Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Wawekezaji njooni tuna umeme wa kutosha

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Wawekezaji njooni tuna umeme wa kutosha

 
Nimekuwa nimekuwa nikimsikiliza na kufuatilia maelekezo ya waziri mkuu kila mahali yanakuwa ya uongo au sio ya ukweli.
Mfano kwa sasa hakuna umeme anasema kuna umeme, mwenye kumwelewa tafadhali tukutane hapa.

9A42E223-E64E-4C44-B5B2-B6E9386A51ED.jpeg
 
Umeme upo imara na unaendelea kuchapa kazi🐒
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina ardhi, barabara na umeme wa kutosha.
Blaa blaa blaa tu lakini labda kweli kwake hakatiwi umeme yuko sawa tu hata barabara anasafishiwa tu hakuna foleni. Nchi ina vitu vingi tunaongea sana lakini uhalisia sasa fuatilia hayo ya uwekezaji kamasi zitakutoka. Kuna vijisera vya kijinga sana humo huwezi kumvuta mwekezaji halafu akaweka mamilioni hapo hapo ukamtaka alipie residence permit bei kubwa kuliko hata huko Dubai.

Wakati wenzetu huko wanawaita wawekezaji pesa ndefu na kuwapa uraia na wengine wanapewa residence miaka kumi sisi tunataka waje halafu tunajenga sera mbovu za kuvutia.

Badala ya hizi hotuba waaite wataalamu wapitie sera zote tuwe na sera bora kuliko nchi yoyote EA nchi nzuri watu watakuja. Mwekezaji kabla hajaamua kuja anatizama vitu vingi kikubwa faida na sera rafiki kupunguza cost. Hili nalo linaugumu gani kwa kweli?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina ardhi, barabara na umeme wa kutosha.
Kama aliweza kuwadanganya watanzania tena akiwa kwenye nyumba ya ibada kuwa Rais ni mzima na anachapa kazi wakati akijua kabisa Rais alikuwa kwenye dakika zake za mwisho za kupigania uhai wala usishangae kwa hilo
 
Blaa blaa blaa tu lakini labda kweli kwake hakatiwi umeme yuko sawa tu hata barabara anasafishiwa tu hakuna foleni. Nchi ina vitu vingi tunaongea sana lakini uhalisia sasa fuatilia hayo ya uwekezaji kamasi zitakutoka...
According to the World Bank's Ease of Doing Business 2020, Tanzania ranks below regional competitors with lower incomes per capita in terms of ease of doing business (Tanzania ranks 141 out of 190, Kenya 56, Uganda 116 and Rwanda 38).

Kwanini vi nchi vidogo nitaushinda nini sisi? tulitakiwa kuwa sisi tunawapa huduma tu wao hawa wadogo tuna nchi kubwa, watu, ardhi yenye rutuba, madini, Gas, sijui mbuga za wanyama tunakila kitu ila ni kama tunakumbatia hii hali achia watu wafanye kazi, walipe tax mzunguko wa pesa ije siku wawe wanakuja kutafuta kazi huku kwetu.

Serikali haitakiwa kuwa tajiri watu ndio wanatakiwa kuwa matajiri lakini tunatunga visheria vya ajabu ajabu utasema tumekuwa Dubai au huko USA. Tubadilikeni..
 
"Rais yupo anachapa kazi" mbaya zaid aliongea maneno haya akiwa msikitini kumbe mtu yuko mahutihuti anapumulia mashine alafu eti leo uamini anachokiongea thubutu!!!
Mkuu embu rekebisha hapo, yale maneno ya uongo wakati Majaliwa anayatoa tayari jiwe alikuwa ameshakufa siku kadhaa na tayari alishaanza kuoza huku tukifichwa.
 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina ardhi, barabara na umeme wa kutosha...
Mkuu labda akili yangu hainipi taarifa sahihi, Ila naona Kama tuna pm 3, wa Kwanza yupo bungeni, mwingine yupo kule anasema maji yazuiwe yasichepushwe halafu Kuna hyu hapa, Sasa kiukwel ninavulugikiwa kabisa,

Ila nyakati zile nlijua alikuwa Ni pm 1 tu,
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameendelea kutoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina ardhi, barabara na umeme wa kutosha.
Anayo haki kusema, hata Magufuli alipotoweka alisema yupo mzima. Nchi joto limepanda, umeme ata wa kuwashia fan hakuna. Nilipo jana ulikatika saa 12 jioni ukarudi saa 5. Leo umekati mara mbili na haujarudi. Maji tangu jana hayatoki, umeme hauna nguvu kuzungusha mitambo ya maji. PM hoyee!
 
Hivi bado kuna mtu anamuamini huyu jamaa mpaka piko?

Mpaka piko hafai kuwa hata mtendaji wa mtaa
 
Back
Top Bottom