Majaliwa alisema Rais Magufuli ni mzima anachapa kazi.

Kilichofuata ni historia.

PM Majaliwa hana ''credibility'' hana '' Integrity''.

Hata kama anasema kweli, PM alishapoteza uaminifu, kuaminika na uadilifu wa kiroho (moral compass).

Watu hawajadili kilichopo, wanajadili uadilifu, uaminifu na uadili wa PM kutokana na historia chafu ya siku za nyuma 'akiongea na marehemu'' . Hili jambo linahitiminisha ndoto yoyote aliyokuwa nay

Halafu alitoa kauli ya kuongea na marehemu akiwa msikitini, kitu kinachoonyesha hana hata hofu ya imani.

SSH ana msitiri sana !
 
Hivi mlitaka aseme kweli wakati Hali ya usalama wa nchi hajahakikishiwa na vyombo husika? Kutoa taarifa kama ya Jiwe lazima tujihakikishie kuwa usalama upo, mipaka imelindwa vema kiasi kwamba hakuna atakae Leta shida wakati wa maombolezo kama Yale.. Hivo Yeye sio muongo ila anafata protocol.. Mpeni heshima yake... Bwanaaa a!😁
 
Hakukuwa na sababu ya kudanganya vile, wangeweza kukaa kimya tu.

Unadanganya nini wakati rais anajifia zake na kila mtu atajua alikuwa anaumwa na mlidanganya?

Hilo linaonesha aliyedanganya si muongo tu, bali pia ni mpumbavu.
 
Majaliwa ni mpumbavu pia.

Alitakiwa kujua kwamba, kwa rekodi yake kwenye kifo cha Magufuli, hatakiwi kufanya kazi ya kuwapoza watu kuwa kiongozi wa kitaifa ni mzima.

Kama ulivyosema.

Majaliwa akisema kiongozi ni mzima, hata kama kweli mzima, kwa rekodi aliyonayo Majaliwa, watu watafikiri huyo kiongozi kashafariki au anafariki huko.
 
Wamarekani wana msemo mmoja.

"Fool me once, shame on you. Fool me twice, shame on me".

Ukinidanganya mara moja, lawama na aibu ni kwako wewe uliyenidanganya. Lakini, ukinidanganya mara ya pili, lawama na aibu ni kwangu uliyenidanganya tena, kwa sababu sijachukua somo uliponidanganya mara ya kwanza ili usiweze kunidanganya tena.

Sasa hivi hata kama Majaliwa anasema kweli, si mtu sahihi wa kutoa taarifa hizi. Kwa sababu tumeshakuwa fooled once.

Waswahili wanasemaje? Aliyeumwa na nyoka, akiona ujani, anashituka.
 
Hv watanzania hamna kazi za kufanya? Sasa kama mmeshaambiwa yupo anachapa kazi mnataka Nini. Kama anaumwa kama mnavyoamini na wao wanawaficha cha Nini kuhangaikia c mdili na mishe zenu za life. Mnajipa tabu Bure tu
 
Halafu hajui aongee wapi. Hili ni kongamano alilotakiwa kuhutubia, sasa akaingiza mambo ya mitandao ili kutoa taarifa inayomhusu VP na kwa historia yake chafu ya ''kuongea na marehemu'' , watu wana wasi wasi.

Sikuwahi kutilia maanani habari hizi, lakini baada ya kusikia Majaliwa anaongea nahisi kuna tatizo.
Majaliwa ana historia ya kuongopa, haaminiki hata kwa bahati mbaya.

Hata kama VP yupo katika 'majukumu' na akapita mahali na kununua Panadol, PM Majaliwa atabeba mizigo mizito sana mbele ya umma. Mtu anayekaimu Urais anapokuwa haaminiwi na Umma ni hatari
 
Zamani viongozi walikuwa wanaandaliwa, wanafundishwa hata jinsi ya kuongea, kujenga hoja, kujua miongozo ya serikali, kujua maadili, kujua mambo ya kimkakati, kujua mambo mpaka ya kijasusi, kujua mantiki.

Siku hizi ni kama wanasombwasombwa tu.

Kiongozi wa kitaifa au mkuu wa mkoa anaongea unaona huyu muhuni tu, mbabe tu, mjingamjinga tu.

Halafu watu wengine ndiyo wanashangiliaa.
 
Ni yule yule yaani !
 
Majaliwa hana tofauti na Tundu Lissu katika huu muktadha.

Lissu aliwahi kumzushia kifo mlinzi wa Magufuli katika kituo cha habari cha kimataifa na hakuwahi kurekebisha uzushi wake!

Majaliwa hayuko peke yake kwenye kusema uongo hadharani.

Sielewi kwa nini Majaliwa anasakamwa sana peke yake kana kwamba hakuna wengine waliowahi kuongopa hadharani kuhusu afya au uhai wa wengine.

Why does Tundu Lissu get a pass?
 
Sema ukiona huyu dingi katamka kitu kama hiki inabidi ukae tu kwa tahadhari maana baada ya hapo huwa zinakuja taarifa sio nzuri. Halafu kama VP yuko na majukumu si tungeona taarifa zake. Au VP hatembeagi na Camera man wala waandishi?
 
Angalao wewe umeongea kitaalamu, a realy great thinker
 
Naona unaelikea kumtaja arasii wetu wa daslam, mwamba kama mwamba
 
Naona unaelikea kumtaja arasii wetu wa daslam, mwamba kama mwamba
Jamaa huwa anajisifu kwa vitu vya kijinga sana.

Halafu wa chini yao wakiangalia mtu kama huyu anapewa promo, wanaona hivi ndivyo jinsi ya kufanya ili kupata promo.

Kwa hivyo, kama huyu asipoadabishwa, wanaokuja baada yake watakuwa na ujinga zaidi ya huu.
 
Huyu mtu ni mwongo sana si kiongozi wa kuaminika tena alitudanganya sana wakati wa JPM. Sasa kama yupo nje kuna siri gani? Aliondoka lini na yupo nchi gani kwa shughuli gani. Huyu hafai kabisa kumdikiliza na kumwamini na kwa kweli this time alitakiwa kunyamaza kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…