Waziri Mkuu, Majaliwa amuwakilisha Rais Samia kumjulia hali Lowassa

Mungu ni wa ajabu sana, kama anavyomlinda siku zote na kila aina ya matamanio yenu maovu dhidi yake basi anaweza kuendelea kumlinda hadi mtakapoangamia nyie kwanza.......kila binadamu Ana mwisho though, kwahiyo mwisho wake haina maana kuwa ni mapokeo ya dua zenu nyie mashetani!
wazuri hawafi
 
MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

View attachment 2461149
Waziri Mkuu amekwenda kama kiongozi wa serikali kumuona mgonjwa; sidhani kama amemwakilisha Rais. Serikali yote imewakilishwa na Waziri Mkuu. Sana sana katika mazungumzo na familia anaweza kutoa salamu za rais.
 
Nyie familia nne wenye hila za kimadaraka, sasa hivi mnao lamba asai, mliomdhulumu haki yake huyu masai , Tunamwachia Mungu
 
MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

View attachment 2461149
Get well soon mzee wetu
 
Waadishi wa habari mko wapi mpaka kiongoziwa ngazi hii anaumwa , anaenda kutibiwa nje ya nchi sisi raia hatuna habari
Ugonjwa unalindwa na the right to privacy, familia ndio huamua ni wakati gani wa kutoa habari, hata ukijua, mfano mimi kutokana na close proximity na watu wake, tangu amepelekwa nilijua ila habari hizi zina kinga ya right to privacy, familia ilipoona sasa ni wakati muafaka kutoa taarifa, then ndio wametoa.

Hata yule Blaza, japo taarifa zilizuiwa kuna waandishi tulikuwa tunajua na hadi alinalii lini lakini tulinyamaza!.

Wakati fulani mimi nikitibiwa South, tuka happen kuwa hospital moja na kiongozi mmoja mstaafu, nikaleta taarifa humu JF, Timoth Apiyo Alazwa Afrika Kusini kilichotokea kwenye bandiko hilo, nilijuta na tangu siku hiyo ikawa ndio mwanzo na mwisho kuleta personal issue ya mtu humu JF, lakini na mimi pia kujifunza Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
P
 
Got well soon baba Yetu Edward Ngoyayi Lowassa. Bado kama Taifa tunakuhitaji mno. Mungu awatumie madakitari hao kukurudisha katka hali yako ya kawaida
 
Alikuwa PM na waziri mara nyingi tu, leo anaumwa anakwenda kutibiwa SouthAfrica, hawa raia aliokuwa anawaongoza masikini wakiumwa na wao wakatibiwe wapi?...

Angepigania Taifa kuwa na hospitali za kisasa na vifaa vya kisasa sidhani kama leo hii angekuwa SA kwenye matibabu..

Haya aendelee kutibiwa na kodi zetu tu, na PM kapanda ndege kwenda tena kumjulia hali kwa kodi zetu...

Alipaswa kulazwa muhimbili au mount Meru pale kuonyesha uzalendo kwa raia aliowaongoza.
 
Ugonjwa unalindwa na the right to privacy, familia ndio huamua ni wakati gani wa kutoa habari, hata ukijua, mfano mimi kutokana na close proximity na watu wake, tangu amepelekwa nilijua ila habari hizi zina kinga ya right to privacy, familia ilipoona sasa ni wakati muafaka kutoa taarifa, then ndio wametoa.

Hata yule Blaza, japo taarifa zilizuiwa kuna waandishi tulikuwa tunajua na hadi alinalii lini lakini tulinyamaza!.

Wakati fulani mimi nikitibiwa South, tuka happen kuwa hospital moja na kiongozi mmoja mstaafu, nikaleta taarifa humu JF, Timoth Apiyo Alazwa Afrika Kusini kilichotokea kwenye bandiko hilo, nilijuta na tangu siku hiyo ikawa ndio mwanzo na mwisho kuleta personal issue ya mtu humu JF, lakini na mimi pia kujifunza Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
P
Pascal Nimeelewa na ninadhani na wengine wataelewa pia
 
Watu wazuri hupendwa na Mungu na kwa ajili hiyo hufa mapema ili aende awatumie
Sijui wenyewe........yaani shauri zenu; mko huru, lolote lipendezalo au liletalo faraja mioyoni mwenu, liongeeni kutoka katika kauli hiyo
 
Back
Top Bottom