Waziri Mkuu ( Premier ) Kassim Majaliwa nadhani GENTAMYCINE nilishakushauri hapa hapa JamiiForums kuwa kukiwa na Taharuki yoyote au Tukio lolote lile la Kihisia usipende kuwa na Kiherehere cha Kulisemea kwani Kirekodi una Gundu kwani kila ukijitokeza Kutetea Jambo fulani kwa dhana ya Kulificha huwa linakuumbua na hatimaye Kudharaulika, Kuchekwa na Kutoaminiwa tena.
Premier Kassim Majaliwa jana Umesikika na Kunukuliwa mahala ukisema kuwa Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isidori Mpango yuko mzima na nje ya nchi anafanya Shughuli zake za Kiutendaji na Kiuwajibikaji.
Premier Kassim Majaliwa Mimi GENTAMYCINE sina tatizo na hii Taarifa yako ila Kinachonishtua zaidi ni kwamba hata kwa Hayati Dk. Magufuli Uvumi wa Kifo chake ulipoanza na Kuenea kwa Kasi ndani na nje ya Tanzania kama kawaida yako ya kuwa na Kiherehere ulijitokeza na Kutuambia kuwa yuko ni mzima wa Afya, ulizungumza nae, anakunywa Chai Ofisini huku akipitia Mafaili yake wakati kumbe tayari na zamani sana alishakuwa amelazwa katika Mochwari ya Hospitali mbili tofauti kabla ya kupelekwa katika Mochwari ya Wanamedani wa kati ya Kawe na Mwenge.
Binafsi sikuamini tena Premier KMK.