Waziri Mkuu Majaliwa, pokea makadirio yangu kibanda cha VETA Tabora

Ukiskia wale mafundi au injinia akikujengea nyumba yako ikiisha na yake inaisha huko kwa gharama ileile ya nyumba 1 aliyokutoza ndio hawa sasa
 
Lakini hadi Mradi ukabidhiwe kwa serikali unakuwa ushakaguliwa na Mkaguzi aliyetuliwa na serikali na wa kutoka Serikalini. Hao ndiyo waulizwe walikubalije hizo gharama? Maana wao ni wataalam wa kukagua hiyo miradi, mkandarasi hausiki hapo.[/QUOTE]

Jamani!!! kwani hamko Tanzania? Hili "dude force account" Haliitaji wakandarasi
Hawa tulio wazoweya ,walio sajiliwa na CRB.
Hata yule fundi wako
anae kujengea mabanda ya sungura, anaweza kupewa hiyo kazi.
 
Kwenye huu mjadala angekua magu ndio kamaindi hicho kibanda ungekuta ni post za kusifia na kumwabudu tu, wanasahau tulipigiwa mikwara na kelele za hakuna kusafirisha makinikia nje lkn ilikua kiini macho bado ulienda na unaenda ulaya
 
Ingekua hela yako mkonon ungejenga yote hio kibanda? Maana ya kutumia force account ni nni? Lengo ni kubana matumiz.mbona katika hela hio umesahau kuweka supervision cost? Contingency cost nayo bei gan? Majenz ya hela za uviko zimetolewa na mh mama ziende zikaguse maisha ya watanzania
 
Miradi ya serikali si ya kwako binafsi.
Miradi ya serikali ina specifications za kuzifuata na ni kwa Tender-yaani kumkopa mzabuni na kulipa naadaye.
Kwa mtindi kama huo ndio maana kina Mwigulu wananunua V8 kwa Shs 500 milioni wakati yeye mwenyewe hawezi kunua kwa hela hiyo.
 
Tutoeni namba tena siyo porojo jamani, tunahitaji namba nyingi zaidi ilk tufanye comparison.
 
Ni kweli unaweza kujenga kibanda kama hicho hata kwa milion 100, ila kwanini ujenge kwa gharama kubwa wakati inawezekana kujenga kwa gharama ndogo na kwa ubora mzuri tu
Ubora unakuwa determined na specifications mlizojiwekea. BBQ inasemaje? Kama ilifuatwa na gharama ikawa 11m, then it is OK
 
Armoured cable kwenye kibanda cha mlinzi kuna item gani za maana zitatumika huko?
Mita 100 ni uwanja wa mpira , kwa nini ujenge kibanda umbali wote huo kutoka main panel?
Mkuu mbona vitu rahisi tunacgukulia kana kwamba hatujui maana ya kuandaa site plan kwa ujenzi wa taasisi Kama Chuo? Yaani unataka kibanda Cha mlinzi kijengwe katikati ya majengo kisa unapunguza gharama?

Lingine unatakiwa kuelewa ni kuwa, ujenzi wa Chuo Kama VETA hakijegwi kwa phase I na kumaliza majengo yote...Kuna sehemu lazima iachwe wazi kwa ajili ya future plan, hivyo Kuna sehemu zinabaki bila machengo kwa ajili majengo ya madarasa pamoja na workshops zingine kadri Chuo inavyozidi kukua.

Hizo sehemu zinazobaki wazi uwezi kupitisha miundombinu kama ya umeme au maji Safi au taka ni lazima ufuate site plan inavyoelekeza, hapo ndo utanikuta unatumia 10milioni kupeleka majisafi na maji taka kwenye kibanda kidogo sana Cha kukaa mlinzi.

Chukulia hicho kibanda kinatakiwa kiwepo simu ya mezani kwa ajili taarifa na Administration ambayo ipo umbali mrefu.

Pia chukulia kuwa Kuna plan ya kuweka umeme kwenye fence kupitia kwenye kibanda Cha mlinzi. Tukubali tu tunapenda sana kusema gharama kubwa kwa kuangalia kilichosimama Kama jengo bila kuangalia sababu ya gharama kuwa kubwa au ndogo.
 
Waziri mkuu kasahau kuwa gharama za ujenzi na vifaa vya ujenzi zimepanda juu, pia ni kama mheshimiwa hajawahi jenga nyumba au kibanda chochote kwa fedha zake labda anajengewa bure na Magereza au JKT Suma
 
Mkuu nadhani wengi hapa wanapanga vyumba au nyumba, gharama za ujenzi zipo juu sana, kuna mambo mengi na gharama zingine ambazo hata upange na kukadiria vipi zinajitokeza na ingekuwa choo cha shimo sijui wangesemaje, hawa watu wasitoe sana mapovu mbona sisi hatulalamiki hayo mashangingi wanayonunua kwa bei za ajabu kutokana na TOZO zetu.
 
Watu
Watu wanataka wajenge Chuo Cha VETA na kuweka mabomba ya class A yaje yapasuke ndani ya wiki mbili then waanze lawama...taasisi zetu hawafanyi ukarabati kwa muda hivyo lazima vitu vile genuine kwelikweli lakini pia plan ya eneo la ujenzi lazima ifuatwe ata kwa gharama ipi. Tuache lawama kwenye vitu vinavyohitaji utaalam.

Mwingine analaumu kisa nyumbani kwake sehemu ya kuweka nondo ya Y20 yeye anaweka Y10 then anadhani kuwa anaokoa gharama.
 
labda kwa Dsm lakini kwa Tabora gharama zako za kuchimba msingi, mawe, udongo moram, mbao ziko chini mno ukilinganisha na DSM. matofali mangapi??? manake kwa Tabora msingi wote jiwe linamaliza kazi mpka ngazi, flemu ya dirisha Tbr haifiki hata nusu ya 150,000 tena mninga karanga tupu, Bati na kofia 2.47 M kweli ndio mana nchi hii haiendelelei.

Ebu tupatie na hesabu kama kiband ahiki ni chako unamjengea baba mkwe wako wa Izimbili.
 
Mjenzi amekili kuweka hicho Cha 40,000.

Cha 300,000 umekiweka wapi?
Amekiri wapi? Liliulizwa swali katika kadamnasi kuhusu bei ya hicho choo na mtu akasema 40000. Hamna mahali ambapo huyo unayemuita mjenzi amekiri chochote.

Amandla...
 
Kuijengea serikali siyo sawa na kumjengea baba mkwe.
Serikali ina viwango vake.
 
Hili ni la msingi sana.
Hata estimates zangu nimereebisha kidgo kulingana na uhalisia.
Kibanda hich kweli chweza fika 16million.
Nawashukuru wana JF mnaoweza kuchambua mada kitaalam.
 
Kuijengea serikali siyo sawa na kumjengea baba mkwe.
Serikali ina viwango vake.
ndio tulinganishe sasa! wengi wetu tukisikia hizi namba tunalinganisha na hizi tunazojenga. Ila mbona kama ubora wa ujenzi binafsi kwa miaka hii 20 tuko juu kuliko huo mnaoongeza 0?!!
 
ndio tulinganishe sasa! wengi wetu tukisikia hizi namba tunalinganisha na hizi tunazojenga. Ila mbona kama ubora wa ujenzi binafsi kwa miaka hii 20 tuko juu kuliko huo mnaoongeza 0?!!
Kwa vile unajuakujenga, tafuta tender , kakope benki ili uianze kazi, ajiri hao mafundi wako na uwapeleke Tabora.
Ulete na vipimo vya viwango vilivyowekwa kwenye Tender.
Ulete na Tender Bonds za kazi.
Serikali itakushukuru sana kukukopa na ikulipe baada ya miezi 6.
Hii ni biashara huria karibu.
 
Wanajenga veta bwana mdogo, yaani mafundi na vibarua wanatoka ndaaani mbona hutaki kuacha kukalili uliyosoma shuleni??? Uyui hapa mawe ununui ni vpande vya kuni na kiberiti yanapasuka, mchanga uhitaji tipa. sie cement tu ndio inatupa shida. Acha kukalili kama wale wenzio waliofundishwa kulima tikiti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…