Waziri Mkuu anatakiwa ajiuzulu nafasi yake kwa kosa la kulidanganya Taifa kuwa Rais haumwi na ni mzima anaendelea na kazi zake. Kauli aliyoitoa tena akiwa "msikitini" ilikuwa ni "uongo" wa wazi na ni aibu kubwa sana siyo tu kwetu sisi Watanzania, bali hata kwa mbele ya jamii ya Kimataifa.
Kwa kosa la kusema "uongo" hadharani, tena ukiwa Waziri Mkuu wa nchi nafikiri ni kosa kubwa sana na anatakiwa ajiuzulu nafasi hiyo haraka iwezekanavyo. Tujiulize, ikiwa katika hili la "ugonjwa" wa Rais, tumedanganywa na Waziri Mkuu, Je, ni mangapi Serikali yake imetudanganya tusiyoyajua?