Waziri Mkuu Majaliwa, pokea makadirio yangu kibanda cha VETA Tabora

Huu ni mchanganuo tu wa ishu ya umeme, Hilo kwingine wajuzi wa hayo mambo wafafanua kwa maana nyingine Bei za huyu mdau za kipigaji, namaanisha hazikubaliki.
Kwa vigezo vya kiserikali vinakubalika. Hoja hapa ingekuwa jee vigezo vimezingatiwa kwa kufuata masharti ya ujenzi wa majengo ya Serikali?
 
Huu ndiyo ukweli. Serikali ina viwango vyake ambavyo kwa mitaani havitumiki na usipovifuata mradi unaweza usipokelewe!!
Wengi hawajui huo mradi utakaguliwa na watu wa PPRA, CAG n.k. Wote hao wataangalia specifications zimesema nini na ubora ulihakikishiwa vipi. Bila ripoti kutoka maabara ya kuthibitisha ubora wa tofali hauchomoki. Hapo matofali na zege vinapelekwa Tabora kupimwa.

Amandla...
 

Acha uongo ww, hapo kwenye bati utumie bati 38.. Kibanda cha bati 10 utumie bati 38.. Acha uongo, nilijua nitakunasa hapo kwenye bati..

Kibanda cha Tabora bati 10 tu, kila upande bati 5... Na bati bei yake ya mita 3.4 ni 47,600 yaani 14,000 kwa mita kwa bei ya serikali kutoka ALAF..!! So bati 10 za mita 3.4 = 476,000 tu

Kile kibanda kwa mil 11 nyingi mno, wizi uko wazi pale.
 
Kwa vigezo vya kiserikali vinakubalika. Hoja hapa ingekuwa jee vigezo vimezingatiwa kwa kufuata masharti ya ujenzi wa majengo ya Serikali?
Masharti ya ujenzi wa Serikali Yana utofauti gani na ujenzi wa kawaida ? Sababu kazi huwa tunafanya na Serikali haya masharti sijawahi kuyaona kwamba Kuna masharti ya ujenzi wa serikali na ujenzi wa usio wa serikali, masharti ya ujenzi wa serikali yanasemaje kuhusu usafiri ? Armoured Cable kwenda uyui usafirishe na Ndege au kwenye cable ya size ya 1.5 au 2.5 utumie 6 au 10 au 16 au 25 ?
 
Ndiyo maana nasema, Waziri Mkuu hakutakiwa kubishia tu gharama, bali alitakiwa ashauriwe kama mradi umefikia viwango au la.

Lakini hadi Mradi ukabidhiwe kwa serikali unakuwa ushakaguliwa na Mkaguzi aliyetuliwa na serikali na wa kutoka Serikalini. Hao ndiyo waulizwe walikubalije hizo gharama? Maana wao ni wataalam wa kukagua hiyo miradi, mkandarasi hausiki hapo.
 
Haya iwe Musoma huko migodini. Sisi haya ndiyo maisha yetu, Kuna muda watu wanapiga tu kwa ujinga wao ila kiuhalisia mambo hayako hivyo.
Watu hawapigi kijinga hivyo. Hiyo pesa yenyewe lazima ipitishwe na kamati kibao na kila mara inakuja kamati kukagua mradi. Shida yenu mnalinganisha miradi ya serikali na miradi ya watu binafsi ambayo hailazimiki kufuata viwango vilivyowekwa na washauri wa serikali.

Amandla...
 
Hapo no 28 kufanya wiring umeme 650000 kwa hicho kibanda !!?hapana gharama za hivyo kwenye umeme hata kama utakiwekea a/c

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Sema vyovyote upendavyo. Gharama za ujenzi wa majengo ya serikali na ya ujenzi wa nyumba zetu mitaani ni tofauti kabisa. Ukijenga Jengo la serikali hela nyingi zinatumika kwenye kufuata Taratibu. Hiyo "Amoured Cable" mtaani unaweza kumpa kuli abebe na ukamlipa buku yakaisha. Serikalini ni lazima uthibitishe kwamba huo waya ulibebwa.
 
Tronic zimepitishwa na nani? Tangu lini umemtumia fundi mwenye diploma kukufungia umeme? Na hiyo diploma in electrical installation inatolewa na chuo gani?

Amandla...
Kijana hata utumie bidhaa za ABB au Panasonic au Legrande sababu Hawa hawazalishi Cable na hapo Cable ndiyo yenye gharama kubwa. Hicho kibanda umeme hauwezi zidi 2mil. Sababu hicho kibanda kitachukua socket mbili tufanye zote Twin Complete, switch light Moja complete, tuchukulie au tuwawekee Light Bulb za bei kubwa mfano Opple hazi zidi nne, nje na ndani.
 
gharama hizo ni kibanda au ni nyumba ya kulala wageni
 
Serikali ipi hiyo unayoifanyia kazi? Hamna mahali katika mkataba panaposema vifaa viletwe kwa njia gani. Kinachotakiwa ni kifaa kifike salama, kwa wakati na katika hali ya kutumika. Hapa unashupalia armoured cable ambazo hata hazipo katika hesabu ambayo mtaalam mwenzako ameiweka.

Amandla...
 
Haya tuseme umeme ni milioni 2. Kwa hiyo gharama inazidi milioni 14? Maana kibanda sio switch socket na wiring peke yake.

Amandla...
 
Sasa naongelea uhalisia wewe unaongelea upigaji. Tofautisha ujinga unao uongelea wewe na uhalisia.

Ndiyo maana nikakwambia hivi Kuna tofauti gani za kitaalamu zinazo tofautisha kati ya Serikali na Miradi ya watu binafsi ?

Sisi kazi zote hizo tumefanya za Serikali na nyingine zote na kazi hizi huwa zinafata Standard za kimataifa.

Sasa Jenga hoja kitaalamu na siyo kipigaji.
 
Haya tuseme umeme ni milioni 2. Kwa hiyo gharama inazidi milioni 14? Maana kibanda sio switch socket na wiring peke yake.

Amandla...
Sasa hizo gharama nyingine waache watalaamu wa hayo mambo waongelee sababu nao wameonyesha upingaji wa hizo gharama.
 
MUNGU akubariki sana
 
Suala la upigaji si umeleta wewe? Mimi nakwambia kihalisia hiyo gharama inakubalika kwa kibanda kilichojengwa kufuatana na matakwa ya serikali.
Standard za kimataifa ni zipi hizo? Nina wasiwasi kama kweli unajua unachozungumzia. Hasa kama haujui tofauti ya miradi ya serikali na ya watu binafsi. Mfano mdogo ni kuwa vifaa vinatumika katika mradi wa serikali vinatakiwa kupimwa na kuthibitishwa na taasisi zinazotambulika. Mradi wa serikali unatakiwa utekelezwe katika hali ambayo haihatarishi maisha ya wanaojenga na wanaopita njia. Miradi ya serikali inakaguliwa na taasisi mbalimbali. Vyote hivi vimaongeza gharama ambazo mtu binafsi haingii. Aidha kila gharama inatakiwa ihesabiwe katika mradi wa serikali wakati katika miradi yetu gharama nyingi hatuzihesabu ( muda wetu, usafiri wa gari la mjomba n.k.).

Amandla...
 
Hapa najadaliana na mtu ambaye hajui haya mambo. Mimi nimefanya kazi na Serikali na nafanya kazi za Watu binafsi na siyo nyumba binafsi.

Nipe Gharama ya kutoa Armoured Cable kutoka Kiwandani mpaka Uyui, Armoured Cable ya 100m ujue si mzigo mkubwa ? Sasa utaniambia sharti ni usafirishe kwa ndege au ?
 
Asante sana. Viongozi wanapaswa kupata ushauri wa kitaalaam kwa utulivu mkubwa kabla ya kuwa na jazba na kuishia kukurupuka.
 
Suala la upigaji si umeleta wewe? Mimi nakwambia kihalisia hiyo gharama inakubalika kwa kibanda kilichojengwa kufuatana na matakwa ya serikali.
Standard za kimataifa ni zipi hizo? Nina wasiwasi kama kweli unajua unachozungumzia.

Amandla...
Kiuhalisia nimekuonyesha na number nimekuwekea mfano tu kwenye umeme, hapo kibanda hicho kitategemea umeme kutokana na miundo mbinu iliyo wekwa kwenye hayo majengo makubwa.

Standard za kimataifa katika selection wa vifaa, kumbuka naongelea mambo ya umeme. Siongelei siasa za uchumia tumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…