kwamba Rais ni mgonjwa ni jambo la fedheha/aibu hasa ikizingatiwa ukweli kuwa kuugua kwakwe kumetokea wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa korona ambao yeye na serikali yake wamekuwa wakikaidi kuonesha uwepo wake hapa nchini hata wakakwepa kuutambua kwa jina lake na badala yake kuubatiza jina la "changamoto ya upumuaji". Lakini kwakuwa tayari ilishaaminika na wanchi kuwa hiyo "changamoto ya upumuaji" inaambukiza na kusababisha watu kuugua au kufa kama korona na kwamba ikiwa changamoto hiyo tayari imeua wasaidizi wa karibu wa Rais, basi kivyovyote vile Rais hasingeweza kusalimika hasa ikizingatiwa kuwa hakuwa anachukuwa tahadhari yoyote kujikinga na maambukizi hayo.
Hakuna ubisha kuwa Rais alikuwa mkaidi kupindukia na ukaidi huo ulitokana na kupenda sifa aonekana yeye ni "MWAMBA" na hatishwi na chochote hata kile kinachoitwa "korona". Lakini pia alifanya hivyo ili aonekana yeye ni mchamungu na kwamba Mungu angemlinda na maradhi hayo.
Kwa misingi hii ni heri kwa Rais na seririkali wabebe LAWAMA hizi za wananchi kwa kuficha ukweli kuliko FEDHEHA ya kutangaza kuugua kwani kivyovyote vile ingeaminika kuwa maradhi hayo ameambukizwa na wasaidizi wake kutokana na ukaidi wake na kwamba korona ni mshindi dhidi ya misimamo ya serikali.
Ni hivyo tu.
Kwahyo kumbe alipokua haonekani alikua anaumwa na kulazwa then akaruhusiwa kwa ajili ya recovery? Sasa kwanini aliruka fact kwamba KWELI ALIUMWA ila AMERECOVER??Si umeambiwa tarehe 7 aliruhusiwa kurudi nyumbani kisha alirudishwa hospitali tarehe 13?
Kwenye taarifa ya VP alisema Rais aliruhusiwa kutoka hospital trh 7 na aliendelea na kazi zake kabla ya kuzidiwa tena, Kwa hiyo PM alikuwa correct aliposema kuwa Rais anachapa kazi zake hakudanganya wakuu unless kama tulichopewa kwenye taarifa siyo sahihi lakini kama ndivyo PM alisema kweli
Only in Banana Republics,Kumbuka Trump alipougua covid19 mambo yakawekwa hadharani mpaka dawa alizopewaFor security purposes state ya ugonjwa wa Rais inakuwa confidential saa nyingine hata Waziri Mkuu sio lazima ajue au aliongelee and especially kwa nchi kama hii ya Tanzania ambayo kila kitu kila saa ni siasa tu
Wanabodi najua kabisa tupo kwenye msiba mkubwa. Msiba ambao umemgusa kila mtu na mpaka sasa kila Mwananchi haamini kilichotokea.
Lakini yapata kama wiki moja iliyopita taifa zima lilikumbwa na taharuki kubwa. Kila raia mwenye mapenzi na mkuu wa nchi yetu alitaka kujua kama anaumwa au haumwi. Wapo waliojitolea kuwa wapiga mbiu. Wao walisema kuwa Rais anaumwa na yupo hoi
Ghafla akaibuka Waziri mkuu akiwa ziarani huko nyanda za juu kusini. Alitoa tamko ambalo sababu yeye ndio msimazi wa shughuli za serikali kila mwananchi alimuamini. Aliwahakikishia watanzania kuwa Rais haumwi na anachapa kazi kama kawaida.
Tamko la Waziri mkuu kuwa Rais alikuwa mzima linakinzana na taarifa tuliyopewa na makamu wa Rais kuwa tangu tar 6 March Rais amekuwa mgonjwa tena aliyekuwa amelazwa.
Je, kwa hali ya kawaida kuna raia ambae bado anaweza kumuamini Waziri Mkuu tena?
[/QUOTE
Na ajiuzuru tu sisi angesema mapema tunfafanya maombi Taifa zima angepona Rais wetu...
Kassim Majaliwa kwa kusema uongo amepoteza imani kwa wananchi kwani kwa kusema uongo itakuwa vigumu kwa wananchi kumuamini kwa lolote lile atakalosema!! He has lost credibility; kwa busara tu naona angepisha mou mwingine achukue nafasi yake, asipofanya hivyo atakuwa kituko mbele ya wananchi popote atakapo fugua mdomo wake!Tena kibaya zaidi, kadanganyia kwenye nyumba ya ibada (msikitini)... shame on him... 🚮
Security purposes zinalazimu ugonjwa wa Rais uwe siri kwa nini?For security purposes state ya ugonjwa wa Rais inakuwa confidential saa nyingine hata Waziri Mkuu sio lazima ajue au aliongelee and especially kwa nchi kama hii ya Tanzania ambayo kila kitu kila saa ni siasa tu
Huelewi kitu wewe, kubishana na wewe ni kupoteza mudaSecurity purposes zinalazimu ugonjwa wa Rais uwe siri kwa nini ?
Tutavamiwa na maadui tukiwa na Rais mgonjwa ????
Basi alipokufa wangeuchuna wamuapishe Samia kisiri siri the same freaking night ili kusiwe na power vacuum for security purposes...
Haya sasa kafa, hatuna rais, mbona tuko njema ??????
Kudanganya umma for security is total nonsense, such foolish argument!
Kwa lipi alilolifanya?J Makamba anafaa kuwa PM
Tanzania sio US, wa TZ mnapenda sana kujilinganisha na mataifa yenya ustaarabu tofauti, uelewa tofauti nasi. Huku kwetu watau wanadanganyika kwa urahisi, wanaogopa kwa urahisi na nchi kuingia kwenye sitofahamu ni rahisi mno. Mnataka mfafanuliwe kila kitu kama watoto wa nursery?Only in Banana Republics,Kumbuka Trump alipougua covid19 mambo yakawekwa hadharani mpaka dawa alizopewa